Loading...

Friday, July 12, 2013

Tangazo la Vodacom na Hatma ya Elimu Tanzania


Hivi tangazo linaloonesha mwalimu anafundisha halafu mwanafunzi anashangilia kupata ujumbe wa simu linatuma ujumbe gani kwa jamii?
---

DAN:
Wanafunzi (hasa wa sekondari na vyuo) ni kundi linalogombaniwa sana na makampuni ya simu. Kuna kampuni moja ambayo iliwashika wanafunzi na vijana mapema tangu 2004/2005 kwa kuwawezesha kupiga simu bure muda wa usiku baina ya mtumiaji mmoja wa mtandao huo na mwingine. Hata mimi wakati huo nilinunua card yao kwa sababu iliniwezesha kuwasiliana kwa garama nafuu sana. Nimekua na namba hiyo kwa miaka 8 sasa mbali na ukweli kuwa karibuni huduma zao zimekua duni na za gharama ni kubwa kuliko nilipojiunga. Siku hizi wananikata fedha hadi 5000 bila maelezo ya kueleweka. Na masiliano huwa mabaya mara nyingi. WAMENIHODHI. Nashindwa kuwahama maana namba yangu ni muhimu sana na ninayo moja tuu.

Wakati huo,hiyo kampuni husika ilijua kundi la wanafunzi liko katika kipindi cha MPITO. Hivyo lilitukopesha. Sasa wengi wetu limetuhodhi  na linatupora tuu. Na hiyo mbinu ilijenga ushawishi mkubwa kwa vijana wengi kununua kadi zao na hadi leo wamejikuta wanakuwa watu wazima na wamebaki nazo.

Naona kampuni nyingine zimegundua hiyo monopoly ya kampuni `niliyoitaja` hapo juu hivyo zinajaribu kuwavuta wanafunzi na vijana zaidi.  Hii ni vita ya mafahari,nyasi lazima ziumie.

Kwa mantiki hii,lengo katika tangazo tajwa ni zaidi ya hilo la bahati na sibu. Ni uthibitisho wa huo ushindani wa kutaka kuhodhi kundi la wanafunzi na vijana kwa manufaa ya kibiashara. Nia ya kutengeneza faida hapo haijali ujumbe/tafsiri ama ushawishi hasi unaoweza  kutokana na tangazo hilo. Atakayeponzwa nalo,hilo ni kosa lake. Shauri yake. Hiyo ndiyo neo-liberal ethic.

---

ALEX:
Mkuu nimekusoma vizuri ila heri wangeweka slogan tu....kama zile za kata wewe, sitaki kata wewe....!!

Ila kwenda na graphic ad na mwalimu mtu mzima kabisa amejaza maths formulas ubaoni ila anapuuzwa mhh....its kinda extreme.

They are so many alternative moral na ethical channels to tap the market they are targeting.

Tukiruhusu competition za kubomoa maadili kama hizi ziendelee sipati picha itakuwaje.

Waache hii ni wrong marketing campaign,hasa hasa wakati huu ambako maadili na elimu vimeporomoka sana (in my opinion).

Imagine then baadaye they come forward and donate books.....!!
----

STEPHEN:
Tajirika na vodacom.
---

ADAM:
Si tumeruhusu FEDHA ziwe msingi wa maendeleo!
---

EDWIN:
Haya ndIo matangazo yanayopotosha jamii kwa kuwafanya wanafunzi na vijana wa kitanzania waamini kuwa ELIMU HAILIPI WALA SI UKOMBOZI KATIKA MAISHA BALI MAISHA NA UKOMBOZI WA KWELI VIMO KATIKA BAHATI NASIBU ZINAZOTOLEWA NA MAKAMPUNI YA SIMU. Kama taifa lazima tulinde maadili na elimu yetu tusiruhusu UBWANYENYE NA UTAWANDAWAZI VITUHARIBIE TAIFA. Nilikuwa natafakari kuhusu tangazo hilo la mwanafunzi akiwa darasani mwalimu anafundisha mara mwanafunzi anaibuka na kusema kwa sauti nimeshindaaaaaaa halafu darasa zima wanampongeza na baadae mwalimu anauliza niliishia wapi wanafunzi wanamjibu kwa kusema ulikuwa umemaliza. Napiga picha na kuirudisha nyuma kwenye darasa letu SCIENCE 2 maarufu kama S2 pale Mwanza Secondari jijini Mwanza; nakujuliza hivi ingekuwaje? Napata jibu kwamba huyo mwanafunzi aliyeshinda angeadhibiwa vikali sana ikiwa ni pamoja na kufukuzwa shule.

Taswira ninayoipata katika darasa hili LA kwenye tangazo ni kwamba mwalimu anafundisha huku wanafunzi wanachat kwenye simu zao za viganjani ndo maana mmoja wao aliweza kubaini kwamba ameshinda na kwa midadi isiyo ya kawaida anaruka kwa sauti huku darasa zima likimuona mwenye bahati maishaini mwake. BINAFSI NACHUKUA WASAHA HUU KULAHANI MATANGAZO YA AINA HII KATIKA VYOMBO VYA HABARI.
---

EVARISTO:
Kama kawaida angalia hata tangazo la coca cola wakati dunia inahofu na majanga au inawaza juu ya kitu fulani Afrika inabirudika na coke, Africa haiwazi. Na tangazo hilo ni yaleyale tu, yapo mengi sana ya ubaguzi wa rangi,  matabaka nk . Ndipo tulipofikia.
---

HILDERGADA:
Inamaanisha watoto wadogo wanakuwa na simu na huzitumia akiwa darasani. Hii ni kweli. Wazazi walichangamkie. Ukimuuliza mtoto atakuambia uongo-kaikota huko nje, alikuwa akijibana ukimpa hela ya nauli akanunua sm (mpunguzie nauli ni nyingi hela umpayo) etc. Wanafunzi wengine vibaka huibia sm watu; wengine huibia hela wazazi wao. Ukimtuma nyama kilo 2 ananunua moja na nusi au mbili kasorobo. Umtumacho-hupunguza ili akuibie hela (usiwatume kununua bulky items hata vijana wakubwa, kanunue mwenyewe bajeti ya familia). Ukizubaa home-anakuchomoa hela ukiisaka anasema hajui hajaiona kumbe ipo mfukoni kwake ili naye apate simu. Mradi sasa dunia imeharibika. Kuharibika mpaka kampuni sa sm kujisahau kuweka matangazo hayo. Ila shule nyingine-sm inatumika kuunganisha na video system kufanya masomo/kufundishia. Tuchague lipi linatufaa.
---

ALEX:
aani huwa kila nikiliona hili tangazo nakereka sana.

Linadhibitisha ni jinsi gani hatuko makini katika Elimu zaidi ya kufikiria 'kutengeneza hela' kwa kubahatisha,mkato

Ndio maana hata pale kiongozi fulani anapoteuliwa nchini au nje ya nchi kushika nyadhifa fulani utasikia magazeti yanasema XX AMEULA au AMEUKATA etc...

Hii inaonyesha jinsi gani tumeweka mbele Hela za kubahatisha na kupenda njia za mkato.

Linapaswa kukemewa na kufutwa ikizingatiwa tunapiga kelele vijana wanaenda shule madarasa na majengo hayatoshi ila cha kushangaza mwaka huu kidato cha tano madarasa na mabweni ndio yamekosa wakukaa eti,hakuna wanafunzi wanaofuzu.

KIULA:
I see! Kumbe macho ya wanazuoni yanafanana sana! Siku mbili zilizopita hili tangazo lilinifikirisha sana hasa pale wanafunzi wanapomjibu mwalimu kuwa ..."ulikuwa umemaliza" wakati alikatishwa kwa kelele za aliyekuwa akishangilia kuwa ameshinda. Pengine linaakisi hali halisi iliyopo mashuleni na namna wanafunzi wa leo wanavyoichukulia elimu.
---

CHAGGAMA:
Labda voda washitakiwe kwa corrupt public morals.
Unlike cultural/tribal values/morals or religious institutions shule zinatengeneza coporate morals at an inclusivistic sense. Hivyo basi Watoto humtazama mwalimu kama role model which inadvertently corrupts public morals.
Labda mjadala huu utawafikia waalimu/ serikali na makampuni za simu.
---

NAMTASHA:
Samahani naomba niulize, je nchini kunayo coalition yoyote ambayo ingeweza kufuatilia na kukemea vitendo amabvyo vinazidi kuharibu mawazo, mtazamo na utamaduni wa Mtanzania kwa ujumla?

http://groups.yahoo.com/group/Wanazuoni/message/19734

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP