Tuesday, January 19, 2016

Alichokisema CAG kuhusu Ujasiriamali wa Kisiasa

"Mimi nafikiri inawezekana ikawa Escrow ni sehemu ndogo ya sehemu kubwa ya utendaji mbaya kwa watu katika nchi yetu. Tunazungumzia kitu kinaitwa Entrepreneurial Politics [Ujasiriamali wa Kisiasa], yaani kuchanganya siasa na ujasiriamali. Kwa hiyo watu wanaingia katika siasa lakini kwa nia ya kwamba wapate faida binafsi katika siasa. Na jambo hili likitokea mara nyingi inatokea watu kutafuta ujanja ujanja wa kuweza kupata pesa. Na kama utatazama mambo yote yaliyofanyika zamani: Uuzaji wa nyumba za Serikali, unawapa watu wafanye uamuzi, watu ambao wao wenyewe ni beneficiaries [wafaidika]; hiyo ni moja katika mfano wa political entrepreneurship [ujasiriamali wa kisiasa]. Ukitazama lile suala la uchukuaji wa pesa za Benki Kuu ya Tanzania, ni ishu hiyo hiyo ya political entrepreneurship, watu wanachanganya faida binafsi na maamuzi ambayo wanatakiwa kufanya katika ofisi za Serikali. Jambo hilo tukishindwa kulidhibiti matatizo haya huenda yakawa mengi zaidi. Na tunafikiri kwamba katika kipindi hiki Mungu amejalia tupo sisi tutalisemea zaidi jambo hilo" - Profesa Mussa Assad

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP