Loading...

Sunday, August 4, 2013

Rafu Katika Ushindani wa Shule za Biashara Afrika?

Nadhani sasa ule mpango mkakati mzima wa "Africa's Top Business Schools" at http://www.africanbusinessreview.co.za/top_ten/africas-top-ten-business-schools umeanza kukamilika. Na nadhani pia kama Graduate School of Business- UCT wameanza kuzunguka na zile shule nyingine za biashara sita kati ya saba za kwanza bora zitazunguka tu. Kwa hiyo huyu mwandishi Ms. Sheree Hanna alifanya makusudi kabisa kutokuweka "hyperlink" ya UDBS kwenye ile habari yake. Kwa sababu ukiona kazi za akina Olomi, Urasa, Lutashobya, Matambalya, Winneaster, Chijoriga, Assad na wengine wengi pale www.udbs.udsm.ac.tz utakuwa huna  haja ya kwenda Protea Hotel kuwasikiliza GSB ya UCT. 

Ukisoma vizuri maelezo yaliyotolewa kwenye kila shule ya biashara katika hizi kumi bora, utaona kwamba Ms. Sheree Hanna yupo kimasoko zaidi kuliko ukweli halisi uliopo kwenye zile shule nyingi za biashara za Afrika kusini. Ms. Sheree Hanna alipaswa kusema upimaji wa hizi shule za biashara ulikuwa na lengo gani, na wao wanafanya kama nani, na wanafanya kwa ajili ya nani. Na pia alipaswa kusema kwamba hizi shule zote za biashara zimepimwa katika vigezo vinavyolingana ambavyo ni 1,2,3...x, na utaratibu wa upimaji ulikuwa 1,2,3...y, na matokeo yake shule za biashara kumi bora Afrika tumepata ni hizi hapa  http://www.africanbusinessreview.co.za/top_ten/africas-top-ten-business-schools 

Nionavyo mimi hivi ilivyo Ms. Sheree Hanna na wenzie katika www.africanbusinessreview.co.za wamelinganisha nyanya na vitunguu katika makala yao hii. Na hawakuzitendea haki shule za biashara ambazo hazipo Afrika ya Kusini.0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP