Wednesday, November 27, 2013

Waraka wa Mkakati wa Mabadiliko - Feki au Orijino?

Katika muktadha wa lugha nchini Tanzania, mtu anaposema 'feki' kwa Kiswahili, je, anamaanisha 'fake' kwa Kiingereza? Kwa mfano, wanafunzi wanaotafuta 'mafeki' kabla ya mitihani ya moko na ya taifa na kufanikiwa kuipata, je, wanamaanisha kuwa ni 'fake' kweli? Au wanamaanisha ni 'kopi' ya 'orijino' ama sehemu ya 'orijino'?

Ukiangalia na kusikiliza kwa makini maelezo katika kideo hicho hapo juu utaona kuwa kuna mstari mwembamba sana kati ya matumizi ya neno 'feki' na 'orijino'. Pengine wanatumia lugha ya wanafunzi wanaosema 'mafeki' wakimaanisha 'feki orijino'. Kama hivyo ndivyo, ina maana 'feki' lililosambazwa magazetini na mitandaoni ni dondoo tu ya kile kilichopo kwenye 'orijino'?

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP