Loading...

Tuesday, October 8, 2013

Overquoting/Underquoting/Misquoting Nyerere

"Japokuwa makala imeandikwa vyema na hoja imepangwa vizuri lakini, najiuliza, ni lazima tumnukuu Nyerere katika kujenga kila hoja? Historia ina wanafikara mashuhuri wengi tu wenye mawazo ya kipekee sana. Wengi wao wameathiri ustaarabu wa ulimwengu kwa kiwango cha juu sana. Vipi kuhusu hawa? Kwani Nyerere alinukuu kina nani? Au Nyerere ndio tiketi ya hoja zetu kukubalika? Just thinking aloud. Though I might have erred in the same way in the past but, I think, are not we overloading the Nyerere argument? Bila kumpotezea heshima Nyerere, tusijepoteza uwezo wetu wa kufikiri wenyewe kwa sababu yake. Yeye avuma anga hizi, lakini wengi wapo" - Charles

"Suala la nani wa kumnukuu hutegemea na mtazamo wa mwandishi husika, na approach anayoitumia. Juu ya Nyerere, nachelea kusema wala hanukuliwi sana kama unavyotaka kutuaminisha. Aghalabu fikra na mtazamo wake hupotoshwa mara kwa mara ili kukidhi mahitaji ya kisiasa. Mathalani, CCM na serikali wanamtumia kama mpenda “amani”, “umoja”, “udugu”, n.k. Hoja hiyo ikitumiwa kuwaambia wanyonge wasiibue minyukano ya kitabaka dhidi ya wawafukarishao. CHADEMA pia, na hasa Dk. Slaa, humtumia sana Nyerere kama msingi wa “uadilifu”, “uchapakazi”, “uzalendo”, n.k. Wazalendo wa Kizanzibari ndio wamepiga kambi kwa kumchana chana Nyerere na kuibua kila aina ya sura yake ya udikteta, ulaghai, ukandamizaji, chuki dhidi ya watu wenye asili ya kiarabu n.k. n.k. Ni nani anayemjadili Mwalimu kama mmajumui au mjamaa? Ni nani anayezichambua fikra zake kwa kina na hata kuzikosoa (bila kuongozwa na maslahi finyu ya kuingia madarakani)?" - Sabatho

"You can't evade to quote Nyerere's wisdom just because there are others. The issue could be whether what the author quoted is out of context or misinterpreted--you can make your case! Kwa nini aende kunukuu mbali ilhali kuna nukuu zinazoweza kueleza jambo husika na likaeleweka na jamii kwa upana wake. Sina hakika kama angenukuliwa Martin Luther King Jr kwa kirefu hoja ingebaki." - Edgar

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP