Friday, December 7, 2012

Ripoti Maalum Yafuta Vumbi la Kabrasha la Utafiti

Mdadisi ameguswa sana na ripoti maalum ya mwandishi wa habari, Daniel Mbega, ambaye ameifuta vumbi ripoti ya utafiti kuhusu migogoro ya yaliyokuwa mashamba ya NAFCO. Japokuwa kabrasha hilo limeandikwa kwa Kiingereza, mwandishi-mchunguzi huyu amefikisha ujumbe wake kwa Kiswahili tena kwa namna inayoweza kueleweka kirahisi. Fuatilia mfululizo wa uchambuzi wake katika viunganishi vifuatavyo:
"Wanaeleza katika ripoti yao ya The state of Nafco farms (Hali ya mashamba ya Nafco), kwamba, uuzaji wa Shamba la Nafco Kapunga ulikwenda sambamba na uuzaji wa Shamba la Mbarali ambalo tangu mwaka 1977 Nafco ilipolichukua kwa Wachina lilitambulika kuwa na ukubwa wa hekta 5,575, lakini lilipouzwa ikaelezwa kwamba lina ukubwa wa hekta 5,842, ikiwa ni ongezeko la hekta 267 ambazo hazijulikani zilikotokea" - Daniel Mbega

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP