Saturday, October 4, 2014

KITABU KWA MAENDELEO TANZANIA (KMT)

KITABU KWA MAENDELEO TANZANIA (KMT)

 KWA KUWA usomaji wa vitabu ni nguzo muhimu katika kujipatia maarifa, kujiburudisha, kujielimisha na kujikomboa kifikra kwa jamii na taifa lolote,  

NA KWA KUTAMBUA kwamba jamii au taifa lolote lisiloukumbatia utamaduni wa kujisomea vitabu ni taifa linalojichimbia kaburi lake lenyewe,

 NA KWA KUELEWA kwamba utamaduni wa kujisomea vitabu umepewa kisogo kwenye nchi nyingi za Kiafrika ikiwemo Tanzania, na hivyo basi kuviza ustawi wa taifa na watu wake kwenye nyanja za kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa, 

HIVYO BASI, Sisi wapenzi wa vitabu wenye ari ya kuibadili jamii yetu kifikra tumeamua kuunda Umoja huu wa Kitabu kwa Maendeleo Tanzania (KMT) ili uwe chachu ya kuhamasisha jamii yetu kujenga tabia ya kujisomea vitabu na maandiko mbalimbali ili kujiburudisha, kujielimisha na zaidi ya yote, kujikomboa kifikra.

1 comments:

Ado Shaibu October 5, 2014 at 9:44 AM  

Shukrani sana ndugu chambi kwa ushirikiano. Tupo pamoja.

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP