Loading...

Monday, August 5, 2013

Soma Kukufikishia Kitabu Kipya cha Mabala Ulipo

Mkahawa wa Vitabu Soma @SomaMkahawani uko mbioni kuanzisha utaratibu wa kumfikishia mteja kitabu anachohitaji pale alipo. Utaratibu huo umepangwa kuzinduliwa rasmi juma lijalo. Maadam Wanazuoni kadhaa wametangaza nia ya kupata kitabu kipya cha Mwanazuoni mwenzetu Richard Mabala kiitwacho Run Free kilichoshinda Tuzo ya BURT ya mwaka huu, Soma Book Cafe itafungua pazia nacho.

Kama unataka kufikishwa kitabu hicho mpaka ulipo (ofisini, chuoni au karibu na mahala hapo), bei yake ni Tsh 10,500. Ila kama utaenda moja kwa moja kukinunua mwenyewe kwenye duka la vitabu Soma (http://www.somabookcafe.com) bei yake itakuwa ni Tsh 10,000.

Kama unataka kufikishiwa kitabu ulipo tafadhali tuma barua pepe yenye anuani yako na namba ya simu kwa: somabookcafe@yahoo.com

Wasalaam,

Timu Ya Vitabu Soma

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP