Tuesday, December 31, 2013

MLIZINGATIA MAONI YA NANI, JAJI WARIOBA?

MLIZINGATIA MAONI YA NANI, WARIOBA?

· Tume imechakachua maoni ya Wazanzibari.
· Watu elfu 16 kuamua hatma ya taifa la watu milioni 45.
Na Mwl. Sabatho Nyamsenda

Ilikuwa majira ya saa 11 jioni, tarehe 30 Desemba 2013, muda mfupi baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kukabidhi Taarifa yake pamoja na rasimu ya pili ya katiba kwa marais wa Muungano na Zanzibar, simu yangu ya kiganjani iliponiashiria kuwa nimepokea ujumbe. Nikausoma: “Haujambo? Vipi, siku zako za mwisho zikoje?”  Rafiki yangu wa Kijerumani aliyekuja hapa nchini alitaka kujua nimejiandaaje kuondoka nchini siku chache zijazo kwa ajili ya masomo ya juu. Nami kwa uchokozi nikamjibu, “Unaulizia siku za mwisho, unanitakia kifo?” 

“Nilijua tu utasema hivyo”, alijibu. Kisha akalipua bomu ambalo lilinifanya nidondoshe machozi: “Nimerudi kutoka Zanzibar leo. Ni kuzuri, na watu wake ni wakarimu kama wa huku Dar. Ama kweli nchi yenu imebarikiwa. Mna kila aina ya utajiri, tangu maliasili hata umoja na ukarimu!”

Eti huyu ndugu angependa kuwaona Wabara wakijivunia rasilimali na vivutio vya Zanzibar. Bila shaka huko Visiwani pia aliwasimulia mengi kuhusu mlima Kilimanjaro na uzuri wa Bara na kuwaambia ni vyao. Maneno “nchi yenu” na “umoja” yalijirudiarudia akilini mwangu. Nilisikia mwili ukinisisimka, moyo ukanidunda, kijasho chembamba kikanitoka huku machozi yakidondoka. Mjerumani huyu alikuwa amenisimulia hadithi nyingi za kwao, na namna ukuta wa Berlin ulivyoangushwa mwaka 1989, na Wajerumani wakaiunganisha nchi yao.

Hivyo nikamjibu kijana huyo, “Labda hukukosea kunitabiria kifo. Hivi karibuni naelekea kufa kama Mtanzania, na kuzaliwa upya kama Mtanganyika. Ama kweli, sijui mlitumia uchawi gani kuturoga. Mpaka sasa tunatukuza mabaki ya ukoloni.” Akanipa matumaini, “Usikate tamaa rafiki. Wapenda Muungano endeleeni kupambana. Tanzania yenye marais watatu, na Afrika yenye marais 54 haina mustakabali katika dunia ya leo.”

Hebu nieleze, ewe msomaji wangu, ingekuwa wewe ungejisikiaje? Huyu ndugu sio Mwafrika. Ni Mjerumani. Anaihurumia Afrika kwa kuendeleaza siasa za utengano. Yeye anajivunia kwamba nchi yake imeungana, na wanapigana kuunganisha Ulaya. Huku kwetu ndio kwanza tunazalisha vi-nchi, halafu tukitegemea tutakuwa na nafasi katika dunia ya leo?

Pengine kilichoniumiza zaidi sio maneno ya heri toka kwa mzungu huyo. Ni maneno niliyoyasikia katika hotuba ya Jaji Joseph Sinde Warioba, wakati wa makabidhiano ya taarifa ya Tume. Kabla sijaichambua nitaomba tukumbushane kitu kimoja: Wakati wa uzinduzi wa rasimu ya kwanza, Jaji Warioba alisema kuwa uamuzi wa Tume wa serikali tatu ulizingatia maoni ya watu walio wengi. Baadaye, na hasa baada ya kugundua kuwa mabaraza ya Katiba yamejaa wajumbe wa chama tawala, alibadili msimamo na kusema kuwa katika rasimu ya pili uamuzi wa Tume hautaangalia tena uwingi wa watu bali uzito wa hoja! Alidiriki kuwaambia wajumbe wa mabaraza ya Katiba wajadili mambo mapya, kwani ya zamani yote Tume inayo na hakuna haja ya kuyarudia. Kwa maana nyingine, aliwatisha wajumbe kurudia suala la Muungano, huku akijua wazi kuwa masuala ya msingi kuhusu maisha ya wananchi kama elimu, maji, afya, ardhi, serikali za mitaa n.k hayakuwa masuala ya Muungano, na kuyajadili kwake kungetegemea muundo wa utakaoundwa.

Ilipotoka rasimu ya kwanza, tupo tuliohoji uhalali wa Tume kupendekeza serikali tatu. Je, ilifikiaje uamuzi huo? Ilizingatia maslahi ya nani? Maswali hayo yalikosa majibu kwani Tume haikuwa imetoa ripoti. Ni ripoti ya Tume ndiyo ingetuondoa katika giza.

Na sio kweli kwamba tume yoyote hufikia kutoa mapendekezo kwa kuzingatia idadi ya wananchi waliozungumza. Tume ya Nyalali ilipendekeza vyama vingi licha ya kuwa takribani ya asilimia 80 ya watoa maoni walipendekeza tuendelee na mfumo wa Chama kimoja. Hali kadhalika, Tume hiyo ikapendekeza serikali tatu licha ya kuwa watoa maoni wengi walitaka tuendelee na serikali mbili. Uzoefu huu unatuambia kwamba kazi ya Tume ni kusikiliza maoni na kisha kuyafanyia uchambuzi wa kina kwa kuzingatia hali halisi ya nchi na dunia pamoja na misukumo inayowafanya watu watoe maoni ya aina fulani.

Kwa uzoefu ambao nchi iliupitia kutokana na utawala wa kiimla wa chama kimoja pamoja na mabadiliko yaliyokuwa yakitokea duniani, haikuwa busara kuendelea na Chama kimoja hata kama ndiyo yalikuwa matakwa ya wengi. Lakini watoa maoni wengi ni watu ambao walikuwa wameaminishwa na chama tawala kuwa upinzani ni vita na uvunjifu wa amani. Tume ya Nyalali iliyazingatia haya ikapendekeza vyama vingi.

Je, Tume ya Warioba imezingatia hali halisi ya Dunia ya sasa? Imezingatia historia ya nchi za kiafrika zilizojaribu kuungana na kisha muungano kuvunjika? Imezingatia ukweli kwamba watoa maoni wengi kuhusu Muungano ni watu waliolishwa “sumu” na vyama vyao kutaja idadi za serikali (mbili, tatu, mkataba)? Je, iliona wimbi la kuvunjika kwa Muungano?

Na sio kweli kwamba Tume ya Warioba ilizingatia idadi ya wananchi waliotoa maoni. Hebu tuzichambue kidogo takwimu zilizotolewa na Warioba kuhusu Muungano. Kwa Tanzania Bara, waliozungumzia Muungano walikuwa 39,000. Kati yao, ni watu 27,000 tu ndio waliozungumzia Muundo. Na kati ya hao 27,000, watu 3,510 (au 13%) walitaka serikali moja, 6,480 (au 24%) serikali mbili na 16,470 (au 61%) serikali tatu. Kwa Tanzania Visiwani, waliozungumzia Muungano walikuwa 38,000 na ni nusu yao tu (19,000) waliozungumzia muundo. Kati ya hao 19,000, watu 6,460 (au 34%) walitaka serikali mbili, na 11,400 (au 60%) serikali ya mkataba, na watu 25 (0.001%) walitaka serikali moja. Katika mikutano ya Tume huko Visiwani wapo pia waliopendekeza serikali nne : ya Tanganyika, ya Pemba, ya Unguja na ya Muungano, huku wakisisitiza kuwa Muungano uwe kati ya Tanganyika na Unguja. Hao, idadi yao, Jaji Warioba kakwepa kuitaja!

Je, takwimu hizo zinatueleza nini? Ukijumlisha idadi ya watu ambao hawakugusia muundo wa Muungano, Bara na Visiwani, ni 31,000. Hawa ni wengi kuliko watu 16,470 waliotaka serikali tatu. Jumla ya waliotaka serikali moja na mbili ni 16,475, na idadi hii pia ni kubwa kuliko waliotaka serikali tatu. Tume inaweza kujitetea kuwa watakao mkataba wakikosa sana wanaweza kuhamia kwenye serikali tatu. Ukikokotoa jumla ya waliotaka mkataba na serikali tatu ni watu 27,870, na hawa ni 36%  (takribani theluthi moja tu) ya watu waliozungumzia Muungano. Na jumla hii ni kijitone cha maji baharini ikilinganishwa na watu wapatao 333,537 waliotoa maoni katika Tume ya Katiba. Pia hakuna utafiti wowote wa kisayansi unaoonyesha kuwa sampuli ya watu 16,000 inaweza kuwa inawakilisha maoni ya Watanzania milioni 45. Wanaweza kuwa ni watu wa wilaya au mkoa mmoja.
Katika lugha rahisi, ni kuwa waliotaka mkataba au serikali tatu walikuwa asilimia nane tu ya waliotoa maoni. Pia, watoa maoni 287,537 sawa na asilimia 86%  hawakugusia kabisa kuhusu Muungano au muundo wake. Je, uwingi aliousema Jaji Warioba kautoa wapi? Na kwa nini adanganye mchana kweupe?

Ni vema tukajifunza kutokana na mchakato wa Katiba mpya, ambao ulitekwa na Wajasiria-Katiba kutoka vyama vya siasa na asasi zisizo za kiserikali. Na mvutano  baina yao ndio ukateka mijadala na kufifisha maoni ya wananchi wa kawaida. Kuna wakati ambapo baadhi ya asasi zilitaka kwenda mahakamani kuusimamisha mchakato baada ya kuona kuwa umetekwa nyara na chama tawala. Chama kikuu cha upinzani pia kikatishia kujitoa na hata kumwandikia mjumbe wake barua ili ajitoe.
Lakini baada ya kunong’onezwa yaliyomo kwenye rasimu, wakafyata. Rasimu ilipotoka, hata kabla hawajaisoma wakaisifu na kusema imezingatia maoni ya wananchi! 

Sasa takwimu ndio hizo, je, ni maoni gani ya wananchi yaliyozingatiwa? Huko Zanzibar, hakuna kitu kinachoitwa serikali tatu: wengi hawakugusia muundo. Wowote utakaokuwepo kwao sawa. Kwa waliogusia muundo, wengi wanataka mkataba, kwa maana kwamba Muungano uliopo uvunjike, nchi washirika zipate mamlaka kamili kisha ziamue kushirikiana kama zikipenda. Kwa nini Tume imeyapuuza maoni yao?

Sababu zilizotolewa na Warioba kwamba Muungano kwa sura yake ya sasa hauwezi kudumu pia hazina mashiko. Eti kwamba Zanzibar tayari imeshajitangaza kuwa ni nchi, na Wabara wanaionea wivu. Na hapa, Warioba anasema, kuna majawabu mawili: ama Zanzibar ibadili katiba au Tanganyika nayo ijitangazie uhuru kamili. Kuhusu Zanzibar kubadili katiba, Tume inaona kuwa “ukarabati” huo hauwezekani, hivyo bora Bara nayo iwe na mamlaka kamili. Kwa maneno ya Warioba, “Hii ndiyo sababu kubwa ya kupendekeza muundo wa serikali tatu!” Kwa hiyo, hapa tunaona kabisa kuwa sababu ya kupendekeza serikali tatu sio maoni ya wananchi bali “busara” za Tume.

Lakini kwa busara hizo hizo, Tume ya Jaji Warioba inaiomba Zanzibar ikubali kubadili katiba ili uraia uwe ni suala la Muungano. Kwa maana nyingine, Tume ya Warioba inataka Zanzibar iendelee kuwa nchi/dola (state) lakini isiyo na raia! Na katika busara za Tume ni kuwa hilo ni jambo linalowezekana.
Tume inadhani kuwa uraia ukibaki katika nchi washirika kutaibuka utaifa (utanganyika na uzanzibari), na hili ni hatari kwa Muungano. Lakini Tume haioni shida kama kila nchi ikiwa na bendera yake, wimbo wake wa taifa na serikali yake. Wala Tume haikuona hatari kwa nchi washirika kuwa na mamlaka ya kushiriki katika mahusiano ya kimataifa kiasi kwamba siku moja Tanganyika na Zanzibar zitajikuta zimejiunga katika mashirika ya kimataifa, kila moja kivyake, na wakifika huko waanze kupigana vikumbo. Lakini kwa busara za Tume, hayo yote ni bora yakawepo, na hayatatishia kuvunjika kwa Muungano.

Tume inatuambia kuwa serikali tatu ndio ‘kiboko’ cha Tanganyika iliyoendelea kuimeza Zanzibar kwa kisingizio cha Muungano. Serikali tatu zitaleta usawa. Ni kweli zitaleta usawa, lakini usawa wa kisiasa. Je, usawa wa kiuchumi utakuwepo kwa wabia wasio na uwezo sawa wa kiuchumi? Bado Tanganyika, kama mbia tajiri, ndiyo itabeba gharama kubwa ya kuuendesha Muungano. Amlipaye mpiga zumari ndiyo huchagua wimbo! Ukaka mkubwa wa Tanganyika ndio utadhihiri. Hata huo usawa wa kisiasa hautakuwapo kwani katika Bunge la Shirikisho, wabunge wengi watatoka Tanganyika (wabunge 50 toka Tanganyika dhidi ya 20 wa Zanzibar). Kwa ufupi, shirikisho litaendelea kutawaliwa na Watanganyika iwe ni katika gharama za uendeshaji, nafasi za kisiasa na hata utumishi wa umma. Watanganyika ni wengi kwa idadi, hivyo wao ndio watakaoamua nani awe Rais wa Shirikisho, na uwezekano kwamba Rais wa Shirikisho atatoka Zanzibar utaendelea kuwa ndoto ya mchana. Uzalendo finyu ndio utatawala Shirikisho.
Kwa ufupi, muundo wa serikali tatu una matatizo na kero nyingi kuliko ule wa serikali mbili. Ubabe wa Tanganyika utadhihirika katika mfumo huu kuliko ulivyokuwa katika serikali mbili, ambako Tanganyika alikuwa kaburini. Na kero zenyewe ni zile zinazohusu mamlaka ya wanasiasa kwani ndizo zinazotawala mijadala ya sasa. Wanasiasa wataendelea kupigana vikumbo hata kwa mambo ya kipuuzi; mathalani, katika itifaki  nani awe wa kwanza kutajwa kati ya rais wa Tanganyika na yule wa Zanzibar, au nani mkubwa kati ya Rais wa Tanganyika na makamu wa rais wa Shirikisho. Katika makabidhiano ya ripoti ya Tume ya Warioba tulimsikia Rais Kikwete akilalamika wakati wa kutaja itifaki kwamba vyeo vingi kweli. Huko baadaye katika itifaki wataongezeka rais wa Tanganyika, makamu wake, waziri mkuu, spika wa Tanganyika, jaji mkuu wa Tanganyika, n.k. Barabarani wataenda kwa ving’ora, hivyo tutegemee foleni zaidi. Vyeo vyote hivyo vinaendana na mishahara na ‘miposho’ mikubwa mno ambao ni mzigo kwa wananchi. Na wabara ndio watakaoubeba hasa!

Uchambuzi huu wote unatuambia kuwa tuwe makini wakati wa kujadili rasimu ya pili ya Katiba. Kabla ya kuijadili lazima kwanza tupate taarifa kamili ya Tume ili kujua vigezo na busara zilizowaongoza kutupatia mzigo huo wa “Danganyika”. Nasisitiza mamlaka zinazohusika zitoe taarifa hiyo ya Tume kwa wananchi ili tuijadili na kuikosoa kwani dondoo tu tulizopata kwa Warioba zinaonyesha kuwa kuna mengi ya kuhoji! Bado naamini tunaweza kuikoa nchi yetu isitumbukie katika shimo la utengano. Hii ni kama wengi wetu tutapiga kelele kuuokoa Muungano wetu na kuwasihi wenzetu waliokuwa wamedandia “Basi la Warioba” kushuka ili tutafakari kwa kina zaidi!

Mwandishi wa makala haya ni mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma. Anapatikana kwa barua-pepe: sany7th@yahoo.com

Tuesday, December 24, 2013

Shivji: Tafakuri Juu ya Operesheni Tokomeza

Tafakuri ya wazi juu ya Operesheni Tokomeza


Issa Shivji

Profesa Mstaafu wa Kigoda Cha Mwalimu Nyerere

Aibu, aibu, aibu. … aibu ya kitaifa!  Utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili uliosababisha mateso, ukatili, udhalilishwaji, upigaji na hatimaye vifo vya wananchi ni aibu kubwa kwa taifa letu. Sio aibu tu bali ni janga la kitaifa linalohitaji kufanyiwa tathmini na tafakuri na wananchi wote katika ujumla wao na kujiuliza: tunaelekea wapi? Nini kimesababisha vyombo vya dola na mfumo wetu wa kisiasa kukosa kabisa uwajibikaji kiasi kwamba vyombo vilivyopewa jukumu la kuyalinda maisha, utu na heshima ya wananchi, vigeuke kuwa watesaji na wadhalilishaji wa wananchi hao hao! Kwa nini hatujifunzi? Kwa nini hatujirekebishi?

Katika historia yetu tumewahi kuwa na janga kama hili mnamo mwaka wa 1976 kutokana na Operesheni Mauaji huko Shinyanga na Mwanza. Mwalimu Nyerere aliwalazimisha viongozi wa kisiasa, akiwemo Mzee Mwinyi,  kujiuzulu na watendaji wengine, wakiwemo wakuu wa jeshi la polisi na usalama katika ngazi ya mkoa, kuchukuliwa hatua za kisheria na kuadhibiwa ipasavyo.  Tukio la operesheni Tokomeza linafanana sana na tukio la Operesheni Mauaji, lina sura ileile ya utesaji, udhalilishaji, ubakaji, na uporaji wa mali ya wananchi.

Matukio mengine ya aina hiyo, japokuwa  hayakuwa makubwa kiasi hicho, yamewahi kutokea huko nyuma.  Katika awamu ya pili, kulikuwa na uaaji wa wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero mnamo mwaka 1986, na madhara na mateso waliyoyapata wananchi wakati wa Mwembechai. Katika awamu ya tatu ilitokea kashfa ya waandamaji huko Pemba kuuliwa na wengine kudhalilshwa kiasi kwamba tukio hili lilileta aibu kubwa sana kwa taifa. Kwa jumla, matukio kama haya, yaani utumiaji wa mabavu na vyombo vya mabavu – polisi, usalama, maaskari wengine kama wanamgambo, askari wa wanyama pori n.k. – yameongezeka awamu hadi awamu kiasi kwamba katika awamu ya nne tunashuhudia mauaji na mateso ya wanahabari na wananchi yakiongezeka mara dufu. Hili la operesheni Tokomeza ni kilele.

Sasa tufanyeje?

Uwajibikaji


Mawaziri wanne wamelazimishwa kuachia ngazi kwa kubeba dhamana ya kisiasa. Na wamepongezwa! Mengi mengine yanazungumziwa kwa mtazamo wa kichama na kisiasa. Wengine wanaenda mbali kusema kwamba Waziri Mkuu pia anatakiwa kujiuzulu.  Haya yanaeleweka kwa sababu tukio lenyewe limeamsha hisia za watu na watu wanataka kuona waziwazi kwamba hatua za maana zinachukuliwa kuwatuliza.

Ni kweli kabisa kwamba tukio hili ni kashfa kubwa sana ya kitaifa. Katika mfumo wa kibunge (parliamentary system), Serikali nzima pamoja na mkuu wa serikali, yaani waziri mkuu, wangejiuzulu na labda uchaguzi mkuu ungeitishwa. Lakini katika mfumo wetu wa kirais (presidential system), mkuu wa serikali sio Waziri Mkuu. Ni rais, na rais pia ni mkuu wa nchi. Kwa hivyo, kujiuzulu kwa Waziri Mkuu hakuna uzito. Kwa upande mwingine, huwezi kutegemea rais mwenyewe na serikali yake kujiuzulu kwa sababu, rais pia ni mkuu wa nchi. Na huwezi ukawa nchi bila kiongozi mkuu; kutakuwa na ombwe la uongozi.

Kwa upande wangu, ili kuonyesha kwamba tukio hili linachukuliwa kwa uzito wake, na hisia za wananchi zinajibiwa zipasavyo, mambo mawili yafuatayo yanaweza kufanyika mara moja:

Moja, Rais kuvunja Baraza lake lote la Mawaziri, kama alivyofanya Mzee Mwinyi miaka ya tisini. Hatua hii itakaribiana na uvunjaji wa serikali. Hii itakuwa ni dalili ya uwajibikaji wa kisiasa.

Pili,  watendaji, wakiwemo wale katika ngazi za juu, wafikishwe mbele ya mahakama kwa mashtaka ya kijinai. Mwanasheria Mkuu amependekeza uundaji wa Tume ya Kimahakama. Hii ni njia moja wapo lakini mara nyingi njia hii hutumika kama mbinu za kufunika kombe ili mwanaharamu apite. Nionavyo, labda safari hii, Rais Kikwete anaweza kutumia njia mbadala ya kuteua Mchunguzi huru (independent investigator and prosecutor) ambaye atakusanya ushahidi na kuandaa mashtaka ya kupeleka mbele ya Mahakama.

Na katika uchunguzi huu, watendaji wote wanaohusika, pamoja na wa kijeshi, usalama, na wa kiraia, wachunguzwe na kushtakiwa bila kujali nyadhifa zao.

Tatu, jambo hili lizungumzwe na kujadiliwa na taifa zima kwa upana na undani wake bila kuficha au kulionea haya. Hakuna shule muhimu ya kujifunza kuliko shule ya Umma. Shule ya Umma inafundisha na pia inasaidia kujenga maadili na uwajibikaji. Katika mijadala idara zitatajwa, watu waovu watasemwa kwa majina, maovu yanayofichwa uvunguni yatafichuliwa hadharani. 

Mwishowe, ningependa kuligusia jambo moja muhimu ambalo linaonekana halijaguswa hata kidogo.

Dola na matumizi ya mabavu


Dola ni taasisi ya mabavu, popote pale duniani. Jeshi, polisi, maaskari wengine kama wa wanyama pori, wa hifadhi na kadhalika ni vyombo vya mabavu. Vyombo hivyo vya mabavu katika dola vinapata uhalali wa kisiasa kutumia mabavu kwa sababu vinadhibitiwa na kusimamiwa na vyombo na viongozi wa kisiasa ambao hupata uhalali wao kutokana na kuwa wawakilishi wa wananchi. Kwa mfano, jeshi la ulinzi hutumia mabavu kuilinda nchi dhidi ya maadui wa nje. Uwezo wa kutangaza vita na kuingiza jeshi vitani ni wa rais kama Amiri Jeshi mkuu; na rais ni kiongozi wa kisiasa aliyechaguliwa, sio mwanajeshi.

Katika mfumo wowote ule ambao ni wa kiraia, kwa maana  kuwa sio wa kijeshi (military) au wa kipolisi (police state), vyombo vya kisiasa ndio hudhibiti na kusimamia vyombo vya mabavu. Jukumu la jeshi la ulinzi ni kuilinda nchi. Jukumu la jeshi la polisi ni kulinda amani, wananchi na mali zao. Majukumu haya mawili ni tofauti na yanatenganishwa kikatiba. Hayaingiliani.  

Ndio maana, jeshi la ulinzi halitumiki kudhibiti ghasia nchini. Hii ni kazi ya polisi. Katika mazingira ya kipekee ambayo kuna hatari ya serikali kupinduliwa kwa nguvu au kama kuna uasi ndio Jeshi la Ulinzi huingizwa mitaani. Na jambo hili hufanyika baada ya Rais kutangaza hali ya hatari kwa mujibu wa masharti ya katiba. 

Kwa hivyo, ni kinyume na Katiba na mazoea mabaya  kuliingiza jeshi la ulinzi katika mambo ya kiraia, kama vile uhalifu au ujangili. Kufanya hivyo ni kujenga mazoea mabaya na ya hatari sana.  

Kinyume na msingi huu wa kikatiba, Operesheni Tokomeza ilichukuliwa kama operesheni ya kijeshi. Katika washiriki 2,371, wanajeshi walikuwa 885 au asilimia 37, yaani zaidi ya theluthi moja. Polisi walikuwa 480 au asilimia 20 tu. Wengine walikuwa kutoka majeshi mbalimbali kama la wanyapori n.k.

Pili, operesheni hii ilisimamiwa na Jeshi la Ulinzi. Na nikinukuu maneno ya Taarifa ya Kamati ya Bunge, “Taarifa za mwenendo wa operesheni zilikuwa zinapelekwa moja kwa moja kwa Mkuu wa Majeshi na kwamba, hazikumfikia Waziri wa Maliasili na Utalii.” Isitoshe, viongozi wa kisiasa kama wakuu wa wilaya na mikoa na viongozi wa kuchaguliwa kama madiwani, hawakushirikishwa wala hawakupewa taarifa zozote kuhusu operesheni hii. Mbaya zaidi, baadhi yao waliteswa na kudhalilishwa na maaskari waliohusika na operesheni kiasi kwamba Mkuu wa Wilaya ya Ulanga alijificha katika hoteli.

Kwa kifupi basi, operesheni hii haikudhibitiwa wala kusimamiwa wala kuendeshwa kama operesheni ya kiraia (civilian operation), badala yake iliendeshwa kama operesheni ya kijeshi (military operation). Hili ni jambo la hatari sana na ni mazoea mabaya, hayakubaliki katika mfumo wa utawala wa kiraia (civilian government).

Kuchanganya jeshi la ulinzi na mambo ya kiraia ni dhambi kubwa katika mfumo wa kisiasa tunaoufuata nchini mwetu. Jambo hili halikubaliki kabisa!.

Kwa hivyo, inashangaza kwamba hata Kamati ya Bunge haikuona hili na badala yake ikapendekeza kwamba Serikali iandaae “operesheni nyingine ambayo itapangwa na kutekelezwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Idara ya Usalama wa Taifa. ” Na hoja hii inaonekana kuungwa mkono bila kutiliwa shaka na wabunge wetu! Maana yake nini, wabunge hawajui na hawatambui kwa kuruhusu hili wanajenga mazoea hatari? Kama ndivyo basi ipo haja ya wanasiasa wetu pamoja na wabunge kujielimisha zaidi jinsi serikali za kiraia zilizochaguliwa na wananchi zinavyoendeshwa.

Angalizo! Tujihadhari, tusizoee kabisa  kutumia Jeshi la Ulinzi katika mambo ya ndani kwa sababu kwa kufanya hivyo tutakuwa tunajenga mazoea hatarishi sana kwa mfumo wa kidemokrasia.

Wednesday, December 18, 2013

Scholarship and Home Going Fundraiser

"I am trying to take some of the weight off of my family. The first need is for Sarah's college account. We spent her funds during the time period when I didn't have health insurance. The second, and most time sensitive, event is for my burial. My bile ducts are blocked. The tumours have grown over and around the opening. It may be 2 to 3 weeks at most before my liver is no longer functioning. Please, please, please give so that I can be put into the earth with a small measure of dignity. If not for me, for my children. Please send money orders, checks or stop by our home to contribute  La Vonda R. Staples, 529 Queen Ann Drive MO 63042. Telephone: 314-731-1176" -  La Vonda Staples

Friday, December 13, 2013

Celebrating Mandela at the University of D'Salaam


Friday, December 6, 2013

Mungu Ibariki Afrika - God Bless Africa

Hamba Kahle Mandela - 'The Black Pimpernel'

"I then truly realized that I was in a  country ruled by Africans. For the first time in my life, I was a  free man. Though I was a fugitive and wanted in my own  land, I felt the burden of oppression lifting from my  shoulders. Everywhere I went in Tanganyika my skin color was automatically accepted rather than instantly reviled. I  was being judged for the first time not by the color of my skin but by the measure of my mind and character. Although I was often homesick during my travels, I nevertheless felt as though I were truly home for the first  time. We arrived in Dar es Salaam the next day and I met with Julius Nyerere, the newly independent country's first  president. We talked at his house, which was not at all  grand, and I recall that he drove himself in a simple car, a little Austin. This impressed me, for it suggested that he was a man of the people. Class, Nyerere always insisted, was alien to Africa; socialism indigenous" - Nelson Mandela's Long Walk to Freedom

Thursday, December 5, 2013

Explanations as Excuses

Explanations as Excuses

Chambi Chachage

Could it be that we fail more when we explain why we have been failing? What if all our analytical explanations amounts to apologetic excuses? Does explaining helps?

Let me explain by way of anecdote. I have been trying to learn how to swim on and off since I was 7 years old. This time around a very good friend of mine invited me for swimming lessons. As usual, I started explaining my limitations to the trainer: Sir, you know what, my left leg is slow – I broke it when I was a kid and it’s a bit shorter!

Surprisingly, he did not even pay attention to my explanation-cum-excuse. Little did I know then that my friend had thus told him beforehand: “I am bringing a new student today, he will give you a lot of reasons why he can’t do this or that, just don’t listen!”

It may just be a personal story but maybe it also applies to the public realm. Here I am talking about the reasonable explanations that we give about why our country is stuck in poverty. Yes, there was colonialism. For sure there is neoliberalism. But what if our analyses of these constraints, among other valid reasons, are tantamount to excuses?

My interest is by no means to excuse the negative effects of structural constraints to our progress as a people. As an analyst I am not interested in seeing us turn into what Mahmood Mamdani critiques as those activists whose focus is “to act before seeking to understand.”[1] But the activist in me would not like to be stuck in the other extreme.

The need to analyze, explain and thus know more about our concrete condition before we bring about social change should not turn into another exercise in excusing. In this regard activists that Mamdani critiques were right when recalling the Rwanda of 1994 as a time when we waited to find out, “when we thought we needed to know more” but, “it was too late”, as needing “to know turned into an excuse for doing nothing.”

A balance is needed if we are not to fall into the trap of feeling “we need to know no more in order to act” especially when what we (think we) know is “not enough to call for action.” This brings me back to the personal anecdote on my swimming classes.

There is no doubt that I knew enough about my conditions prior to the lessons. I have explained them so many times – in the soccer pitch where I can hardly exercise in unison with my fellow players; in the dance floor where I miss the steps more often than not; in wedding marching where my left leg goes up when others’ legs go down.

What I need to do is quit using that explanation – and many others that range from having hearing difficulties to having a bad posture – as an excuse. By the way, I am already overdoing it here – excusing myself by explaining! All I need now is to act.

The same logic can be extended to the society as a whole, especially one that Eckhart Tolle refers to, psychoanalytically, as having “national and racial pain-bodies.”[2] They already know enough about why they are on the ‘periphery’ and our analysts are still busy studying them to know more about that ‘great divergence.’ Perhaps the matter of more urgency now is to indeed prioritize doing over knowing as we know so much.

For quite some time now I have been wondering why Ben Carson tends not to dwell on explaining the structural limitations that makes it hard to succeed like him. Why, I pondered, does he think anybody can rise above any condition just because he did?

Here is a sample of such seemingly Carsonian ‘pep talks’: “It doesnt matter if you come from the inner city. People who fail in life are people who find lots of excuses. It’s never too late for a person to recognize that they have potential in themselves”; “So after a while, if people wont accept your excuses, you stop looking for them.”[3]

Now I am starting to make sense of Carson’s emphasis. We cannot simply explain our structural limitations away. But we can seriously expand our capacity to change them.

For sure, as Barack Obama correctly noted in his touching “statement about Trayvon Martin”, it can be frustrating when context is being denied.[4] But, again, that does not mean societies and individuals that are ‘marginalized’ have to spend all the days of their lives explaining and explaining why they are where they are in the first place.

As one analyst once concluded: “The philosophers have only interpreted the world, in various ways; the point is to change it.”[5] To that I would add: We have explained our situation away, in various excusable ways; the point is to change it. Let’s just act now.[1] Mahmood Mamdani (2009). Saviors and Survivors: Darfur, Politics, and the War on Terror. <http://www.amazon.com/Saviors-Survivors-Darfur-Politics-Terror/dp/0385525966>
[2] Eckhart Tolle (2005). A New Earth: Awakening to Your Life’s Purpose. <http://www.amazon.com/New-Earth-Awakening-Purpose-Selection/dp/0452289963 >

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP