Saturday, December 13, 2014

Ripoti ya CAG ina kitu tusichokijua kuhusu ESCROW?


"Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali iliombwa na Katibu wa Bunge na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kufanya ukaguzi maalum wa Akaunti ya Tegeta Escrow. Tunapenda kuwajulisha Umma taarifa kuhusu mwelekeo wa ukaguzi huo. Tafadhali pakua kiambatanisho cha taarifa kamili kuhusu suala hilo kwenye link hii 2014 IPTL Press Release WORD" - Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) [16 Oktoba 2014]

"Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali CAG - Prof MUSSA JUMA ASSAD, ameahidi kufanya marejeo katika Ripoti ya ofisi yake kuhusu Akaunti ya TEGETA ESCROW ambayo iliibua mjadala mzito Katika Mkutano wa Kumi na sita na Kumi na saba wa bunge wiki iliyopita mjini DODOMA.Prof ASSAD ameeleza hayo mjini ARUSHA baada ya kufungua Mkutano wa Bodi ya wahasibu NBAA ambapo amesema katika ripoti hiyo ya TEGETA ESCROW kuna mambo machache yanayohitaji kufanyiwa kazi" - Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) [5 Desemba 2014]

"Kufuatia kupokea nyaraka hizo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa Ripoti ya CAG iwekwe hadharani kwa ajili ya umma kuweza kuisoma na kujua nini hasa kimesemwa na kupendekezwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Rais Kikwete ameelekeza kuwa Ripoti hiyo itangazwe kwenye magazeti yanayosomwa na watu wengi na kwenye mitandao ya kijamii, ili Ripoti hiyo iweze kupatikana kwa Watanzania wengi" - Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais [9 Desemba 2014]

"Ikulu imeagiza Taarifa ya CAG ichapwe kwenye magazeti, jambo ambalo halijapata kutokea huko nyuma kwani sio mara ya kwanza PAC kutumia Taarifa ya CAG kuwajibishana" - Ukurasa wa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) [12 Desemba 2014]

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP