Thursday, November 27, 2014

Tofauti Kati ya Ripoti ya Escrow na ya Richmond

Tofauti kubwa kati ya ripoti ya uchunguzi wa RICHMOND na ya ESCROW ni kuwa:

Ya kwanza ilitolewa na KAMATI TEULE ya BUNGE ambayo ilikuwa na MUDA mwingi sana na RASILIMALI nyingi mno za kufanya UCHUNGUZI uliohusisha hadi ZIARA za kwenda NCHI za MBALI kufuatilia KAMPUNI hiyo ILHALI hiyo ya pili imetolewa na KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE ambayo ilikuwa na MUDA mfupi sana na RASILIMALI chache mno za kufanya UCHUNGUZI ambao ulihusisha kupitia/kuchambua/kuhakiki/kujumuisha TAARIFA za UCHUNGUZI wa CAG n.k. pamoja na kuwahoji wakuu wa TAKUKURU, TRA, CAG et al.

Kilicho muhimu sasa ni kuhakikisha haturudii makosa yaliyogusiwa hapa chini kuhusiana na MAAZIMIO ya BUNGE:


Tusirudie makosa kwenye maazimio ya #Escrow,tujikumbushe maazimio ya #Bunge kuhusu #Richmond ambayo hayakutekelezwa:http://mnyika.blogspot.com/2012/01/taarifa-ya-hoja-kuhusu-utekelezaji-wa.html …


Tujikumbushe maazimio ya Bunge kuhusu Richmond ambayo hayakutekelezwa ili tusirudie makosa kwenye maazimio ya Escrow: http://www.-----------.co.tz/richmond_kufunga_mjadala_bunge ni_ni_kukejeli_umma …


0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP