Loading...

Friday, February 8, 2013

Kuvunjwa kwa POAC: Nini Hatma ya UDA, TANESCO n.k?

Taarifa kutoka Bungeni Dodoma zinathibitisha kuvunjwa kwa Kamati ya Kusimamia Mashirika ya Umma (POAC). Imeunganishwa na Kamati ya Mahesabu (PAC) na kumeundwa kinachoitwa Kamati ya Bajeti ikiwa na mara baada ya Andrew Chenge kuwasilisha ripoti iliyoelezwa hapo chini kabisa. Hili linatokea katika kipindi ambacho kuna hitaji kubwa la kufuatilia kwa undani ufisadi kwenye mashirika haya. Kama inavyoonesha katuni hiyo hapa juu safari ya kuelekea 2015 inazidi kuwa tete na tata. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
"Mwenyekiti wa kamati Mahsusi iliyoundwa na Mhe Spika kuishauri serikali namna ya kuongeza uwigo wa mapato Mhe. Andrew Chenge akimkabidhi Spika wa  Bunge  Anne Makinda ripoti yao. Kamati hiyo iliundwa na Mheshimiwa Spika kwa lengo ka kuaandaa Mapendekezo ya kuishauri serikali kuhusu kuainisha vyanzo mbalimbali vya Mapato ndani ya serikali yaliyo ya kodi na yasiyo ya kodi" - http://haki-hakingowi.blogspot.com/2013/02/taswira-kutoka-ofisi-za-bungespika-anne.html

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP