Wednesday, June 4, 2014

Kwaheri Mwanaharakati Fides Chale

Kumbukizi:
Udadisi inasikitika kumpoteza Mwanaharakati na Mwenyekiti Muasisi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Fides Chale. Mdadisi ni miongoni mwa wadau waliobahatika kufundwa uwanaharakati na Mwalimu huyu katika matamasha ya jinsia (GF) na semina za jinsia (GDSS) za kila jumatano. Washiriki wa warsha kuhusu "Haki ya kupata Ajira yenye Heshima, Maisha yaliyo Endelevu na Kipato kinachomwezesha Mtu Kuishi" katika Tamasha la Jinsia la mwaka 2007 tunamkumbuka kwa ucheshi wake, umahiri wake wa kuwezesha mijadala na upendo wake. Mama Kazikupenda ametuachia urithi mkubwa na ni wajibu wetu kuenzi kazi zake kwa kuendelea kupigania haki za wanawake na wanaume wanyonge waliosukumwa pembezoni na mfumo dume.

Tanzia:

Maziko:
"Alhamisi Juni 5, 2014 Misa itakuwa St. Peters kuanzia saa 8 mchana na kutoa heshima za mwisho. Mazishi katika makaburi ya Kinondoni saa 10 jioni" - REPOA

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP