Loading...

Thursday, October 24, 2013

Buriani Profesa Lionel Cliffe

"Moyo yangu unalia katika kuwaletea habari hii yenye uchungu -  kamaradi profesa Lionel Cliffe ametuacha jana usiku. Amefariki dunia nyumbani kwake, South Yorkshire, baada ya ugonjwa wa muda mfupi. Mzee wetu aliwahi kurudi Tanzania mwaka huu wa 2013, kujiunga na tamasha la Mwl. Nyerere, na kurudi na mipango mingi kuhusu kuendelea na utafiti wa kihistoria kuhusu suala la ardhi [Arumeru]. Tutaendelea na kazi yako Lionel, tutakukumbuka daima" - Dakta Elisa Greco

"Poleni sisi sote. Tutamkumbuka Lionel daima. Ametuachia mengi katika maandishi yake, hususan kitabu chake na John Saul ambacho ni cha aina yake - a reference book. Tuendelea kumuenzi kwa kuendeleza kazi zake" - Profesa Issa Shivji

"Ni habari ya kusikitisha. Pamoja na mambo mengine, tutamkumbuka Emeritus Prof. Cliffe kwa mchango wake madhubuti kwa the Review of African Political Economy (ROAPE). Ametuachia mengi ya kujifunza mwanazuoni huyu nguli" - Dakta Mathew Senga

"Nimesikitika sana, tawi la kushoto la upande wa magharibi limedondoka. Ni tawi lililokuwa imara sana hasa wakati huu wa migongano ya kimaslahi kati ya wenyedunia na wakazi wa dunia. Apumzike kwa amani kamaradi" - Dakta Vicensia Shule

"Afrika na dunia tumepoteza mwanazuoni makini na mwenye mapenzi mema na watu wote wanaonyonywa/wanaonyanyaswa na ubepari katika hatua yake ya ukichaa ya utandawizi...Kila nilipokutana naye nilipata sababu tena ya kukukubaliana na imani ya kwanza ya  ya mwana TANU kuwa binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja. Hakuna kutoa machozi lakini inauma kupoteza ucheshi wake Lionel" - Mwalimu Azaveli Lwaitama

"Apumzike kwa amani, kama bahati tu nilipata fursa ya kuonana nae na kuongea wakati wa tamasha la Mwalimu Nyerere, shukrani kwa wadau wa tamasha kwa kunialika katika hafla ya jioni pale Rose Garden. Ilikuwa jioni nzuri kweli kuonana na makamaradi waliowahi kuipenda Tz na kutumika pia hapa, natumaini Kigoda kitatuandalia kumbukizi yake hapo Udsm bila shaka" - Bernard Baha

"Ni vigumu kuamini kweli katuacha.Tulikuwa ndiyo tunafikiri mambo mazuri ya kuyafanya lakini Mungu amempenda zaidi...Alitokea hapa Cape Town kuwahi Tamasha la Mwalimu na alinionea huruma nilipomwambia mimi nina safari nyingine .Tena, ana taarifa nyingi muhimu sana kuhusu Mwalimu... Ninatumaini mengi atakuwa amempatia Prof Shivji. Apumzike kwa amani" - Emmanuel Sulle

"How sad very sad. When I learnt he was ill some weeks ago I wrote to wish him well; he never replied.I wrote again-no reply. Rest in peace dear Lionel, the journey is over and you have come home" - Annar Cassam

1 comments:

chungeh November 12, 2013 at 6:08 PM  

I'm glad we met again in Dar es Salaam this year, 2013, and had a chance to chat about many things including cricket. As a member of the Yorkshire County Cricket Club his loyalties were misplaced, but a great chap nevertheless. Sadly we cannot bat forever at some point we have to take the field. But we enjoyed the company. One love

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP