Friday, August 28, 2015

Kaskazini?

"La pili ni hii ya ukanda. Tumesoma jinsi watamani urais hujipangia mikakati ya kuungwa mkono na watu wa kanda anakotokea mgombea. Yaani bila aibu au kificho tunasoma kwamba kuna kamati au vikundi vya kikanda vinavyopanga na kuweka mikakati ya kufanikisha azma ya mtu yao. 

Ukanda ni kama ukabila. Ni sumu ileile ya kuingiza dini au ukabila katika siasa. Tunayempigia kura za kisiasa ni Mtanzania na sio Msukuma au Muhaya.

Tuwe waangalifu. Tusihatarishe amani yetu. Tukijitumbukiza kwenye shimo la kuwania madaraka kupitia udini, ukabila au ukanda, tutakuwa tumeingia katika janga lisilo na mwisho.

Wananchi na hasa wanazuoni, kwa kauli moja tukomeshe jambo hili kabla halijazoeleka" -

Issa Shivji

8 Januari 2014

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP