Friday, October 9, 2015

Kwa nini hawaleti haya mawazo nyumbani?

Waafrika kupigwa butwaa Ughaibuni hakujaanza leo. Pamoja na harakati za kupinga Ubeberu wa nchi za 'Magharibi', hali hiyo imeendelea kutusumbua. Hata Wanamapinduzi wa Kiafrika hupatwa na hisia hii. Zifuatazo ni nukuu na rejea kadhaa zinazoonesha kwamba kuna hitaji kubwa sana la kubadilisha hali ya nchi zetu ili tusiendelee kubaki na bumbuwazi japo kwa kiasi kikubwa mabibi na mababu zetu wameshiriki kujenga nchi za watu:

Mwaka 1932


Mwaka 1984

"[H]ivi hawa viongozi wetu akina Msuya, etc. wanapokuja Washington kila mwaka, hawaoni hizi infrastructure za wenzetu? Kwa nini hawaleti haya mawazo nyumbani? - Freeman Mbowe (Kwa mujibu wa Emmanuel Muganda)

Mwaka 2015

Chambi Chachage:

[P]ia nilifanikiwa kufanya utafiti kwenye makavazi ya maktaba yao kuu [ya Chuo Kikuu cha Cambridge] na za Colleges zao 3 kati ya Colleges 32 walizonazo - wamejipanga vizuri mno, natumai ipo siku nasi Watanzania tutajipanga hivyo 

Anna Mghwira:

Ninajua inawezekana, na kuwa tunahitaji / tutahitaji kujikomboa, tunahitaji kujikwamua katika mfumo huu na kuhakikisha kuwa tunaanza kusimama kama watu, kama taifa/mataifa ya Afrika...sehemu ya dunia. 

Nguvu kubwa ya wengi inahitajika kufikia lengo hili, la sivyo naona kama waliotangulia pia wasipokubali kushirikiana nasi katika vita hii, itatuchukua muda mrefu sana kuwapinga na kujikwamua nao.

Mgune Masatu:

Nchini Japan, mathalan, suala la usafi na kutupa takataka linaanza kufundishwa nursery schools. Watoto hao wanafundishwa namna ya kutenganisha takataka (plastics, burnables, etc) na wanadeki vyoo wao wenyewe - I was so surprised! Na yote hayo yanakuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku. Jambo kubwa nililojifunza kutoka kwa wajapani ni kuweka maslahi ya umma kwanza kisha ndio maslahi binafsi yanafuata. Jana nilibahatika kuingia kwenye maktaba moja ya ughaibuni - hakyamama sina maneno ya kuelezea! We will have a long way to go with our current mentality.

Aikande Kwayu:

Well, I still remember some of the main points of which I thought contributed to Japan’s economic growth and left Tanzania hundreds years behind despite lots of potential that my country has. http://aikandekwayu.com/japan-from-my-eyes/

Mathew Mndeme:

Nadhani swali alilojiuliza Mbowe hiyo miaka 30 iliyopita ni maswali ambayo kila Mtanzania anayeipenda nchi yake na kuumizwa na hali iliyoko anajiuliza siku ya kwanza anapotoka nje ya mipaka na nchi yetu, hasa anapokwenda nchi zinazopendwa kutembelewa na wale "waliojaliwa" kupewa/kujipa nafasi ya kutuongoza kisiasa na kitaaluma pia. 

Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita mimi na watanzania wengine tuliokua hatufahamiani tulikutana kwenye ndege tukielekea chuo kimoja huko [Uru] Kishumundu [i.e. UK/Uingereza] kuanza masomo kwa muda wa miezi kadhaa. Wote ilikua mara yetu ya kwanza kufika kwenye ile nchi. Kesho yake tukaamua tutembee kidogo kuona mazingira. Tulijikuta wote tunashangaa kila kitu tunachokiona na kwa muda mwingi mjadala wetu ulikua ni kujuliza swali hilo hilo:

Viongozi wetu wakija huku huwa wanafuata nini? 

Huwa wanaona nini? 

Mbona vingine tuvionavyo huku vinahitaji maamuzi tu na ushawishi na vikabadili hili na lile bila hata kuhitaji rasilimali?

Huwa wanajisikiaje kutembelea huku kila siku halafu wanarudi nyumbani wanaendelea na maisha "business as usual" hadi watakapopata safari nyingine?

Haya mamilioni wanayokuja kuyatumia huku kila siku kwa mikutano, semina, kujifunza, mafunzo ya vitendo, ziara, mikutano...kwa nini basi angalau yasingerudisha fadhila nyumbani kwa kuiga mawazo na vitu wanavyokutana navyo huku?

Tulipoanza kuingia madarasani na kuona mfumo wa elimu na miundombinu yake tukaanza tena kujiuliza:

Mbona kule kwetu karibu maprofesa wote tunasikia wamesoma huku? Kwani hawakupata cha kujifunza wapeleke kwetu?

Mbona kule kwetu wanawaza kikwetukwetu sana kama vile hawajawahi kukutana na mawazo mapya?

Mbona kuna baadhi ya vitu wangeweza kufanya kwenye vyuo vyetu vikaleta mabadiliko na maboresho hata bila rasilimali nyingi?

Mbona, ..
Mbona,...

Nakumbuka mjadala ule uliendelea kila mara kwa miezi kadhaa hadi tuliporudi "nchi ya kitalii yenye mlima Kilimanjaro na visiwa vya Zanzibar". Tulipofika nyumbani tukaanza kushangaa kuanzia pale "Njia Panda ya Ulaya": 

Kwa nini hapa kwetu kuko hivi? mbona hewa nzito? kuna harufu, kuna foleni, kuna vumbi, kuna,...kuna...kuna...kuna...kuna ...kuna...

Baada ya wiki chache nasi tukazoea kuwa haya ndiyo maisha, tukaacha kulalamika, tukaendelea na maisha na kusahau tuliyokuwa tunayashangaa huko Kishumundu huku tukiyazoea tena yale ya kwetu. Nikahisi huenda lililotukabili sisi ndilo linalo/lililowapata akina "waliolala mauti", akina Msuya, akina Warioba, akina Salim, akina Malecela, akina Miwinyi, akina Mkapa, akina Sumaye, akina Lowasa, akina Kikwete, akina Pinda na akina "Watakaokuja".

Jibu jepesi nililonalo hadi leo (maana gumu sijalipata) ni kwamba:

 "Sisi tunaridhika kirahisi sana na kwa vitu vidogo sana hivyo ya nini kujichosha? Zaidi ya yote hatujaona sababu ya msingi ya kuyafanya maisha yetu kuwa na thamani na dunia yetu ituzungukayo kutuvutia, kutupa matumaini na hatuthamini kuishi/maisha ya furaha"

Huenda tukaendelea kusimulia maajabu ya tunayokutana nayo huko Kishumundu kwa miongo mingine mingi sana hasa ukichukulia kwamba wao bado hawajaridhika na wanatafuta kuhamishia makazi kunako "Pluto" kama sio "Sayari Nyekundu".

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP