Tuesday, January 13, 2015

Watanzania Uwezo Tunao Wa Kuwekeza Katika Gesi?

Salim Khatri:

Ukiweka mazingira mazuri kwa wawekezaji utaambiwa unakumbatia wageni. Prof. Muhongo alipowaambia wakina Mengi walipe $700,000 kwa ajili ya tender document na $3,500,000 for data ili wakashindane na wenzao kupata vitalu vya mafuta na gesi, wakamwambia hana uzalendo.

Emmanuel Sulle:

[Salim] kwa sentensi yako hii ni kweli Muhongo hana uzalendo kwa sababu hata hao wawekezaji wa nje unawaosema wengi wanapewa misaada au mikopo nafuu sana kutoka nchi zao kulinganisha na hapa kwetu.  Je, una habari hii?

Nchi yoyote inaweza kuendelea kwa kuwaendeleza watu wake na siyo kuwaleta wageni ambao faida wanakwenda kuziwekeza nchini mwao. Fanya utafiti kwenye sekta ya madini, tumepoteza hela kiasi gani.


Chambi Chachage:

Nimewahi kumuuliza mtafiti mmoja wa masuala ya gesi na mafuta  ambaye hana mapenzi na Muhongo kwamba: Hivi tukiweka pembeni huo 'ujuvi' na 'majigambo' ya Profesa, je, ni kweli hatuna watu wenye uwezo wa kuwekeza kwenye gesi? Akanijibu: HAKUNA! Nikamuuliza hata kina Bhakresa, Mengi, Rostam et al. wakijikusanya? Akasema: Hata iwe hivyo hawana mtaji wa kutosha kutafuta na kuchimba gesi/mafuta. Katika hili Muhongo ni 'mwongo' pia?

Juma Mwapachu:

Huu ni uelewa hafifu kabisa kuhusu suala la uwekezaji kijumla hata kama ni kuhusu sectors ambazo wengi wetu wanadhani mitaji ya uwekezaji inatoka katika mifuko ya watu binafsi. Hakuna matajiri binafsi wanaowekeza katika sectors hizi kwa kutumia fedha zao. Mitaji inatokana na proofs za kuweko dalili nzuri za kuwepo rasilimali. Fedha zipo nyingi katika global capital markets. Tatizo ni Serikali zetu kutokuwa na confidence na watu wenyewe na kuwa tayari kukubali mabilionea kuibuka.  Tuondokane na fikra hizi zisizo na  manufaa. Tubadilike la sivyo tutabaki nyuma.


Emmanuel Sulle:

Huh!

I am not sure if this researcher is really saying the truth! It is not true that we need cash like that. Govt can issue loans to its committed citizens or companies to do business. This is how some countries have done either in Asia or Europe. And, govt too can seek loans from financial institutions to subsidize the locals business!

There are also different models in which locals can participate in this business and that is joint ventures. In Asia, people owns wells of oils simply because they did not give out their oil/gas land but rather invited investors to harvest while paying them royalties/certain amount of revenues in special/specific agreement(s).

[…]

Excellent point from Hon. Mwapachu. 

If we "wanazuoni" still think that we as "a country" are so poor then we are not different from "laymen", excuse my language, but that is the reality. The national wealth is not simply pegged on the revenues you see/count. Infact, the value of our nation increased several folds in the global capital from the day we discovered gas, Tanzanite etc. Unfortunately, we are here because of our choices, and because of these choices, we are likely to continue to be here unless we change our mindset and make better choices

[…]

Tukiuchukulia huu mjadala kama mapambano kati ya Mengi na Muhongo tutakuwa tunakosea. Muhongo ni waziri, ni mtumishi wa umma. Anawasilisha maoni ya serikali tuliyoiweka madarakani. Kwahiyo, yeyote anayehoji hoja zake anafanya vile kwa mujibu wa haki zake kama mwananchi (mwenye nchi) na asingeweza kujibiwa kwa dharau kama alivyofanya Muhongo.

Pili, suala la wazawa kupendelewa, ni dhana inayotumika duniani kote kulinda maslahi ya nchi na watu wake. Anayeona hili nalo mbaya hajui msingi wa hili jambo. Katika nchi karibu zote za Ulaya na America, wazalishaji wa ndani wanapewa ruzuku wazalishe kwa ajili ya mauzo ya nje au ndani ili kuustawisha uchumi wa nchi zao. Labda sisi tunaona wivu watanzania wenzetu wakiendelea, kwahiyo bora wageni waje waendelee.

[...]

Chambi Chachage:

Mkopo watoe vipi/wapi kama hadi leo tunaambiwa hata mabilioni ya kuwalipa watu RUIPA hawajayatoa? Kwenye 'Escrow'? Wauze 'Sovereign Bond'? Wakope 'World Bank' na 'IMF'? Hebu tufanya mahesabu. Njia rahisi ni kutaja kiwango cha fedha ambacho Serikali inacho (kwa mfano, bajeti ya nchi ni trilioni ngapi sasa?) na kukilinganisha na hizo zinazosemwa ni gharama (halisi) za kutafuta na kuchimba gesi/mafuta. Nakisi ni hasi, chanya? Waipe TPDC?

PS. Halafu tukumbuke kwamba wanaochangia kufadhili bajeti yetu ndio hao hao ambao makampuni ya nchi zao yanatafuta gesi na mafuta nchini kwetu - rejea ramani ya utafutaji wa gesi/mafuta iliyopo kwenye tovuti ya TPDC.


Alex Kobalyenda:

Exactly my Point Comrade...

We put our emotions and political fronts too high and ignore uhalisia wa mambo.

If we can’t feed ourselves, who will agree tukope to gamble?

It’s sad but ndio ukweli wenyewe....best option ndio hiyo kuvizia wapate then we jump wagon.....with good policies in favor ta Mtanzania.


Salim Khatri:

And that's why Prof. Muhongo gets attacked from all sides for stating facts that are common knowledge in the oil and gas industry.

[...]


[…]


Hizo dharau zinatokea wapi? Yaani kuambiwa mkashindane kutengeneza juisi, biashara mliyokuwa na ujuzi pamoja na uzoefu nao ndiyo dharau? Mbona ni ukweli mtupu? Bakhressa, Muhammed Enterprise, Mengi (matajiri watatu wakubwa kabisa nchini) biashara wanayoshindana ni kutengeneza maji, soda na juisi. Huo ndiyo ukweli kaka. Sasa na mimi kaniweke kwenye hilo kundi la watu wanaoshindana kutengeneza juisi kama nitakuona unanidharau ama unanipandisha chati.


Kupewa ruzuku uendelee kuzalisha ili ulinde ajira za nchini siyo sawa na kukabidhiwa bure biashara usiyokuwa na ujuzi wala uzoefu nao. Mfano uliotolewa na Prof. Muhongo ndiyo huo wa Mengi kukabidhiwa leseni za madini zenye ukubwa saw ana Dar es salaam tatu. Mpaka leo kazalisha madini kiasi gani? Akataka akabidhiwe hoteli ya Kilimanjaro kwa bei chee wakamkatalia kumpa upendeleo huo. Baada ya kuikosa Hoteli ya Kilimanjaro keshajenga hoteli ngapi mpaka hivi sasa? Alichotaka Mengi apewe hoteli kwa USD 1 million (ndiyo lilikuwa dau lake – the lowest bidder) halafu akaiuze kwa mtu mwengine for USD 15 million na kuweka mfukoni USD 14 million net profit. Hapo mgonjwa anayesugua benchi kwenye hospitali ya Mwananyamala anafaidika vipi?

[...]

Bado sioni wapi Prof. Muhongo ameleta hadithi... 

Mavere Tukai:

Utaona vipi wakati umeamua kuwa na selective blindness Nd. Salim??

Sabatho Nyamsenda:

Hili jukwaa nadhani linaionea wivu JF na linataka kuiiga. Muda si mrefu tutaenda kulekule. Nashauri tujikite zaidi katika hoja badala ya mashambulizi ya watu binafsi ili tuwe na uwezo wa kuchambua.

Suala hapa ni umiliki, udhibiti na ufaidikaji wa rasilimali. Nani amiliki, na kwa faida ya nani?

Kuna lugha mbili zinazotumika: “watanzania” na “wazawa”. Hizi ni tofauti kabisa.

Kuna mtu kashadadia hoja ya “wazawa” na kusema kuwa duniani kote ndivyo ilivyo. Pengine hatujaingia zaidi katika historia ya “uzawa” hapa nchini, na kwingineko. Yapaswa turejee mjadala wa uraia katika baraza la sheria la Tanganyika mwaka 1960, ambako hoja ya “uzawa” ilikuwa ikitumika kudai haki ya uraia, na haki ya utawala kwa watu weusi tu. Nyerere aliipinga na kutishia kujiuzuru uwaziri mkuu. Hoja hiyo ilijitokeza tena wakati wa ubinafsishaji ambapo wazawa walidai kupendelewa. Mwalimu aliipinga kwa nguvu na kuiita “ukaburu” rejea hotuba yake Kilimanjaro Hotel, mwaka 1995.

Hoja hii ilipoibuliwa na akina Mengi wakati wa gesi, “mzawa” ni nani hasa? Katika “wazawa” Bakhresa, Manji na Rostam wamo? Katika kile kisa cha Kongamano la Udasa nilichokisimulia hapo awali, Muhongo alitaja watanzania 10 walioohodhi umiliki katika madini. Mengi alikuwa wa tatu. Wakati akitaja majina mawili ya mwanzo, japo ni Watanzania, majina yao yanaonyesha dhahiri kuwa wana asili ya Kiasia. Washiriki katika Ukumbi wa Nkrumah walikuwa wakipiga kelele “sio wazawa hao”!

Kwa hiyo watetezi wa uzawa kueni macho, na mseme waziwazi kinachotetewa ni nini? Dhana ya Uzawa imeshatafitiwa vya kutosha (rejea vitabu vya Mamdani 1. Citizen and Subject; 2. When Victims become Killers; 3. Define and Rule), na imeonekana kuwa chanzo cha migogoro mikubwa ya kisiasa pale ambapo “wazawa” wanahisi kunyang’anywa haki zao na “wahamiaji”. Mfano wake ni mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Hilo mosi. Pili, tunaposema “Watanzania wamiliki” tunamaanisha nini hasa? Hapa kuna watetezi wa mabepari wa bongo (akina Mwapachu); watetezi wa umiliki wa dola kwa niaba ya Watanzania; na watetezi wa mchanyato (dola + binafsi). Tungejikita katika kujadili njia hizi na kuonyesha ni ipi yenye tija na manufaa kwa sasa na vizazi vijavyo.


Kwa vyovyote vile, hapa nchini hakuna tabaka la mabepari wenye mtaji (national bourgeosie) bali tuna tabaka la mawakala (compradorial bourgeosie). Uwekezaji mkubwa binafsi wa ndani utahitaji tulijenge tabaka hilo, kwa kulipatia upendeleo na kuliruhusu kupora pale inapowezekana. Tufumbie macho Escrow, EPA, Richmond, ukwepaji kodi n.k., na tuwahimize hao waporao kuwekeza fedha “zao” katika shughuli za uzalishaji. Ndivyo zilivyofanya nchi zote zilizojenga tabaka la mabepari wa ndani, zikiwemo Japan na Malaysia. Ndiyo maana ya upendeleo kwa “wazawa” hiyo!

Chambi Chachage:

Salim, ungekuwa wewe unaambiwa maneno hayo hapo chini ungejisikiaje ilhali unajiona ni mzalendo/mzawa?

Mheshimiwa Spika, gesi asilia na mafuta: Napenda kurudia tena hakuna Mtanzania aliyezuiwa, hayupo wala hatujamzuia Mtanzania yeye akatafute kampuni waje naye akiwa na ubia hatujazuia, na tuna kampuni ya Watanzania ambayo tayari inafanya kazi na Wa-Australia na wote hata wao wenye kampuni hiyo walikiri kwamba hawana fedha, hawana teknolojia ndiyo maana wametafuta kampuni ya Australia wafanye nayo kazi.

Kwa hiyo ndugu zangu kama nia ya mtu ni kitalu, wewe njoo na wawekezaji mshindane. Lakini nataka kusisitiza tena haitatokea kwamba kuna mtu atapewa kitalu yeye na familia yake, haiwezekani! Na hii hata mtu aandike asubuhi na mchana, aimbe, haiwezekani! TPDC ndiye anayetuwakilisha, anawakilisha Watanzania wote tajiri na maskini, lakini hamna vitalu vya familia hapa.

Mheshimiwa Spika, sheria ambayo tunayoileta na nimeshaongea na wakuu wangu wote kwamba hii gesi iliyogundulika tusipokuwa waangalifu tunaweza tusifaidike. Ndiyo maana ni lazima tuwe waangalifu kwa sababu huyu mtu akivuna gesi, sasa tuamue je, hizo fedha kama kitalu ni chake ni fedha zake na familia yake, lakini kama ni za TPDC ni zetu wote, za Watanzania wote.

Kwa hiyo msidanganywe na hadithi yoyote na tutakuja hapa, sheria tunayoileta hapa ya sovereign fund ni kwamba zile fedha hata Hazina hawatazichukua zile fedha kwamba yamepatikana mabilioni tunaenda tunayamwaga yote pale Hazina, hakuna kitu kama hicho. Patatengenezwa mfuko maalum na fedha zile hazitatoka bila ya uthibitisho wa Bunge.

Kwa hiyo Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu hakuna atakayetoa ruhusa kwenda kuchukua zile fedha, lazima Bunge litoe idhini. Kwa sababu hawa Wabunge ndiyo wanaowawakilisha wananchi. Tutaweka kwamba haziwezi kutolewa zote zig zag, itakuwa ni kwa percent kwa sababu sisi wenyewe tunajua ukimpa mtu hapa shilingi milioni mia moja ukasema tumia tuletee mrejesho ataonesha amezimaliza zote milioni mia moja.

Kwa hiyo hatuwezi kufanya kosa kama hilo, itakuwa ni percent fulani kwa mwaka kusaidia bajeti kwa mwaka huo, fedha zingine zinatunzwa kwa ajili ya vizazi vinavyokuja na kusaidia uchumi wa nchi utengemae, na ndiyo maana kama tunakuwa na sovereign fund ni hatari sana kuruhusu mtu na familia yake awe na kitalu. Haya yote ndiyo nilikuwa nataka ayaweke kwenye bajeti, sasa yakawa ni hadithi tu.

 - PROF. MUHONGO - UKURASA WA 311 - 312 WA HANSARD YA MAJADILIANO YA BUNGE YA 30 MEI 2014

Zitto Kabwe:

Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza. Hiyo hadithi hapo [juu] bado ni hadithi tu. 

Emmanuel Sulle:

Mh Zitto, tusaidie, hadithi ipi unayoizungumzia? ya Muhongo?

Salim Khatri:

Nilikuwa nataka kuuliza hicho hicho. Kipi kwenye maneno aliyonukuliwa Prof. Muhongo ni "hadithi", yaani masimulizi yasiyokuwa na ukweli.

Jambo usilolijua ni kweli giza na ndiyo maana Prof. Muhongo anasema anapozungumzia hayo mambo uchukue karatasi na kalamu.

Chambi Chachage:

Labda wasiokuwa katika "usiku wa kiza", i.e., wanaojua "jambo" ni wenye hoja hii aliyokuwa anaijibu kwa "hadithi":

Mheshimiwa Spika, katika bunge la bajeti kwa mwaka wa fedha 2013/2014, kambi ya upinzani bungeni iliitaka serikali kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanamiliki na kunufaika na rasilimali za Taifa hili ikiwa ni pamoja na gesi iliyogunduliwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Aidha miezi michache baadaye Tanzania ilishuhudia mivutano mikubwa kuhusu uwekezaji katika sekta ya gesi hapa nchini. Mvutano huo ulijitokeza kati ya taasisi ya Uwekezaji nchini (TPSF), kupitia kwa mwenyekiti wa taasisi hiyo na serikali kupiti kwa Waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini kuhusu taasisi hiyo (TPSF) kuwekeza katika suala la gesi nchini.

Mheshimiwa Spika, katika maoni yake, TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Watanzania katika uchumi wa gesi na kuishauri serikali kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi hadi sera ya gesi itakapokuwa tayari na taasisi hiyo iliomba kukutana na Waziri Muhongo mwenye dhamana ya nishati na madini kwa majadiliano zaidi. Tofauti na ilivyokusudiwa, serikali ilijibu kupitia vyombo vya habari kwamba mpango wa kugawa vitalu vya gesi na kuingia mikataba uko palepale kama ulivyopangwa kufanyika bila kuzingatia mchango ambao ungetolewa na taasisi ya uwekezaji hapa nchini. Mbaya zaidi serikali ilikataa bila kumng'unya maneno kwamba haina mpango wa kukutana na TPSF, kwani kufanya hivyo ni kupoteza muda, na kuongeza kuwa uwezo wa wafanyabiashara wa Tanzania ni kuwekeza kwenye soda na juisi, si kwenye sekta ya gesi. Septemba 7, mwaka 2013, mtu aliyejitambulisha kwa jina la "CCM Tanzania", alisambaza taarifa kwa njia ya barua pepe kwa vyombo vyote vya habari na kumshambulia mwenyekiti wa taasisi ya uwekezaji TPSF kwa kumwita fisadi, mbinafsi na mfitini wa maendeleo.

Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na hisia kuwa mjadala wa haja ya wazawa kumiliki na kuendesha sekta ya gesi nchini iliyosimamiwa na taasisi ya uwekezaji nchini TPSF ina lengo la kutaka kuionesha jamii kuwa serikali kupitia wizara ya Nishati na Madini na watendaji wengine wa wizara hiyo hawajali masilahi ya wazawa na hawana utaifa wala uzalendo.

Katika kuonesha kutokuwa tayari kwa serikali katika kuwasaidia watanzania kumiliki rasilimali za taisa hili, serikali kupitia waziri mwenye dhamana Profesa Muhongo alisikika akiwaambia watanzania kupitia kongamano lilifanyika katika ukumbi wa Nkurumah, chuo kikuu cha Dar es salaam kuwa “Watanzania: Kampuni za Mengi zimeshikilia vitalu 59 vya madini vyenye ukubwa wa mita za mraba 3,752.37 (sq km) sawa na Dar es salaam tatu,amevishikilia, ameshindwa kuviendeleza. Watanzania wanakosa mapato na ajira! Sasa anataka vitalu vya gesi na mafuta. Je, huu ndio uzawa... tutatoa orodha ya vitalu vya madini vilivyoko mikononi mwa Mengi ambavyo anafanya ulanguzi. Ukweli utaonyesha ubabaishaji na ulanguzi wa Mengi wa genge lake.”

Mheshimiwa Spika, kauli ya serikali ilitolewa na waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini, inasikitisha jinsi ambavyo serikali hii ya CCM ina watendaji ambao hawawezi hata kufanya jambo dogo la utofauti, hoja ya TPSF ni tofauti na hoja ya bwana Mengi kama mtu binafsi, tamko la TPSF, lilitokana na kikao cha bodi ya taasisi hiyo cha Agosti 28, maoni yaliyo wasilishwa kuhusiana na gesi asilia yalikuwa ya TPSF kama wadau wakubwa wa uwekezaji. Aidha Katika maoni hayo, TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Watanzania katika uchumi wa gesi na kushauri kusitishwa ugawaji wa vitalu vya gesi hadi hapo sera ya gesi itakapokuwa tayari.

Mheshimiwa Spika, serikali hii tayari katika jambo hili la uwekezaji wa gesi imeonesha msimamo wake, awali serikali ilisema kinaga ubaga kwamba sheria iliyopo haikidhi mahitaji ya sekta ya gesi asilia ndiyo maana serikali ikaamua kusimamisha ugawaji wa vitalu vya gesi na kuamrisha mikataba ipitiwe upya na sera ipatikane. Waziri wa Nishati Septemba 2012 alikaririwa akisema: “Baadhi ya mikataba ni ya ovyo, na inahitaji kuvunjwa.”Na “Sitovumilia mikataba ambayo haina masilahi kwa nchi na inawanufaisha wachache.”

Mheshimiwa Spika, msimamo huo wa serikali ulianza kwa kuamrisha Bodi mpya ya TPDC kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi ambao ulipangwa kufanyika Septemba 2012 na kupitia upya mikataba yote. Aidha miezi michache baadaye, Februari 26, 2013, serikali ilirudia azma yake hiyo mjini London katika ukumbi wa Chatham kwenye mkutano uliopewa jina la “Tanzania: An Emerging Energy Producer”.

Katika hali ya kustajabisha, serikali ilibadilisha mawazo ghafla, na sasa serikali ilitaka vitalu vigawiwe kabla ya kuwapo kwa sera ya gesi. Waziri wa Nishati na madini, Prof. Muhongo alinukuliwa na gazeti la Daily News la Agosti 31, 2013 akieleza sababu zake za kutaka vitalu vigawanywe kabla ya kupitishwa kwa sera ya gesi kuwa ni pamoja na mosi, ushindani wa soko na majirani zetu, akitolea mfano wa Msumbiji. Pili, sheria ya mwaka 1960 iliyoanzisha TPDC na Sheria ya Petroli ya mwaka 1980, kwamba zinatosha kusimamia ugawaji wa vitalu, akimaanisha sera na sheria mpya zitafuata baada ya ugawaji wa vitalu; na tatu, Watanzania hawana uwezo wa kuwekeza katika sekta hii akimaanisha waachiwe wageni peke yao.”

Aidha serikali katika kusisitiza nia hiyo ilisema wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza tu kushiriki biashara ya juisi na soda na hawana uwezo wa kushiriki katika biashara ya gesi ambayo ni moja ya utajiri unatokana na ardhi ya nchi yao Tanzania.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaungana na maoni yaliyotolewa na taasisi ya uwekezaji Tanzania TPSF juu ya uwekezaji kwenye sekta ya gesi asilia, pamoja na hayo, tunaitaka serikali kufanya mambo yafuatayo; mosi kutoa hadharani taarifa ya kupitiwa kwa mikataba yate ya vitalu iliyoagizwa kufanywa na TPDC.

Pili, kambi rasmi ya upinzani inaitaka serikali kuacha dharau kwa Watanzania kuwa ni masikini na hawana uwezo huku jukumu la kuondoa huo umasikini likiwa mikononi mwao, ni kweli kuwa ghara za uwekezaji zinaweza kuwa ni kubwa lakini, kama tunashuhudia makampuni ya kigeni kama IPTL yakija kuwekeza Tanzania bila mitaji na yanapewa mikataba, makampuni ya uchukuzi kwenye reli na makampuni lukuki yakija hapa bila mtaji na kudhaminiwa na serikali, serikali hii inashindwa nini kuwadhamini Watanzania kuwekeza katika sekta ya gesi asilia?

[...]

Mheshimiwa Spika, kampuni ya Pan African Energy Tanzania (PAT) Ilikosa sifa za uaminifu ambapo Kamati ilishauri Mkataba wa Pan African Energy Tanzania (PAT) usitishwe. Aidha, utekelezaji wa kuvunja mkataba huu ulipaswa kwenda sambamba na kuhakikisha kuwa taratibu za kisheria na za kimkataba zinazingatiwa, uwepo wa usalama wa visima na mitambo na uwepo wa uhakika wa huduma ya upatikanaji wa gesi nchini. Hili lilikuwa ni pendekezo namba 4 la kamati iliyochunguza uendeshwaji wa sekta ndogo ya gesi asilia hapa nchini na baadae kuwa azimio la Bunge.

[...]

Mheshimiwa Spika, Waziri wa Nishati wa Madini alipokuwa anazindua Bodi mpya ya Shirika la Maendeleo ya Petrol alitoa maagizo ya kupitia mikataba yote ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta kupitiwa upya baada ya kuonekana ya kuwa ilikuwa na hisia za rushwa na haina maslahi kwa nchi.

Mheshimiwa Spika, Aidha maelezo kuwa Muundo ulishirikisha wafanyakazi wote management, TUICO na Bodi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Inasema kuwa huo sio ukweli kwasababu muundo uliotengenezwa ambao ulishirikisha hao hapo juu ulipelekwa Wizara ya Nishati na hadi leo haujawahi kujibiwa. Muundo unotelekelezwa sasa ni muundo uliotengenezwa na Wizara na Bodi kwa siri. Kuna vitengo vimefutwa, na kuna kazi zilizofutwa na wanaozishikilia hawajaelezwa hatima yao.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda kupata majibu katika masuala yafuatayo kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini;

(i) Ni hatua gani zimechukuliwa kwa waliobainika kuwa walihusika katika kuingia mikataba mibovu?

(ii) Mikataba yote ya PSA na hususan ile ambayo inakaribia uzalishaji imeongezewa “Addendum” za kifisadi zenye vipengele ambavyo havina masilahi kwa nchi ila vinamnufaisha zaidi mwekezaji? Mikataba iliyoongezewa “addendum” ni ya STATOIL ambao wapom pamoja nja EXONMOBIL na ile ya BG wakiwa pamoja na OPHIR. Kwa sasa OPHIL wameuza baadhi ya hisa kwa Kampuni moja kutoka Singapore. Tunaomba Rais wetu aingilie kati kwani Wizara imethbitisha kutokuwa na uwezo wa kurekebisha hali iliyopo. Serikali ilishakiri ya kuwa mikataba upande wa madini haikuwa kwa maslahi ya nchi. Tunaomba Serikali iangalie kwa upana hii mikataba ya utafutaji na uchimbaji wa gesi kwani kuna kila dalili ya kwamba nchi haitaweza epuka laana ya gesi kutokana na
mikataba iliyopo.

(iii) Badala ya bodi kutekeleza majukumu iliyopewa, kazi yake ni kusafiri nje ya nchi kila kukicha. Mwenyekiti wake amefanya safari sita nje ya nchi kuanzia Januari mpaka May 2014 tu. Inatisha.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Utoaji Wa Vitalu Bila Kufuata Taratibu, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania lilitoa vitalu kwa Kampuni ya OPHIR bila kutangaza Tenda, tunaomba maafisa wote walioshiriki kutoa vitalu kwa Kampuni ya OPHIR wachukuliwe hatua zinazostahili.

Mheshimiwa Spika, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utafutaji na Uzalishaji wa mafuta na gesi amejiunga na kampuni ya Ophir. Kampuni hii ilipewa kitalu bila kufuata sheria za manunuzi, leo mkurugenzi huyu amestaafu amejiunga nayo na kupewa wadhifa mkubwa. Nchi yetu kweli tutafika!

Mheshimiwa Spika, Alieshindwa Kuendeleza Kitalu cha Gesi Analindwa. Kampuni ya HYDROTANZ inayomilikiwa na Bwana SING (SINGASINGA) ambae ndiye aliyenunua IPTL kupitia kampuni ya PAP ndiye mmiliki wa kampuni ya HYDROTANZ ameshindwa kuendeleza kitatu alichokuwa amepewa kwa mujibu wa Mkataba. Alistahili kunyang‟anywa kitalu husika kutokana na kushindwa kukiendeleza ila kutokana na kulindwa na wizara bado ameendelea kumiliki kitalu husika.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inajua kuwa kuhusu Viongozi Walioshiriki Katika Mikataba Mibovu Kama Wa Songo Songo. Cha kushangaza ni kwamba Katibu Mkuu aliyekuwepo wakati wa utiaji saini mikataba inayosemekana ni mibovu ya Songo Songo na PAN AFRIKA Mhe. Rutabanzibwa ndiye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Pan Afrika Tanzania.

Hivi sasa anafanya mbinu waziwazi za kuisafisha Kampuni hiyo ambayo imeonekana kuwa na dosari lukuki za kiutendaji na kimaadili. Kampuni ya PAN AFRIKAN ENERGY inafanya jitihada za makusudi “ku-sabotage” mradi wa bomba la gesi asilia unaoendelea kwa kutotekeleza majukumu yao mya kuongeza kiwango cha gesi asilia kinachoweza kuzalishwa kwa ajili ya mradi huu mkubwa wa serikali.

[...]

- JOHN MNYIKA - UKURASA WA  83- 128 WA HANSARD YA MAJADILIANO YA BUNGE YA 30 MEI 2014

Paul Ngana:

Wadau,

Below is a very good piece written by Zitto sometime ago. In my opinion, anasahau kitu kimoja, kwenye utafutaji wa oil na gesi kuna kupata na kukosa. Na ni mara nyingi hawa watu huwa wanakosa, though the success rate is somehow higher now with advances in technology. Sasa wakipata, some of exploration costs, can be recovered, depending on agreed PSA. Ikibuma, its your loss. As an example Shell to write-off $200 million on Tanzania Well. Now that’s just one well. Drilling ships for offshore wells can cost up 1 million USD per day. So depending on the size of your bock, you might have to continue drilling to gain more data. So yo do the math.

So you can understand why that could be too expensive for individuals. So Prof Muhongo yuko sawa, vitalu vipo wazi for all to bid. Kama, Mengi na wenzake wanaweza, kutafuta mitaji kwenye masoko ya hisa (kama alivyoelezea Zitto hapo chini), please go ahead. Ila wasiseme, kwa sababu nina passport ya Tanzania, nipewe upendeleo. Mimi hicho sikubaliani nacho. Ndio wazawa wapewe kipaumbele, ndio maana kuna local content policy, ila tusijiumize kisa uzalendo. Tuangalie mwisho wa siku taifa tunapata nini. Hela zinazopatikana ziwekwe kwenye sovereign wealth fund kama wenzetu "Sovereign wealth Fund", halafu matumizi yaamuliwe bungeni.

Pia Muhongo yuko sawa, kwamba TPDC awe mwakilishi wa watanzania, there are many successful examples like Saudi Aramco (Saudi Arabia), Petronas (Malaysia), Petrobras(Brazil), PVDSA (Venezuela), Gazprom(Russia) you name it. Ni kweli ndio kuna baadhi ya nchi ambazo unasikia watu binafsi wana hivi vitalu. Kwa mfano kule Nigeria na Russia, utaona hao watu binafsi ni marafiki wa watu jeshini au high level ranking politicians. And some of them, wanakaa na hivi vitalu, halafu wanaziuza tena. Others wanataka quick wins, wanaenda nje wanachukua contractors, na hiyo hela inaishia mifukoni kwao na hakuna faida kwa taifa. Kwa hiyo hapo [juu] Muhongo yuko sawa in my opinion.

Pia alichosema Zitto kwenye conclusion yake ni muhimu sana, uchafuzi wa mazingira ukitokea Mtwara, watakaoumia ni hao watu wa mtwara na sio watu wa arusha. Na kwa uzoefu wangu mdogo kwenye hii sekta, utaona kuwa kwenye maeneo yenye uchimbaji wa gesi/oil huwa wanakuwa masikini kuliko maeneo mengine ya nchi hizo. Wanaofaidika na hizo hela huwa wanaku mbali kabisa na hayo maeneo.

Kitu kingine, skyrocketing of costs of livings, pia kuna issue ya uharamia, target areas for terrorist attacks, majangili etc.  Yaani, majanga juu ya majanga. Nawaonea sana huruma hao watu wa Mtwara, Lindi. Imekula kwao.

Paul

-------------

by Zitto Kabwe

Nani anamiliki rasilimali za nchi

NANI ana miliki ya dhahabu yote iliyogunduliwa Tanzania hivi sasa? Nani ana miliki yote ya misitu iliyopo nchini? Nani ana miliki ya gesi asilia iliyogunduliwa hivi karibuni mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara? Watanzania wachache sana wanayo majawabu ya maswali haya.

Inasikitisha hata Watanzania tuliopewa fursa ya kuwaongoza wenzetu milioni 45 hatuna majawabu na wala hatutafuti majawabu ya swali hili. Viongozi tunawaambia wananchi kwamba “maliasili ya nchi ni mali ya umma.” Ni kweli mali ya umma? Umma ni nani? Hebu tuangalie mfumo wetu wa miliki ya rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia. Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haisemi lolote kuhusu ‘miliki’ ya utajiri wa taifa. Isipokuwa katika ya kifungu cha tisa (c) na (i) na ibara ya 27 (1) suala la maliasili ya nchi limewekewa masharti ya Katiba.

Ibara ya 9 (c) inasema shughuli za serikali zitatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha utajiri wa taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa ujumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine. Ibara ya 9(i) inasema matumizi ya utajiri wa taifa yatatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umasikini, ujinga na maradhi.

Ibara ya 27 inahusu wajibu wa raia kulinda maliasili ya Jamhuri ya Muungano. Ibara ya 9 kuna masharti ya Katiba ya kujenga Ujamaa. Hakuna ibara ya Katiba inayozungumzia ‘miliki’ ya utajiri wa taifa. Suala hili liliachiwa sheria zilizotungwa na Bunge. Kwa suala utajiri tuliochagua kufanyia kazi katika makala haya sheria hizo ni Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Sheria ya Utafutaji wa Mafuta ya Mwaka 1980.

Nani anamiliki madini nchini?
Sheria ya madini ya mwaka 2010 imesema madini ni mali ya umma, hata hivyo, imeweka masharti ya kuhamisha umiliki huu kwa watu na kampuni binafsi kwa mtindo wa leseni. Dhahabu ni mali ya umma pale tu utafutaji wake na hatimaye uchimbaji haujatolewa kwa mtu binafsi. Leseni ikishatolewa miliki (mineral right) inahamia kwa mwenye leseni na hapo taifa linabakia kupata mrabaha tu kama tozo ya uvunaji wa rasilimali hii.

Kiuhalisia, mfumo huu unaruhusu maliasili ya nchi kumilikiwa na watu binafsi wawe raia wa Tanzania au la. Angalia mfano huu.Kampuni iitwayo ZiMinerals LTD kutoka Canada inakuja Dar es Salaam katika Wizara ya Nishati na Madini na kuomba leseni ya kutafuta dhahabu huko Kahama. Wizara inampa leseni ya utafutaji ya mamia ya kilometa za mraba. ZiMinerals inakwenda kujiandikisha katika soko la mitaji la huko Australia na kuanza kukusanya fedha kwa kutumia leseni ya utafutaji dhahabu Tanzania.

Ikishapata fedha inaanza kazi ya kutafuta na baada ya kupata kiwango cha dhahabu wanatangaza na bei ya hisa za kampuni hii zinapanda maradufu. Serikali inaipa kampuni hii leseni ya kuanza kuchimba na kampuni sasa inaanza kuuza dhahabu duniani au inauza miliki hii kwa kampuni nyingine kubwa na yenye uzoefu zaidi au mtaji zaidi. Kitendo cha ZiMinerals kuuza hisa zake huko Australia tayari miliki ya rasilimali iliyopo Tanzania inakuwa inamilikiwa na wananchi wa nchi hiyo au raia wa nchi nyingine yoyote duniani mwenye kuweza kununua hisa katika soko ambalo hisa za ZiMinerals zinauzwa.

Hivi ndivyo inafanyika. Wanakuja watu hawana hata nguo ya kubadili, wanapata leseni wanakwenda kwao kukopata fedha kwenye masoko ya mitaji na wanakuwa matajiri wakubwa kwa kutumia miliki ya rasilimali za Tanzania na Watanzania wanabaki fukara.

Hivyo ndivyo ilivyofanyika Bulyanhulu, Kampuni ya Sutton Resources ilipewa leseni, ikaenda sokoni kufanyia biashara leseni hiyo, wakawekeza dola za Marekani 20,000 kwenye utafutaji kisha wakauza leseni yao kwa Kampuni ya Barrick Gold, kwa Dola milioni 348. Kwa hiyo tunaposema maliasili hii ni ya taifa tunajidanganya tu. Ukishatoa leseni kinachobaki cha taifa ni ule mrabaha wa asilimia nne tu kwa mujibu wa sheria mpya ya madini ya mwaka 2010 iliyoshinikizwa na sakata la Buzwagi.

Kwa upande wa rasilimali ya gesi asilia na mafuta hali ni tofauti. Miliki ya umma inakuwa ni milki ya serikali na inasimamiwa na Shirika la Umma la Mafuta, hivi sasa TPDC. Kwa hiyo, kwa mfano, kampuni ya ZiGas Limited kutoka Australia inapokuja hapa nchini na kuruhusiwa kutafuta mafuta au gesi na kisha kuchimba, inakua imeajiriwa na TPDC.

Ikienda kule Australia kutafuta fedha itauza kwenye soko ile asilimia yake tu, mara nyingi ni asilimia kati ya 80 na 85. Lakini pia hata ikiuza mafuta au gesi, kulingana na kiwango cha mauzo hayo, asilimia sio chini ya 60 ya mauzo baada ya kuondoa gharama za uzalishaji inachukuliwa na TPDC (serikali).Hata hivyo tofauti na madini, mrabaha sasa unalipwa na TPDC kwa serikali na sio hii kampuni ambayo ni kama mkandarasi (contractor) wetu. Kwenye gesi tunaweza kusema mali yetu, ingawa si kwa asilimia 100.

Kwa nini mifumo tofauti?
Hakuna maana yoyote ile zaidi ya umazwazwa (ujuha) tu. Kwa nini kampuni za ndani ama za serikali au za watu binafsi haziendi kutafuta fedha kwenye masoko ya mitaji na kufanya utafutaji na kisha kuvuna utajiri huu? Ni ujuha tu maana yote yanawezekana.

Walipokuja Ophir Energy hapa Tanzania na kupata mkataba wa kutafuta mafuta kwenye kitalu namba moja kule Bahari ya kina kirefu mkoani Mtwara, walikwenda kuuza hisa kwenye soko la mitaji na hisa moja ilikuwa inauzwa senti nne ya Pauni ya Uingereza (4  pences). Huu ulikuwa ni mwaka 2006. Mwaka 2011 baada ya kupata gesi asilia kwenye visima kadhaa, hisa moja ya kampuni hii ilifika senti 654 ya Pauni (654 pences). Licha ya bei kupanda namna hii lakini pia waliuza sehemu ya kampuni yao kwa Kampuni ya BritishGas na kupata mabilioni ya pauni za Uingereza bila Tanzania kupata lolote licha ya biashara hii kuwa ni mali iliyopo Tanzania.

Hivi kweli baadhi yetu tunasimama na kusema gesi asilia mali ya umma? Dhahabu mali ya umma? Almasi mali ya umma? 

Tunawadanganya wananchi. Lazima kufanya mapinduzi ya kifikra na kivitendo. Maandamano ya watu wa Mtwara yasukume . Watanzania kufukua zaidi kuhusu unyonyaji wa utajiri wa nchi. Mapinduzi ni lazima.

Katiba ya nchi sasa iseme kinagaubaga kuwa rasilimali ni mali ya wananchi (sio mali ya umma). Miliki (mineral right) ya utajiri wa nchi iwekwe kwenye mikono ya wananchi wenyewe kwenye maeneo ambayo rasilimali imepatikana au inatafutwa. Serikali itakuwa ni  msimamizi wa uvunaji wa rasilimali hii kwa manufaa ya wananchi wote. Wananchi wa eneo ambalo rasilimali inatafutwa au imepatikana wawe na haki ya kuridhia kuvunwa kwa rasilimali hiyo kabla Serikali Kuu haijatoa ruhusa ya kuvunwa kwa rasilimali hiyo (The right of prior informed consent).

Mapinduzi haya ya umiliki wa rasilimali za nchi kutoka kwa serikali kwenda kwa wananchi wa maeneo yenye rasilimali kutawezesha mrabaha wote unaolipwa na kampuni za uvunaji wa rasilimali kulipwa kwa wananchi hawa kupitia serikali zao za mitaa na majimbo (provinces).

Mapato haya ndio yatafidia kuondolewa kwa wananchi kwenye mashamba yao kupisha uvunaji huu au kufidia samaki wanaopotea kutokana na uchimbaji mafuta na gesi kwenye bahari. Ieleweke kwamba mrabaha si kodi bali ni tozo la fidia kwa kunyonya (kuvuna) mali katika eneo husika.

Viongozi tunaposema maliasili ni mali ya taifa tuna maana fedha zitokanazo na maliasili ni mali za taifa. Hivi tumewahi kujiuliza madhara ya uharibifu wa mazingira nayo ni madhara kwa taifa zima?

Kwa mfano madhara ya kuchimba mafuta kule Mtwara, madhara ya kimazingira ikiwamo sumu yanamilikiwa kwa pamoja kati ya Kigoma na Mtwara au Kigoma itafaidi tu dola zitakazotokana na gesi ya Mtwara lakini Mtwara itaumia peke yake na uharibu mkubwa wa mazingira unaotokana na uchimbaji wa gesi.

Tusiwe na midomo mikubwa kuona fedha za kugawana nchi nzima na kufumbia macho uharibifu mkubwa wa mazingira na upoteaji wa maisha unaowaathiri Watanzania wanaoishi kwenye maeneo fedha hizo zinatoka.

Sumu katika Mto Tigite kule Tarime haigawanywi kwa Watanzania wote isipokuwa mapato ya dhahabu, japo nayo ni kidogo tu maana miliki ni ya kampuni binafsi, inayovunwa na kuchafua maji ya mto huu inagawanywa kwa Watanzania wote. Hatuwezi kuendelea kuwa na taifa ambalo Wilaya ya Geita yenye mgodi mkubwa zaidi wa dhahabu barani Afrika, ukiondoa Ghana na Afrika Kusini lakini ni masikini zaidi Tanzania. Halafu tunasema maliasili ni mali ya taifa. Turudishe rasilimali kwa wananchi.


Sabatho Nyamsenda:

Mie sioni kwa nini debate ya Mengi na Muhongo itulazimishe kuchukua upande ama wa Mengi au wa Muhongo. Mie sifungamani na yeyote, japo napigia chapuo dola kuwa na uhodhi katika uwekezaji wa uchumi.

Tarehe 9 Desemba 2013 kulikuwa na Kongamano la Udasa kuadhimisha kumbukizi ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara. Kongamano lile liliwaleta pamoja Mengi na Muhongo. Mwenyekiti wa Udasa wakati huo (ambaye baadaye alijiteua kuiwakilisha Udasa katika Bunge la Katiba) anafahamika kama kada wa CCM, na katibu wake ni sympathiser wa upinzani. Katika mjadala ule Muhongo alipewa nafasi ya mwisho kuzungumza na akapangua hoja zote za Mengi na kisha kulipua bomu kuwa Mengi anamiliki ardhi ambayo ni mara tatu ya mkoa wa Dar es Salaam.

Baada ya bomu la Muhongo washiriki waligawanyika katika makundi mawili. Vijana wa CCM wakiwa nyuma ya Muhongo, na wale wa CDM/CUF wakiwa nyuma ya Mengi. Likaitishwa Kongamano la pili (kwa kuwa la kwanza lilikuwa limekwisha) hapo hapo Nkrumah, huku viongozi wa upinzani (Lissu, Mnyika, Esther Wassira na Mtatiro) wakipanda jukwaani na Mengi, na kusema kuwa Muhongo ni mwongo. Muhongo kabla hata Kongamano la pili halijaanza, Muhongo akakata umeme wake, huku askari wakitumwa kuwaondoa washiriki ukumbini.

Nje ya ukumbi vijana wa vyama walitaka kupigana. Niliingilia ugomvi wa kundi moja na kuwauliza, “Hivi mnachopigania ni nini hasa?” Hawakuwa na hoja. Baada ya kutoa mhadhara mfupi, nikahitimisha: “Muhongo ni mwongo, na Mengi kaficha mengi”! Nikawaambia kama wanapigania maslahi ya wanyonge basi wasichukue hizo pande mbili.

Na kwa kweli, ni pande mbili zenye lengo moja. Muhongo na Mengi hawatofautiani: wote wanapigia chapuo uwekezaji toka ughaibuni. Wanapotofautiana ni nani awe dalali? Mengi anasema nafasi ya udalali ya TPDC ichukuliwe na “wazawa”. Muhongo anasema ifanywe na dola kupitia TPDC. Kwa hiyo hapo bado kuna dhana ya uchumi tegemezi, ambao mashabiki wake (akina Mwapachu) wanasema “pesa tutapata toka huko nje”.

Zitto Kabwe:

Ni kwa vipi Muhongo anataka TPDC iwe ndio dalali wa dola?

Mjadala mzima huu upo katika msingi wenye nyufa kwani suala sio Mengi v Muhongo. Suala ni 'nani mmiliki wa rasilimali hizi za asili?

TPDC ni mtoa leseni na msimamizi tu wa vitalu. TPDC imepewa haki ya kumiliki mpaka 20% ya hisa za kampuni za uwekezaji katika sekta (kwa kununua hisa hizo). Pia TPDC ni mpokeaji wa fedha za Serikali zinazotokana na 'profit oil/gas ' pamoja na mirahaba. ' hadithi ' ni pale ambapo Watanzania wanaambiwa kuwa TPDC inamiliki kwa niaba yetu, kivipi? Wapi?

Wakati wa zabuni ya kugawa vitalu vipya Rais alinukuliwa akisema kuwa ' TPDC itakuwa na hisa 80% kwa niaba ya watanzania ' kitu ambacho kilionyesha ujuzi mdogo sana wa viongozi wetu kwenye suala la mafuta na gesi. Zipo wapi hizo hisa 80%? Hii hadithi inayorudiwa rudiwa bungeni na kukaririwa bila kuhojiwa. Hakuna kitu kama TPDC kumiliki kwa niaba yetu. TPDC ni mpokeaji wa mgawo wa mrahaba na mafuta au gesi Asilia ya ziada. Umiliki wa mpaka 20% ni ' option'  iwapo TPDC itataka kununua. Option hii ipo kwenye mikataba yote, apewe mtanzania kitalu au mgeni. Lakini ni option ambayo sio ya ' lazima ' na sio ya bure.

Ni dhahiri Watanzania wanapaswa kumiliki makampuni haya. TPDC inapaswa kuwa na kampuni tanzu ( Niliwahi kushauri mwaka 2010 kampuni hii kuitwa PetroTan). Kampuni hii tanzu ikamiliki hizo haki za TPDC katika kampuni za utafutaji na 50% ya kampuni hii ikauzwa kupitia soko la hisa na nusu iliyobakia ikamilikiwa na TPDC au Msajili wa Hazina.

Hadithi ni kuwaambia watanzania kuwa wanamiliki kupitia TPDC wakati sio kweli. Ni hoja ya kupinga hoja lakini iliyojengwa kwenye msingi dhaifu kwa pande zote zenye kushindana hoja hizo

George Fumbuka:

Kwa uelewa wangu TPDC ni DEPOSITORY ya share za Watanzania, kama UTT walivyopewa hisa za TBL na TCC kama seed capital. Baadaye TPDC watadwnloand hisa hizo kwa wananchi. Katika hiyo 80% ndiyo ya kudownload. Where is the problem? 

Demere Kitunga:

Hiyo 80% inatoka wapi kama wanaruhusiwa 20% tu, labda kama sikumuelewa vizuri Zitto.

Zitto Kabwe:

Huo uelewa wako unatokana na nini? Hizo ni hisia zako au unataka iwe hivyo lakini sio uhalisia. 

Hakuna sheria inayosema TPDC ni depository 

Salim Khatri:

Zitto, Twende taratibu. Mimi nikiwekeza hela yangu kwenye kampuni nachotaka zaidi humo ni hiyo faida inayotokana na hiyo kampuni. Na nikisia kuwa hiyo kampuni ina tabia ya kuingiza hasara badala ya faida, mimi hiyo kampuni sitawekeza. Naamini hata wewe hautawekeza kwenye hiyo kampuni. Hivyo hivyo kama Taifa (siyo individual wenye kuyatolea macho hayo mafuta na gesi) tunachojali na kutaka ni kuwa hiyo faida wanayopata hayo makampuni pale wanapochimba hayo mafuta na gesi na sisi tunafaidi, again tunafaidi kama Taifa na siyo individuals, yaani faida hizo ziingie kwenye mfuko wa serikali zikajenge hospitali, shule na mambo mengine ya maendeleo. Kumiliki kampuni (“all affairs” kama zile za IPTL) ni pamoja na kumiliki madeni na matatizo ya kampuni hiyo. Nani anataka hayo?

Kumiliki asilimia kadhaa ya faida ni bora kuliko kumiliki hisa za kampuni. Huo ndiyo umilikaji anaozungumzia Rais Jakaya Kikwete. Kwa model PSA Tanzania kama nchi itakuwa inamiliki faida ya mpaka 80% yanatokana na shughuli za kuchimba mafuta/gesi. Mafuta yetu, wanachimba wao. Faida tunagawana kwa mujibu wa uzalishaji. Kuna ubaya gani hapo?

[...]

Kwanini tuitake serikali iwekeze hela zetu ama ikakope kuweka maisha yetu rehani kwenye biashara ambayo ni “kamari” tu? Alex Kobalyenda kauliza swali la kimsingi kabisa “If we can’t feed ourselves, who will agree tukope to gamble?”


Nafikiri wengi wengu hampendi huu mjadala uwe kati ya yale anayoyasema Prof. Muhongo na yale yanayodaiwa na Mengi kwa sababu hizo ndizo hoja kuu mbili. Mmoja anataka Tanzania kama taifa lifaidike collectively, mmoja anataka few selected Tanzanians wafaidike zaidi. Na ndiyo hoja za eti wanaounga mkono hoja ya Prof. Muhongo “wana wivu”.

Dr. Antipas Massawe:

Watanzania wanao uwezo mkubwa sana wa kuwekeza kwenye sekta ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta ya petroli na gesi asilia hapa nchini kwa sababu mtaji unaohitajika ni sehemu kidogo mno ya thamani ya hatimiliki za vitalu husika kwenye utafutaji na uchimbaji wa hiyo raslimali yetu ya madini. Kuwapa watanzania hatimiliki za vitalu hivyo ni kuwapa uwezo wa kuwagawia wawekezaji wa kigeni sehemu kidogo tu ya hisa kwenye hatimiliki hizo ili wawekeze mtaji kidogo unaohitajika kuvijengea vitalu husika uvutio kwa wawekezaji wengine matajiri zaidi na/au taasisisi zinazotoa mikopo wa kuwekeza mtaji husika kwenye kukamilisha utafutaji na kuanzisha uchimbaji wa vitalu vitakavyogundulika kuwa na raslimali zinazochimbika kwa faida. 

Kilichotakiwa kifanyike ni serikali kuwezesha ubia kati ya watanzania na serikali yao (kupitia TPDC) kwa kuupa hatimiliki za vitalu vyote vya mafuta ya petroli na gesi asilia uweze kugawa sehemu kidogo tu ya hisa kwenye hati miliki hizo kwa wawekezaji wa kigeni watakaochangia mitaji midogo inayohitajika kuvifanya viwe kivutio kwa wawekezaji wengine wakubwa na/au taasisi zinazotoa mikopo kujinunulia sehemu nyingine ya hisa za vitalu hivyo kwa njia ya kuwekeza mtaji utakaohitajika kukamilisha utafiti na kuanzisha uzalishaji kwenye vitalu vitakavyogundulika kuwa na rasilimali zinazochimbika kwa faida.

Tunapogawa vitalu vya utafutaji kwa wageni tumewapa pia mtaji wa kuviendeleza ambao ni sehemu kidogo sana ya dhamani ya hatimiliki ya vitalu hivyo kwenye soko. Wote wanaosema watanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye sekta ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia hapa nchini ni wasiolewa biashara hiyo inakwendaje, na hivyo kutokuwa na uelewa wa namna gani serikali ingeweza kuwawezesha watanzania kuwa wamiliki wakuu kwenye biashara hiyo na kuliletea taifa manufaa makubwa zaidi. Nimechangia mada kadhaa kuhusu namna watanzania wanavyoweza kushiriki kwenye utafutaji na uchimbaji madini hapa Tanzania na kuiletea manufaa mkubwa zaidi kwenye blog ya GOXI hapa: Antipas Massawe's Blog - GOXI <goxi.org/profiles/blog/list?user=39h14kv44tucu>

Chambi Chachage:

"TPDC will continue to attract International Oil Companies through promotional campaigns as a strategy to maintain the momentum of petroleum exploration in the country....TPDC will continue to participate in Production Sharing Agreement negotiations with International Oil Companies interested to take Exploration Licences on basis of available data and information" - Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC),14 July 1998

"To encourage investments and attract international oil companies to operate in the country, Tanzania shall strive to maintain competition in the licensing process through carefully planned and transparent license bidding rounds and regular review of fiscal framework. The rounds should aim at attracting a variety of technically and financially qualified applicants. These principles on licensing shall be entrenched in legislation...The rapid growth of the petroleum upstream sub-sector, and huge natural gas discoveries, prompted the need to review and update the key legislation governing petroleum upstream in the light of this policy so as to facilitate its implementation, appropriately capture the recent changes in the industry and prudently manage the exploration, development and exploitation of petroleum in the country. The provisions that need to be revisited or added in the legislation include the following .... Review exploration license period. ii. Review the exploration licence acreage size. iii. Government benefits from all transactions of assets related to in-situ petroleum resources...e) Provision for the clarification of roles and responsibilities of the various institutional entities involved in the petroleum activities (Ministry, regulator, national oil company)...."  - The National Petroleum Policy of Tanzania, Draft, 3 July, 2014

"Mheshimiwa Spika, sheria ambayo tunayoileta na nimeshaongea na wakuu wangu wote kwamba hii gesi iliyogundulika tusipokuwa waangalifu tunaweza tusifaidike. Ndiyo maana ni lazima tuwe waangalifu kwa sababu
huyu mtu akivuna gesi, sasa tuamue je, hizo fedha kama kitalu ni chake ni fedha zake na familia yake, lakini kama ni za TPDC ni zetu wote, za Watanzania wote. Kwa hiyo msidanganywe na hadithi yoyote na tutakuja hapa, sheria tunayoileta hapa ya sovereign fund ni kwamba zile fedha hata Hazina hawatazichukua zile fedha kwamba yamepatikana mabilioni tunaenda tunayamwaga yote pale Hazina, hakuna kitu kama hicho. Patatengenezwa mfuko maalum na fedha zile hazitatoka bila ya uthibitisho wa Bunge"- Minister of Energy & Minerals, 30 May 2014

"TPDC ni mtoa leseni na msimamizi tu wa vitalu. TPDC imepewa haki ya kumiliki mpaka 20% ya hisa za kampuni za uwekezaji katika sekta ( kwa kununua hisa hizo ). Pia TPDC ni mpokeaji wa fedha za Serikali zinazotokana na ' profit oil/gas ' pamoja na mirahaba. ' hadithi ' ni pale ambapo Watanzania wanaambiwa kuwa TPDC inamiliki kwa niaba yetu, kivipi? Wapi? Wakati wa zabuni ya kugawa vitalu vipya Rais alinukuliwa akisema kuwa ' TPDC itakuwa na hisa 80% kwa niaba ya watanzania ' kitu ambacho kilionyesha ujuzi mdogo sana wa viongozi wetu kwenye suala la mafuta na gesi. Zipo wapi hizo hisa 80%? Hii hadithi inayorudiwa rudiwa bungeni na kukaririwa bila kuhojiwa. Hakuna kitu kama TPDC kumiliki kwa niaba yetu. TPDC ni mpokeaji wa mgawo wa mrahaba na mafuta au gesi Asilia ya ziada. Umiliki wa mpaka 20% ni ' option'  iwapo TPDC itataka kununua. Option hii ipo kwenye mikataba yote, apewe mtanzania kitalu au mgeni. Lakini ni option ambayo sio ya ' lazima ' na sio ya bure." - Mwenyekiti wa PAC, 12 January 2015

Zitto Kabwe:

Pia tusichanganye hisa na mgawo wa mapato (profit gas or oil). Mjadala hapa ni umiliki wa watanzania au ushiriki wa watanzania katika sekta. 

[…]

Pia ninadhani mjadala huu ni muhimu sana kwa ajili ya kuona namna watanzania wanaweza kushiriki katika sekta hii. Napendekeza mjadala uitwe ' Watanzania na Sekta ya Mafuta na Gesi' 

Salim Khatri:


Kuna faida gani ya kumilika hisa za kampuni (advantage) dhidi ya kupata mgawo wa mapato (profit) ya hiyo kampuni?[..]Dr. Antipas Massawe:

Hapana,  kumiliki hisa kadhaa za hatimiliki za vitalu vya mafuta ya petroli na gesi asilia kuna manufaa makubwa zaidi ya kuwa na hisa ya faida itakayopatikana kutokana na uvunaji kwenye vitalu vitakavyogundulika kuwa na rasilimali inayovunika kwa faida.

Kuwa na sehemu ya hisa za hatimiliki za vitalu kunamwezesha mwenye nazo azitumie kama rehani ya kujipatia mikopo kwa ajili ya kuwekeza kwenye miradi mingine inayozaa faida kubwa, ya uhakika na kwa haraka zaidi mara kadhaa na kujipatia faida kubwa maradufu ya thamani ya hisa zake kwenye hatimiliki za vitalu husika ambazo bado ziko mikononi mwake au thamani ya rasilimali yote iliyomo kwenye vitalu husika.

Kuwa na sehemu ya hisa kadhaa za hatimiliki za vitalu hivyo pia humwezesha kuzitumia kama reheni ya kujichukulia mikopo kwa ajili ya kuwekeza kwenye biashara nyingine zenye kuleta faida kubwa na kwa haraka zaidi hata kama vitalu husika vitakuja vionekane havina rasilimali yoyote inayovunika kwa faida.

Kwa hiyo faida kubwa na yenye maana kubwa zaidi kwenye sekta ya mafuta na gesi ni ile inayotokana na utumiaji wa hisa kwenye hatimiliki za vitalu husika kama rehani ya kujichukulia mikopo kwa ajili ya kuwekeza kwenye miradi mingine yenye faida kubwa, ya haraka na ya uhakika zaidi mara kadhaa huku hisa za mhusika kwenye hatimiliki ya vitalu husika kwenye utafutaji unaoendelea zikiendelea kubakia palepale.

Ndio maana wawekezaji wakishagundua gesi huwa wakiwauzia wawekezaji wengine watakaochimba ili kwenda kuwekeza kwenye kujipatia hisa nyingine nyingi zaidi kwenye vitalu vingine vingi zaidi vya utafutaji ili waweze kuendelea kutumia hisa hizo kama rehani ya kujichukulia mikopo kwa ajili ya kuwekeza kwenye miradi mingine yenye kuleta faida kubwa, ya haraka na ya uhakika zaidi huku wakisubiria kuuza hiza zao na kujipatia faida kubwa kwenye vitalu vitakavyokuja kugundulika vinachimbika kwa faida.

Bonanza kwenye biashara ya madini (hasa mafuta na gesi) hupatikana kwa njia ya kutumia hisa kwenye hatimiliki za vitalu husika kwenye utafutaji unaoendelea kama rehani ya kujichukulia  mikopo ya kuwekeza kwenye miradi mingine inayoleta faida kwa haraka zaidi, na kuuza hisa kwenye hatimiliki za vitalu vitakavyokuja kugundulika kuwa vina rasilimali inayochimbika kwa faida, na mtaji utakaopatikana ukaendelea kuwekezwa kwa kwenye kujipatia hisa za hatimiliki kwenye vitalu vipya vya mafuta na gesi na sio kusubiria mgawo wa faida itokanayo na uchimbaji ambayo huwa ni kidogo sana.

Wachimbaji huwa wakiendelea na biashara yao ya uchimbaji ingawa hawapati faida kubwa kama wanaocheza na hisa kwenye hatimiliki za vitalu vya utafutaji kwa sababu tu uchimbaji ndiyo taaluma wanayoijulia vizuri zaidi. Wenye kupata faida kubwa kwenye uchimbaji ni wale wanaochangia mitambo, huduma  na vifaa vingine husika kwenye shughuli hiyo ya uchimbaji.

TUSISAHAU KWAMBA MITAJI HUSIKA KWENYE UTAFUTAJI NA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI NI SEHEMU KIDOGO SANA YA THAMANI YA HATIMILIKI ZA VITALU HUSIKA.

Kwa hiyo Tanzania inapoteza kwa kiasi cha kutisha pale ilipokwepa kujibakizia hisa kubwa kwenye hatimiliki za vitalu husika kwenye utafutaji wa mafuta na petrol unaoendelea na badala yake ikaamua isubirie mgawo wa faida itakayopatikana na uchimbaji kwenye vitalu vitakavyokuja kugundulika kuwa na rasIlimali inayochimbika kwa faida ambAvyo ni chini ya 1% ya vitalu vyote husika kwenye utafutaji wa mafuta na gesi ambavyo vyote huwa vikiwaletea wenye hisa kwenye hatimiliki zake faida kubwa pale hisa hizo zinapotumika kama rehani kwenye kujichulia mikopo ya kuwekeza kwenye biashara nyingine zinazoleta faida kubwa, ya uhakika na haraka zaidi mara kadhaa wakati utafutaji kwenye vitalu ukiwa bado unaendelea.

Salim Khatri:


Ahsante kwa majibu yako. Naona hapo umeonyesha faida tu ya biashara ya “exploration” na sana sana faida ya kuweza kupata mkopo kutumia hati miliki za vitalu kama rehani (ambayo bado nina mashaka kama kuna benki zinatoa mikopo ya namna hiyo na kuchukulia “kitalu” kama security hasa ukizingatia benki zetu zinataka “tangible assets” kama security). Kwenye exploration ni kamari ama “pata potea”, aidha unapata gesi/mafuta ama hupati kitu baada ya kutumia mabillioni kuchungulia huko chini. Nafikiri hapo ni wazi serikali yetu haiko tayari kucheza huo upatu/kamari. Prof. Muhongo kasema katafute wawekezaji ingieni nao ubia mkashindanie hizo. Hakuna anayekatazwa.


Swali langu liko kwenye uchimbaji. Kumiliki hisa za kampuni zina faida gani za ziada (advantage) juu ya kupatiwa mapato ya “gesi ya faida” (siyo faida ya kampuni)?

Chambi Chachage:

Kwa hiyo "mgawo" wa mapato na "umiliki" wa chanzo cha mapato hayo haviendani? Toleo hilo la rasimu ya sera lililotoka miezi miwili tu baada ya hayo maneno ya Waziri yenyewe haivihusianishi? Haipaswi kuvihusianisha kama Waziri alivyovihusianisha? Hadithi yao ni nini - hayo mabadiliko waliyotaka kuleta 2014 au hicho kilicho(kuwe)po?

"Mheshimiwa Spika, gesi asilia na mafuta: Napenda kurudia tena hakuna Mtanzania aliyezuiwa, hayupo wala hatujamzuia Mtanzania yeye akatafute kampuni waje naye akiwa na ubia hatujazuia, na tuna kampuni ya Watanzania ambayo tayari inafanya kazi na Wa-Australia na wote hata wao wenye kampuni hiyo walikiri kwamba hawana fedha, hawana teknolojia ndiyo maana wametmafuta kampuni ya Australia wafanye nayo kazi. Kwa hiyo ndugu zangu kama nia ya mtu ni kitalu, wewe njoo na wawekezaji mshindane. Lakini nataka kusisitiza tena haitatokea kwamba kuna mtu atapewa kitalu yeye na familia yake, haiwezekani! Na hii hata mtu aandike asubuhi na mchana, aimbe, haiwezekani! TPDC ndiye anayetuwakilisha, anawakilisha Watanzania wote tajiri na maskini, lakini hamna vitalu vya familia hapa... na ndiyo maana kama tunakuwa na sovereign fund ni hatari sana kuruhusu mtu na familia yake awe na kitalu. Haya yote ndiyo nilikuwa nataka ayaweke kwenye bajeti, sasa yakawa ni hadithi tu" - Minister of Energy & Minerals, 30 May 2014

"The Government Shall.... Encourage local companies to enter into partnerships with international companies as one of the means of acquiring technology transfer and developing competence in Tanzanian companies" - The National Petroleum Policy of Tanzania, Draft, 3 July, 2014

Zitto Kabwe:

Mgawo wa mapato (production sharing) ni tofauti sana na umiliki wa kampuni. Tofauti kubwa. Hata kama TPDC isingepewa haki ya kumiliki hisa hizo mpaka 20% bado mgawo wa mapato ungekuwa vile vile tu. 

Sera hizo ni hadithi kubwa zaidi. Sera ya upstream? Au unasemea sera ya uchuuzi? Sera ngapi za Tanzania ni hadithi tu, zinatungwa na kuwekwa kwenye makabati. 

Sheria ya gesi ipo wapi? Sheria ya utafutaji mafuta (Mpya ) ipo wapi? Sera ya matumizi ya fedha ipo wapi? Natural gas master plan ipo wapi? 

Hadithi njoo uwongo njoo. Porojo tu 
---

MJADALA UNAENDELEA KWENYE:

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP