Thursday, May 15, 2014

Masaa Matatu na Mwandishi Mabala - 17 Mei 2014

MASAA MATATU NA RICHARD MABALA

Taasisi za Soma: Leisure Culture and Learning na Kitabu Nilichosoma” zinazojihusisha na kuhamasisha jamii kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu zimeandaa mjadala ambao utawakutanisha wasomaji wa vitabu na mwandishi nguli wa vitabu nchini Richard Mabala.

Richard Mabala atatoa mada kuhusu tasnia ya uandishi wa vitabu nchini. Kwa wapenzi wa vitabu na tasnia ya uandishi wa vitabu kwa ujumla, hii ni fursa adhimu kujumuika na Richard Mabala na kujifunza kutoka kwake.

Pia kutakuwa na mjadala kuhusu kitabu chake kipya cha RUN FREE kilichojinyakulia Tuzo ya Burt ya Fasihi ya Kiafrika. Taasisi za Soma Book Café na ‘Kitabu Nilichosoma’ zitatumia fursa hiyo pia kuwazawadia vitabu washindi mbalimbali wa mashindano yao yaliyopita.
Kitabu cha RUN FREE kinazungumzia changamoto zinazowakabili vijana hasa katika kuchagua njia waipendayo katika kutimiza ndoto zao za maisha. Tumemwalika Masoud Kipanya (kwa nafasi yake ya uchoraji) na Antony Mtaka (kwa nafasi yake ya udau kwenye riadha). Njoo uzisikilize simulizi za mbio zao za maisha na za washiriki wengine kisha nawe ueleze uzoefu wa mbio zako! 

Siku: Jumamosi tarehe 17/5/2014

Mahali: Soma Book Café ( http://www.somabookcafe.com/ )

Shuka mataa ya Morocco. Rudi nyuma hadi hospitali ya AAR. Kisha fuata barabara inayokwenda Chama cha Wanasharia wa Tanganyika (TLS). Hapo utaliona bango linalokuelekeza Soma Book Café. Kwa msaada zaidi kuhusu ilipo Soma Book Café piga 0653619906/0785014070.

Muda: Saa 4.00 Asubuhi hadi saa 7.00 mchana.

Thibitisha ushiriki wako kwa namba zifuatazo:

0653619906 (Ado Shaibu)
0785014070 (Soma Book Café)
0717577517 (Seif Abalhassan)

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP