Wednesday, February 17, 2016

FASIHI YA VIJANA WA LEO

Ni dhahiri tunafahamu nafasi ya fasihi katika ukombozi wa nchi yetu na wananchi wake. Fasihi ilikuwa (na inaendelea kuwa) mstari wa mbele katika kulikomboa bara na taifa letu. Fasihi ilikuwa na mchango mkubwa katika ukombozi wa fikra na kuamsha na kuhamasisha harakati va kuupinga udhalimu wa aina yeyote hapa barani kwetu kwa miaka na miaka. Kutokana na fasihi yetu hii (hususani andishi) nchi yetu imepata kubarikiwa na wanafasihi mashuhuri (kila mtu anaweza akamtaja wake).

Licha ya utajiri wa fasihi tulionao leo... idadi ya waandishi miongoni mwa vijana wa leo (na hata idadi ya wale wenye mapenzi ya usomaji) inatilia mashaka makubwa sana. Hivyo, taasisi yetu pendwa - Soma (Soma Book Cafe) katika kukuza na kuhamasisha uandishi kwa vijana wa leo - imeaandaa na inaratibu - shindano la hadithi fupi kwa wanafunzi wa shule za sekondari kwa ajili ya kuendeleza upenzi wa fasihi na ikilenga kuweza kuzalisha kazi mpya za vijana wa leo.

Soma, inachukua nafasi hii adhimu kukuomba wewe kama mdau wa usomaji, maarifa, elimu na maendeleo kuwashirikisha, kuwasihii na kuwahimiza - WATOTO, WAJUKUU na VIJANA wetu walioko katika shule za Sekondari kushiriki SHINDANO hili la Hadithi Fupi ilimradi kuendelea kuudumisha utamaduni wetu adhimu wa Uandishi.

Maelezo zaidi kuhusu shindano hili yameorodheshwa kwenye kipeperushi kilichoambatanishwa kwenye ujumbe huu.

Shukrani kwa ushirikiano wako.

ADDRESS: Mlingotini Close, Plot Number 53 Regent Street - Mikocheni A, Dar es Salaam
PHONE: 0673014071

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP