Wednesday, August 13, 2014

WASIFU WA WANAZUONI (WA)TANZANIA

Ndugu Mwanazuoni,

Blogu ya Udadisi inakuomba/inakukaribisha ulete wasifu wako iweze kuutoa katika mfululizo wa WASIFU WA WANAZUONI (WA)TANZANIA. Huu utakuwa ni mwendelezo mpya wa PROFILING TANZANIA'S SCHOLARS IN THE DIASPORA. Tofauti ni kuwa utahusisha na waliopo Tanzania.

Ili wasifu wako utokee Udadisi tukufahamu wewe na kazi/tafiti zako, tuma vitu vitatu vifuatavyo kwa chambi78@yahoo.com: (1) Picha (2) Kiunganishi cha Chapisho na (3) Tovuti yenye wasifu.

Picha inaweza katika JPG, GIF, PNG au kiunganishi/tovuti yenye picha au Video katika Youtube, ama Vimeo. Kama chapisho halina kiunganishi unaweza kulituma ili Udadisi iliweke mtandaoni liwe na kiunganishi. Tovuti ya wasifu inaweza kuwa ya Linkedin, yako binafsi, ya chuo chako, kazini kwako na kadhalika. Unaweza pia kuwa mbunifu zaidi kwa kuwasilisha taarifa zingine.

Wasalaam,

Chambi

2 comments:

AMINA August 13, 2014 at 8:14 AM  

Nimeipenda hii ngoja na mimi niangalie vyeti vyangu kama vitaniruhusu kuleta wasifu wangu.

AMINA August 13, 2014 at 8:20 AM  

Hongereni sana udadisi blog kwa wazo hili zuri sana. hapa tutapata kuwafahamu wanazuoni wetu na maisha yao Hongereni sana

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP