Monday, May 28, 2012
Thursday, May 24, 2012
Surviving the African Identity Crisis at Harvard
Posted by
Chambi Chachage
at
5:49 PM
0
comments
Reactions/Hisia:
Zitto na Lwaitama: 'Denti' anapomsahihisha 'Ticha'
Hata hivyo bado Mwalimu wangu na Watanzania wengi wamejikita katika mjadala wa Serikali ngapi. Idadi ya Serikali inaonekana kama ndio dawa ya kero za Muungano. Ni kweli Wazanzibari wanataka uhuru zaidi na wengine hawataki kabisa Muungano. Unawalalia. Unawanyima uhuru wa kuamua baadhi ya mambo yao na japo halisemwi unawanyima wanasiasa wa Zanzibar mamlaka ya masuala mengine ambayo yangewafanya wajilimbikizie madaraka.
Kimsingi idadi ya wapinga Muungano inazidi kuongezeka siku hata siku. Ukiwauliza kwa nini hawataki Muungano wanasema aah, basi tu. Kama ni Mzanzibari atasema Tanganyika wanatutawala. Kama ni Mtanganyika atasema Wazanzibari wamezidi kelele, tunataka Tanganyika yetu. Sisi ‘Unionists’ (Wanamuungano) nao hatuna majibu ya kuridhisha sana na ya kukonga nyoyo. Isipokuwa tu, Muungano huu ni wa aina yake Afrika na Duniani. Ni alama pekee ya kuonyesha Mwafrika kupinga mipaka ya kikoloni. Sasa hili haliwaingii kichwani ‘secessionists’ (Wanautengano) na hatuna la kuwasaidia. Lakini ni lazima tuurekebishe Muungano huu. Ulivyo sasa utavunjika tu. Kuulinda Muungano ni kuufanyia marekebisho makubwa. Mwalimu Lwaitama kaliona hilo. Pendekezo lake liboreshwe sasa. Sio rahisi sana.
Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye Wajumbe wasiozidi 101 pamoja na Rais wa Bunge la Muungano. Wabunge wa Muungano watatoka kwenye mikoa (au Majimbo kama sera ya Majimbo itakubalika). Kwa utaratibu wa sasa kila mkoa utachagua wabunge 2 mmoja mwanamke mmoja mwanaume kwenda Bunge la Muungano. Wajumbe wa Ziada watatokana na uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata kwenye kura za Rais wa Muungano. Idadi hii yaweza kupunguzwa na hata kuwa na Wabunge 51 tu akiwemo Rais wa Bunge la Muungano ambapo kwa mikoa ya sasa kila mkoa utachagua Mbunge 1 na wengine watokane na uwiano. Rais wa masuala ya Muungano atakuwa Mkuu wa Shughuli za Serikali katika Bunge la Muungano na Rais kwa mwaka mara moja atahutubia Baraza la Taifa (Wabunge wa Bunge la Muungano na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka kila upande wa Muungano). Wazungu wanaita hotuba hii ‘State of the Union’ (Hali ya Taifa) na wengine huita ‘Queen’s Speech’ (Hotuba ya Malkia).
Posted by
Chambi Chachage
at
4:48 PM
1 comments
Reactions/Hisia:
Wednesday, May 23, 2012
How far can artists and their detractors go?
Posted by
Chambi Chachage
at
6:07 PM
1 comments
Reactions/Hisia:
Tuesday, May 22, 2012
Ihefu hadi Ikwiriri: Majuto ni Mjukuu?
Sijasoma yote yaliyoandikwa katika mjadala huu wa Wanabidii lakini nina machache ya kuchangia kuhusu suala la Ikwiriri kwa kuwa ni eneo ambalo nimekuwa nikifanya kazi za utafiti kwa muda mrefu sasa.
Takriban miaka mitano mpaka kumi iliyopita hakukuwa na mfugaji wa ng'ombe hata mmoja. Wengi wa wafugaji ni wa kabila la wasukuma ambao wamehamia toka Ihefu. Tukumbuke serikali iliwafukuza/kuwahamisha Ihefu kinyume cha taratibu na kuwanyang'anya mifugo baadhi yao waliochelewa kuondoka. Walitakiwa kwenda maeneo tengefu ya Lindi na Mtwara na kwingineko. Maeneo tengefu mengi hayafai kwa ufugaji kwani hayakutengwa kwa kuzingatia mahitaji ya wafugaji: maji, malisho na huduma za kijamii. Hivyo wafugaji wamelazimika kubuni mbinu zao za kuweza ku-survive in the absence of effective structural, infrastructural and institutional support systems from the State.
Hali ikoje: Kwa kuwa hakuna kanuni nzuri za kuhakikisha kuishi kwa pamoja baina ya wakulima na wafugaji na kwa kuwa shughuli zao haziendani, kwa maana ya kwamba wanyama wa wafugaji wanaharibu mazao ya wakulima, hitilafu zilipotokea, wananchi (wakulima na wafugaji) walikimbilia ofisi za serikali za vijiji na polisi kuweza kupata usuluhishi. Kesi ziliongezeka mno. Polisi wetu na viongozi wetu wa vijiji, kata, tarafa na wilaya tunafahamu kuwa hawalipwi vizuri na serikali. Wafugaji ambao huwa wana uwezo bora kimaisha na kifedha kuliko wakulima katika maeneo ya Ikwiriri walianzisha mchezo mchafu wa kuhonga polisi na kuwabambikia kesi wakulima kuwa wao ndio wavurugao amani.
Nina mifano kadhaa kutoka kwa wananchi wengi niliopata kuongea nao. Mfano: Mzee XX amekuta mifugo shambani kwake na kuanza kujibizana na mfugaji YY kufikia hatua ya kutaka kupigana. Mkulima XX anatamka kuwa ni lazima suala hili alifikishe kunakohusika. Mfugaji YY anachukua pikipiki na kuwahi Ikwiriri police post. Mkulima XX anafika polisi, anakamatwa kuwa ametishia uhai wa Mfugaji YY na mifugo yake. Anawekwa ndani kwa muda ambao polisi wameamua wenyewe.
Nikitumia taarifa halisi ambazo si rasmi kwa kuwa hazijatolewa na vyombo vya usalama (polisi) lakini nimezipata toka kwa jamaa zangu waishio Ikwiriri:
Mapigano ya juzi ni kilele cha ugomvi ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka kadhaa sasa na wakulima ndio wamekuwa waathirika wakubwa. Huyu Mzee alieuawa Ijumaa aliwahi kutoa taarifa kuhusu wafugaji kuingiza mifugo shambani kwake mwaka jana. Alikamatwa na kuwekwa ndani. Alipotoka aliendelea kudai haki yake kwa kwenda mahakamani. Alishinda kesi mahakamani na mfugaji mhusika alitakiwa kuondosha mifugo yake mara moja. Lakini hakufanya hivyo kwa kuwa mahakama si yenye kusimamia migogoro ya wakulima na wafugaji on a daily basis but ni polisi, hivyo mfugaji aliendelea kuhonga polisi.
Siku ya tukio, mkulima mzee wa miaka 60 alikuta mifugo shambani kwake na kuanza kujibizana na wenye mifugo. Wafugaji walipiga kelele na kuchukua marungu, mapanga na silaha nyinginezo wakampiga mpaka kumuua yule mzee. Ina lillah wa in illaih rajiun! Wananchi wakaenda kutoa taarifa polisi Ikwiriri. Kwa mujibu wa wananchi, hawakupendezwa na namna polisi walivyolishughulikia suala hili. Waliona kuwa polisi wamechukulia kana kwamba kimekufa kiji-mnyama tu kidogodogo na si binadamu tena wa miaka 60 ambaye alishinda kesi mahakamani kuhusu mgogoro uliopelekea mauti yake. Wananchi wakulima wakasema "enough is enough".
Wakazifunga barabara za kutoka Lindi na Dar na kuanza kushambuliana na wafugaji. Kwa kuwa wafugaji waliompiga na kumuua yule mzee ni wa kabila la kisukuma, wakulima walilenga kuwashambulia wasukuma irrespective ya kuwa ni wafugaji ama la. Maduka, magari, nyumba na mali nyinginezo zinazomilikiwa na wasukuma zimechomwa moto. Polisi mmoja wa kabila la kisukuma amechomewa nyumba yake kubwa yenye wapangaji kadhaa kwani wananchi walimtuhumu kuwa huwa anawasaidia wasukuma wenzake.
Wakulima wa Ikwiriri nilioongea nao kwa simu wanahoji kwamba: kwa nini vyombo vya habari na jeshi la polisi wametoa takwimu za wafugaji waliojeruhiwa na kuharibiwa mali zao lakini hawajasema kuhusu WANANCHI WAKULIMA WA KABILA LA WANDENGEREKO WAWILI WALIOUAWA KWA RISASI NA MFUGAJI WA KABILA LA KISUKUMA SIKU YA MACHAFUKO? Kwao wao, wanadai kuwa hii bado inalenga kumkandamiza mkulima hasa wa kabila la kindengereko (nimetaja makabila kwa kuwa wao walioniambia wamesisitiza katika maandiko nifanye hivyo ili ichangie kuonesha ukandamizaji wa kabila la wandengereko. Mimi si mndengereko wa silazimishwi kufanya wanavyotaka wao, bali nimeona nifanye hivi kujibu hoja ya mmoja wa wachangiaji aliyehoji kwa nini ukabila umekuwa "issue" katika suala hili.)
Sasa hivi hali bado ni mbaya kwani Wandengereko wamedai hawawezi kuendelea kuishi kwa kuonewa na wasukuma, hivyo wasukuma waondoke. Hii ndio hali halisi kwa vyanzo nilivyoweza kuvifikia mimi. Maswali ambayo yameulizwa kuwa wafugaji waende wapi na ni nani mwenye haki zaidi ya ardhi, mkulima au mfugaji? Majibu yangu ni kama ifuatavyo:
Serikali ilipaswa itambue mahitaji ya wafugaji kama vile kutenga maeneo yenye malisho na maji ya kutosha na kuweka miundombinu ya kukidhi mahitaji hayo. Namna ambavyo serikali inaachia suala hili liwe baina ya wakulima na wafugaji ndicho chanzo kikubwa cha migogoro. Vijiji vingi vya Ikwiriri, Lindi na Mtwara vimeshurutishwa na serikali kutengeneza mipango ya matumizi bora ya ardhi ikiwemo kutenga maeneo ya wafugaji. Wananchi hawa hawana uzoefu na ufugaji na hivyo hawajui mahitaji maalum ya wafugaji. Kwa mfano, katika Kijiji cha Mavuji wilayani Kilwa, wananchi wametenga eneo la malisho ambalo liko milimani ambao mifugo haiwezi kutembea kwa urahisi. Mipango hii ya matumizi bora ya ardhi imetengenezwa bila ushiriki wa wafugaji kwa kuwa hakukuwa na wafugaji katika vijiji husika. Halmashauri za Wilaya husika zilikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa mipango ya matumizi ya ardhi iliyotengenezwa imekidhi vigezo vya kitaalam ili kuepusha migogoro kama hii tunayoiona sasa. Kwa hali ilivyo sasa, tutegemee migogoro mingi kama hii kuibuka.
Tutaendelea kushughulikia matokeo mpaka lini ilihali vyanzo twavijua?
Mwandishi: Baruani Mshale
Posted by
Chambi Chachage
at
3:16 PM
0
comments
Reactions/Hisia:
Wakulima na Wafugaji Wanagombania nini?
Kinachoendelea ni watanzania kuzoea fujo na mapambano ya kumwaga damu taratibu na kwa uhakika. Ni kweli itafika sehemu, hali itakuwa mbaya kama juhudi za makusudi kuepusha haya haitafanyika.
Ni mara ngapi sasa wananchi wanaona Polisi ndio kikwazo? Juzi juzi wakulima wa korosho kusini walipambana na polisi. Si muda mwingi umepita wananchi walichoma kituo cha polisi kule Hedaru. Na sasa Ikwiriri!! Risasi, mabomu na mizinga haijawahi kushinda duniani. La sivyo Siria ingekuwa imetulia sasa.
Watawala amkeni!!!!"
Mifugo inalimbikizwa sasa kutokana na hela/mali inayopatikana Mererani na hapo Loboisirret kijijini kwa mfano kuna machimbo pia. Akitoka Simanjiro anaingiza mashamba ya Wapare Ruvu analisha. Mkulima Maasai wa Ruvu halishii shamba lake analolima. Ukiwa na silaha ya mkuki na mbio za kukimbia utaumiza wengine tu. Ila kiboko ya wote ni Waikoma wa Ikoma Robanda huko wanakuogopa hawaingii hovyo labda kuiba mifugo tu. Akiwa Naberera, Kitwai etc analishia katika shamba la mtu ambaye ni wa-kuja (Sio Maa). Kilimo siku hizi hata wafugaji ambao wamekuwa agropastoral wanalima ili wapate chakula wasiuze mifugo ili kununua mahindi. nani ambae haoni mashamba ya mahindi Ngwara, maharage, Monduli, Manyara etc. hata ndani ya ngorongoro ugonmvi kilimo kuongereza.
Kilimo cha mpunga katika majaruba na cha mahindi, kunde Bunda, Geita, Nyanza etc huko Usukumani asiyekiona nani? lakini wanapotaka utajiri kwa kulimbikiza mifugo kuiondoa makwao wakafuge kwingine hulishia mashamba ya wanyonge. Wengine watembeao na mifugo ni vibarua analipwa mfugo kwa miezi ya kuchunga. Mfugaji wa Kisukuma akifika Kigamboni, Rufiji, Mkuranga, Kilwa, Lindi anaona misitu ilivyoshona ni kufyeka miti, kuchuma na kuuza mkaa ili apate chakula na matumizi, akipata fedha nyingi anapeleka kwao kununua mifugo kupata jina la utajiri bila ya kuangalia carrying capacity. Si anajua TZ unahanja na kuharibu popote kisha unahama unakwenda kuharibu kwingine?
Hata siku moja hutoona mfugaji akilishia mifugo shambani kwake lakini kwa mkulima au mtu si wa kabila lake atafanya calculated humiliation na ethnocentrism zao na kutesa wengine. Hata hapa DSM wenye mifugo hawalishii mashambani mwao. Ifike sasa kufuga na kulima sustainably iwe sheria; kuhifadhi ardhi na misitu iwe sheria; watu kuhama hama hovyo nje ya maeneo yao kwa kibali na mifugo isitembee kwa miguu inaleta matatizo; mifugo inayowekwa kwa siri na viongozi wa kata, vijiji kuruhusu wafugaji kukaa katika mapori kwa siri, kupitisha mifugo usiku mashambani wawajibishwe. Kwani wafugaji wanalishia mashamba ya watu usiku wa manane mtu anakosa food security. Kutoka Geita hadi Kilosa au Manyara hadi Mikumi National Park ni ufisadi na rushwa zinazoleta mauaji ya watu wasio na hatia. Vibibi haviruhusiwi kuokota kuni maeneo yao ya zamani eti sasa ni maeneo ya wafugaji waliohamia-kisiri. Kibibi kikienda kinabakwa.
Hayo mauaji ya Rufiji huko Kilwa na Lindi watakuwa wameshajiandaa hao wafugaji hawatopita kama ndio wameua na wanaelekea huko. Hiyo Rice bread basket area imekwisha hakuna kulima tena mipunga ni mifugo mashambani. Hata Uvuvi-wanaingia kuvua kwa mabomu kutoka maeneo yao ya mbali kwenda maeneo ambapo wavuvi wa huko wanalinda mikoko na masalia ya samaki. Kisha wavuvi wenyeji wakichoma vibanda ya wavuvi wahamiaji waharibifu wa mazingira ili waondoke-serikali inawakamata na kuwafunga (Kilwa Kisiwani).
Wanapoharibu mazingira yao kisha ni kuvamia maeneo na mashamba ya wawekezaji kwa visingizio wadhibitiwe. Tunapogawiwa maeneo ya mashamba ya serikali ya zamani tulime-lakini tunauza kwa wengine ambao wanajenga majumba za biashara badala ya sisi kulima kisha tunahamia barabarani ambako tunabomolewa.Ifike wakati kuwa, ukipewa ardhi marufuku kuiua mpaka miaka kadhaa ipite na usibadili matumizi bila kibali. Hii itaepusha watu kuuza ardhi na kulewea pombe hela kwa kisingizio cha kuhamia kwingine mapori yapo.
Uhamaji hamaji, ujambazi na mauaji, usalama mdogo vijijini inakera. watu hawatalima, hawatasoma, hawatakwenda hospitali, watachomeana nyumba haya mambo yatokomezwe.
Inakera.
Posted by
Chambi Chachage
at
2:00 PM
0
comments
Reactions/Hisia:
Monday, May 21, 2012
2013 PhD Applications Now Open at MISR
Posted by
Chambi Chachage
at
3:56 AM
0
comments
Reactions/Hisia:
Saturday, May 19, 2012
mtaji wa makampuni 45 kuinua kilimo kwanza ?
Posted by
Chambi Chachage
at
7:17 PM
0
comments
Reactions/Hisia:
Kisa cha Mahojiano ya Viongozi Wawili Wachumi
Posted by
Chambi Chachage
at
6:39 PM
0
comments
Reactions/Hisia:
Friday, May 18, 2012
How President Kikwete justified his trips in 2006
Posted by
Chambi Chachage
at
9:52 PM
5
comments
Reactions/Hisia:
Thursday, May 17, 2012
This is BIG News - Please PASS ON To Support the FIRST TANZANIAN TO CLIMB TO THE TOP OF MOUNT EVEREST
- sponsoring his climb by using the 'Just Giving' link on his blog wilfredmoshi.wordpress.com
- visiting his Facebook page www.facebook.com/MountEverestHandinHand and 'liking' him
- walking with him by keeping him in mind over the next few days
- e mailing this information and the attached Newsletter to your family and friends. Help us to reach as many people as we can in the next 4 days!!!!!
Wilfred is a certified KINAPA (Kilimanjaro Tanzania National Park) guide and holds a NOLS certification as a 'Wilderness First-Responder' (WFR) and 'Heart Saver CPR'. He completed Advanced Secondary School in Moshi and trained to become a computer hardware and software technician. Wilfred serves as the Technology Adviser for the Twende Pamoja Trust on a voluntary basis.
Posted by
Temu, A.B.S
at
11:36 AM
0
comments
Reactions/Hisia:
Wednesday, May 16, 2012
STICK TO AFRICA'S PLANS/ACHA AFRIKA IJIPANGIE
SIGN "Stick to Africa's Plans:
Posted by
Chambi Chachage
at
4:39 PM
0
comments
Reactions/Hisia:
Sunday, May 13, 2012
Toa Kitabu Kisomwe-Utata wa Uhuru wa Kifikra
La kwanza ni mahusiano kati ya kupatikana kwa vitabu na kusomwa kwa vitabu. Ingawa kampeni inasisitiza ``TOA KITABU KISOMWE`` haisemi ni kwa jinsi gani itahimiza, kushawishi na kusaidia kujenga tabia ya kusoma katika jamii husika. Ukosefu wa tabia ya kupenda kujisomea katika utamaduni wetu ni jambo linalolalamikiwa na wengi na lenye kuathiri uelewa na uwezo wa kifikra wa watanzania. Hili pia linaathiri ushindani wa watanzania katika Nyanja za kimataifa. Pale UDSM kuna maktaba kubwa tu na yenye vitabu vingi(vya kisasa?), lakini kuna wanafunzi wanamaliza mwaka bila kusoma hata kimoja. Hasomi kitabu labda aambiwe kitatumika kujibu mtihani. Hawa ni wanafunzi wetu wa elimu ya juu ambao, kwa kawaida, walitakiwa wawe ndio vinara katika kupenda na kusaka maarifa yaliyo katika vitabu (lakini wapi!). Hivyo kupatikana kwa vitabu hakumaanishi kusomwa kwake. Kupatikana kwa vitabu bila kuwa na mpango-mkakati wa kutatua tatizo la ukosefu wa tabia ya kujisomea kwa kiasi kikubwa vitaishia kwenye makabati na kuwa maficho ya mende, mazalia ya panya na hifadhi ya vumbi.
Katika kuelezea lengo la hii kampeni ya ``TOA KITABU KISOMWE``, mwandishi Mnyika anaandika:
Neno `Uhuru wa kifikra` linarudiwa mara kadhaa na Mnyika ingawa bila ufafanuzi. Je, kumpa mtu elimu ni kumpa uhuru wa fikra au kumuongezea uwezo wa kufikiria? Kimsingi, na kwa mtizamo wangu, hakuna mtu asiye na uhuru wa kifikra. Ila hoja ni unafikiria nini? Je, unachofikiria ni cha manufaa na kinachoendana na muktadha hata kukidhi ushindani? Nani alishaweza kumpokonya mfungwa uhuru wa fikra? Kujaribu na hata kufanikiwa kwa mfungwa kutoroka ni ishara kuwa alinyimwa uhuru mwingine wowote ila sio wa kifikra. Hata wakati wa biashara ya utumwa, watumwa, watu ambao hawakuwa na elimu na walioonekana kutostaarabika walipinga kunyanyaswa kwa kujaribu na hata kufanikiwa kumuua mmiliki wao, familia yake au kujiua wenyewe. Walijaribu kutoroka pia. Hii ni ishara kuwa walipokonywa vyote isipokua `uhuru wa fikra`. Kwangu mimi, Uhuru wa Fikra ni haki ya kufikiria. Haki ambayo hauwezi kumpokonya mtu yeyote, kwa njia yeyote mbali na kumuua.
- demere kitunga
Posted by
Chambi Chachage
at
4:27 PM
0
comments
Reactions/Hisia:
Thursday, May 10, 2012
THERE SHALL BE A DAY - WHAT DAY?
I dream of the day of peace and calmness,The day of prevailing truth and buried lies,The day of flourishing honesty, perfection and openness,A day when an innocent lamb survives slaughter,There will surely come that one day!When man and woman will walk truth,When child and old will sing kindness,When sick and healthy will embrace faith,When body and spirit will dance freedom,There surely will come that one day!Free to lead and free to preach,Free to speak, talk, listen and hear,Free of lies and distortions, but beneficiary of truth,Free of every wrong, but full of right,There surely will come that one day!A day when an innocent lamb survives slaughter,Amid the empty noise and aggressiveness,The day of peace in tranquility and humbleness,Whether I will be there or not is immaterial,But that day will surely come!For the record of my future presence or absence,Herewith the reassurance in my reiteration,"I vow to thee my country, all earthly things above,Entire and whole and perfect, the service of my love,"And I love you all, foes and friends alike!Omari Rashid Nundu
Posted by
Chambi Chachage
at
5:21 PM
0
comments
Reactions/Hisia:
















