Friday, September 27, 2013

Book on Mining&Social Transformation in Africa


DOCTOR MKUNDE CHACHAGE

Wednesday, September 25, 2013

UJASIRIA-VIJANA NA UKABURU WA KIUMRI

UJASIRIA-VIJANA NA UKABURU WA KIUMRI

Na Mwl. Sabatho Nyamsenda

Sehemu mbalimbali za dunia hii zimewahi kutawaliwa na viongozi wenye sifa na tabia tofauti, na waliofanya mambo makubwa ya kuziendeleza nchi zao, na hata kuzibomoa. Afrika pia ilizalisha viongozi wa aina hiyo. Uwatajapo Kwame Nkrumah au Julius Nyerere unataja viongozi waliokuwa na ndoto za kujenga jamii zenye utu. Uwatajapo Bokassa, Mobutu, Idi Amin au Kamuzu Banda, unakuwa umetaja viongozi wakatili, vibaraka wa mabeberu, waliopora nchi zao na kuwatesa wananchi wao.

Lakini utu wa Nkrumah na Nyerere haukutokana na dini zao au makabila yao. Ulitokana na itikadi ilizowaongoza katika mapambano yao. Wote waliongozwa na itikadi ya Umajumui wa Afrika (pan-Africanism), itikadi ambayo ililenga kulikomboa bara la Afrika toka katika utawala wa kikoloni, na hatimaye kuliunganisha ili kuunda dola moja lenye nguvu. Uundwaji wa dola hilo ndio ungekuwa salama ya Afrika katika mfumo katili na wa kinyonyaji wa ubepari wa kimataifa (global capitalist system). Hivyo, kati ya nguzo kuu za Umajumui wa Afrika ni upingaji wa ubeberu. Sina hakika kama mtu anaweza kuwa mmajumui mzuri bila kuwa mpinga ubepari, na mpiganiaji wa mfumo mbadala wa uzalishaji mali na ugawanaji ziada. Ndio maana Nkrumah na Nyerere walikuwa pia wajamaa.

Kusema kwamba wote walikuwa wakiongozwa na itikadi ya Kijamaa na dira ya Umajumui wa Afrika hakumaanishi kuwa magwiji hawa hawakutofautiana. Ndani ya itikadi hizo mbili kuna tofauti nyingi. Lakini tofauti hizo zilikuwa ni za njia (means) za kufikia lengo (end). Lengo ni kuiunganisha Afrika, kujenga mfumo mbadala, na kupambana na kila aina ya unyonyaji, ubaguzi na ukandamizaji. Hivyo, mara kwa mara walipokutana, hasa katika mikutano ya nchi za Umoja wa Afrika walibishana juu ya namna ya kujenga dola huru la Afrika. Kamwe hawakutofautiana juu ya haja ya kuwa na Afrika iliyoungana.

Kwa bahati mbaya kizazi hicho cha viongozi wenye dira, na wanaoongozwa na itikadi pana kimeondoka. Tumebaki na watawala vibaraka, wanaopigania fursa za kupendwa na mataifa ya mabeberu na wanaoshindania kinyang’anyiro cha kuzirudisha nchi zao utumwani kwa kuvutia makampuni ya kimataifa kuwekeza katika nchi zao. Miongoni mwa vivutio hivyo vikiwa kutoa misamaha ya kodi, kuruhusu utoroshaji wa mitaji na faida, na kuwalazimisha wanyonge kuwapisha wawekezaji-papa hata ikibidi kwa mtutu wa bunduki. Taifa letu la Tanzania haliko nyuma katika hilo.

Nimetaja neno taifa. Je, ni sahihi kuiita Tanzania taifa (nation)? Kuelekea uchaguzi wa mwaka 1995, Mwalimu Nyerere alitumia jitihada kubwa sana kusisitiza kuwa sisi bado ni taifa changa. Na kwa kweli hatukuwa taifa. Tulikuwa mkusanyiko wa makabila mbalimbali. Vikabila hivi ndivyo vitaifa vyetu. Mwalimu alitolea mfano wa George Kahama alipokuwa katika ndege. Ndege ilipopata msukosuko akasema “My God! Lakini ilipotikisika mara ya pili akasema “Mungu wangu! Ilipotikisika zaidi Akasema “Mawee”! Kwa jinsi kataifa ketu kalivyo kachanga, alisisitiza Mwalimu, mtu akipatwa na msukosuko atasema, “Mawee”! Bado tuna damu ya makabila ndani yetu.

Lakini kwa Mwalimu, ukabila haukuwa usukuma, uzanaki au uhaya peke yake. Hata utaifa [kwa maana ya nationalism] pia ni ukabila. Mwalimu alisisitiza kuwa utaifa [nationalism] usioongozwa na itikadi pana ya Umajumui, ni sawa na ukabila katika ngazi ya bara la Afrika [Nationalism outside pan-Africanism is equivalent to tribalism at the continental scale]. Ndio maana Mwalimu alipinga vikali ukabila wa Utanganyika na Uzanzibari.

Leo hii Mwalimu angefufuka angeomba arudi huko aliko. Asingeamini kuwa kale kataifa kachanga sasa kameshakufa. Hakuna Tanzania tena: tunaimba nyimbo za Utanganyika na Uzanzibari. Labda angepigwa butwaa zaidi kuona nyimbo za Utanganyika zinapigwa zaidi, na safari hii madijei wakiwa wale “vijana wake” aliowakabidhi kuendesha taasisi yake, huku wacheza dansi wakuu wakiwa wanasiasa na wanaharakati toka asasi za kiraia. 

Udini, alioupinga kwa nguvu zote, sasa ndio umekolea. Bila shaka hata yeye angepokea ujumbe wa simu ya kiganjani toka kwa  wakristo wakiwabeza waislamu, au waislamu wakiwabeza wakristo. Ambacho kingemchefua ni kuona jinsi wanasiasa wanavyotumia madhehebu na misikiti kupandikiza udini ili wapate urahisi wa kuingia Ikulu!

Yumkini hayo yangemsikitisha na kumsononesha, lakini yasingemshangaza. Alikuwa ameyaona na kushiriki kuyakemea kikamilifu katika miaka ya tisini. Labda ambalo lingemshangaza lingekuwa ni aina mpya ya Ukaburu. Hii sio ile ya “Uzawa”, ambayo pia Mwalimu aliita “Ukaburu”! Hii ni aina mpya ya Ukaburu, na bila shaka Mwalimu angeiita “Ukaburu wa Kiumri”. 

Katika miaka ya mwanzo ya Uhuru, Mwalimu alipambana kwa dhati na Ukaburu wa Uzawa, uliolenga kutoa uraia na nafasi za uongozi na fursa za kiuchumi kwa watu wenye ngozi nyeusi peke yake. Akiwa Waziri Mkuu wa Tanganyika, Mwalimu alikemea hilo, katika Bunge la Tanganyika tarehe 18 Oktoba 1961:

Kama sisi Watanganyika tutaanza kusema kuwa watu wote wa Tanganyika ni sawa isipokuwa Wahindi, na Waarabu na Wazungu, na Wachina, wanaoishi Tanganyika tutakuwa tumevunja kanuni. Kanuni hiyo haitaturuhusu tuishie hapo. Kama uraia wetu utakuwa si jambo la utii wa nchi bali jambo la rangi, hatutaishia hapo. Tutaendela kuivunja kanuni hiyo, na nimeshasikia watu hapa wakifanya hivyo tayari. Nimesikia mara kadhaa… maneno ‘Waafrika Wazawa’. Wameanza kuwatofautisha Waafrika pia… ipo siku ambayo tutasema watu wote ni sawa isipokuwa Wagogo, isipokuwa Waha, isipokuwa waliooa zaidi ya mke mmoja, isipokuwa Waislam, n.k. Tutaendelea kuzivunja kanuni hizi”
“Unajua nini kinachotokea pale watu wanapoanza kuleweshwa na madaraka na kuanza kutukuza rangi zao, akina Hitler, ndicho wafanyacho. Unajua wananakopeleka ubinadamu, akina Verwoerds wa Afrika Kusini, ndicho wafanyacho… Hawa watu wanatuambia tubaguane kwa sababu ’ya mazingira maalum ya Tanganyika.’ Hiki ndicho Verwoerd anachosema ‘Mazingira ya Afrika Kusini ni tofauti’. Hoja hii hutumiwa na wabaguzi wa rangi/Makaburu”!

Leo hii wameibuka wanasiasa ambao kwa kila namna ni makapuku wa kisiasa na mbilikimo wa kiitikadi.  Wameona hoja pekee ya wao kuteuliwa kugombea urais katika vyama vyao ni kupandikiza sumu ya ubaguzi wa kiumri. Hoja hii haikuanza kama ubaguzi. Bali ilianza kama ujasiria-vijana, yaani utumiaji wa kundi la vijana kama mtaji wa kisiasa. Hivyo makaburu hawa walianza kupigania haki ya kupunguza umri wa kupiga kura hadi miaka 16, na kugombea urais hadi miaka 35. 

Muda ulivyokwenda ndivyo sura halisi ya ukaburu ilivyoibuka. Hoja ya umri wa kupiga kura ikafifia, ya umri wa urais ikapaa. Taifa zima likaingia katika mjadala ili kumwezesha mtu mmoja kutimiza ndoto ya kuwa atakuwa rais akiwa na umri chini ya miaka 40. Baada ya muda ukaburu halisi ukajitokeza: sasa wenye hoja hiyo wakadai kuwa mwaka 2015 watu wote waliozaliwa kabla ya 1961 wasiruhusiwe kugombea urais. Wanadai kuwa sasa ni wakati wa vijana. Wazee ndiyo chanzo cha matatizo, waiachie nchi kwa vijana. Ndani ya UVCCM pia wapo vijana wamebeba bango hilo: Rais awateue wao vijana kuwa wakuu wa wilaya na mikoa, na Chama kiwateue kuwa makatibu wa wilaya na mikoa kwa sababu wazee wameshindwa!

Na vijana wameimeza sumu hiyo. Wanakutana katika makundi yao na kupendekeza majina ya “vijana” wenzao kugombea urais. Wanaopendekezwa ni wale wale waliobeba hoja ya kupunguza umri na kuzuia waliozaliwa kabla ya 1961 kutogombea. Mmoja wao sasa keshaanza pia kuzunguka makanisani!

Kwa namna yoyote kinachopandikizwa hapa ni sumu ya ubaguzi – ubaguzi wa umri. Katika mfumo wa kandamizi na wa kinyonyaji tulionao, uliowafanya watu kupoteza matumaini, ni rahisi sana kupandikiza sumu ya aina hiyo na ikafanya kazi. Kama hoja ya leo ni umri, kesho itakuwa ni dini. 

Tuna hoja gani ya kumjibu atakayetushawishi kuwa nchi hii imetawaliwa na wakatoliki wawili na waislam wawili katika kipindi cha miaka 50 na hakujawahi kuwa matumaini? Kisha akituambia kuwa chanzo cha matatizo yetu ni hizo dini mbili, na kwamba ni wakati sasa wa kuwajaribu waprotestanti au wapagani, tutakataa? Akija mwingine akatuambia chanzo ni makabila yaliyotawala na kwamba sasa ni wakati wa kuwajaribu wahaya, wasukuma, wanyakyusa au wachagga tutakataa? Na, je atakayetuambia chanzo ni kutawaliwa na watu wasio na Phd za darasani? Na, vipi atakayesema kuwa chanzo ni kuwa marais wote walikuwa wanaume, na kwamba sasa ni wakati wa kumjaribu mwanamke?

Ukaburu wa kiumri, kama ulivyo udini, ukabila, ni mjadala uliolenga kununua hisia za wanyonge na kuwafanya wasihoji chanzo cha ufukara wao na kudadisi sababu za utajiri wa wenzao; waendelee kutawaliwa na kunyonywa na kijitabaka kilekile ambacho kinazidi kujizalisha (tena sasa kinajizalisha kinasaba); na wasiweze kujenga umoja ili kukipindua kijitabaka hicho kinachokumbatia mfumo kandamizi wa uliberali mambo-leo. Ni mjadala unaogusa hisia na kujaribu kuwafanya vijana wajione wao ni kundi moja, kundi linalounganishwa na umri. 

Ni kipi kimfanyacho kijana mlalahoi wa Nyamitwebili ajione kuwa yeye si sawa na walalahoi wenzake wenye umri wa zaidi ya miaka 40, eti kisa ni wazee? Halafu ajione yuko sawa na jamaa fulani wanaopokea milioni 1o kwa mwezi, eti kisa ni vijana? Ni wakati sasa wa wanyonge kuamka na kukataa itikadi na mirengo finyu inayokumbatia dini, kabila, nchi, chama.

Mwandishi wa makala haya ni mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma. Anapatikana kwa barua-pepe sany7th@yahoo.com

Friday, September 13, 2013

Steve Biko and the Fact of Blackness

"Without doubt, Steve Biko (18 December 1964 - 12 September 1977), the father of Black Consciousness Movement in South Africa, read ‘The Fact of Blackness.’ The title of his fifth chapter of his book ‘I write what I Like’ echoes the terms employed by Frantz Fanon i.e. "Black Souls in White Skin"? It seems that Biko (1996), like Fanon, reached that point that forced a black person, out of the quest for self-identity and self-determination to make himself known. That is it to affirm his blackness. He agreed with Fanon that blacks were suffering from an inferiority complex. It seems that he agreed with Fanon that a black man was not a man: “To a large extent the evil-doers have succeeded in producing at the output end of their machine a kind of Black man who is man only in form. This is the extent the process of dehumanization has advanced. Black people under the Smuts government were oppressed but they were still men…. All in all the black man has become a shell, a shadow or man” (Biko, 1996, pp. 28-29). But while Fanon (1986) advocated the liberation of the black man from himself, Biko (1996) decided to advocate black pride: “ the first step is to make the black man come to himself; to pump back life into his empty shell; to infuse him with pride and dignity…. This is what we mean by an inward-looking process. This is the definition of black consciousness” (Biko, 1996, p. 29). However, a close examination of the conditions that necessitates the emergence of black consciousness as well as the difficulty Biko had in defining who was black in South Africa reveals that Biko (1996) was aware of the same dilemma of black essentialism that faced Fanon. Now wonder his 7th chapter of ‘I write what I like’ is entitled ‘Fragmentation of the Black Resistance’" - 'FACT OR FICTION? A CLOSE READING OF FRANTZ FANON’S ESSAY “THE FACT OF BLACKNESS"'
---
Biko, S. (1996). I write What I Like; a selection of his writings. Randburg, SA: Ravan

Fanon, F. (1986). Black Skin, White Mask. London, UK: Pluto Press.

Sunday, September 8, 2013

Mama Kamm on Educating the Girl Child - 12/09/2013


Tuna ardhi na watu wa kutosha kuendelea?

Tuliwahi kuambiwa ardhi na watu wanahitajika ili tuendelee. Leo tumeongezeka hadi kufikia milioni 44+. Pia tunaambiwa kuwa bado tuna ardhi nyingi ndio maana 'inawekezwa'. Wapo wanahistoria wa uchumi wanaodai kilichofanya/kinachofanya tusiendelee kiuchumi ni mchanganyiko wa kutokuwa na nguvukazi ya kutosha (watu) ya kutumia ardhi 'tele' tuliyonayo n.k. Je, hili ni kweli? Nimeambatanisha makala inayochambua hilo.

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP