Monday, October 31, 2016

Ripoti za CAG kuhusu Ubia wa NSSF Zinapingana?

Ripoti za CAG kuhusu Ubia wa NSSF na AZIMIO zinapingana?

Chambi Chachage


Nianze kwa kukiri kwamba mimi ni 'mshabiki' wa 'weledi' na 'ujasiri' wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Juma Assad. Japo hatufahamiani, nilivutiwa  na umakini wake nilipokuwa namwona asubuhi kwenye kilima cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akifanya mazoezi kwa umakini mkubwa. Alipoteuliwa kuwa CAG nilifurahi hasa baada ya kuyasikiliza mahojiano yake na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa mwaka 2014. Katika mahojiano hayo alisema:

"Mimi nafikiri inawezekana ikawa Escrow ni sehemu ndogo ya sehemu kubwa ya utendaji mbaya kwa watu katika nchi yetu. Tunazungumzia kitu kinaitwa Entrepreneurial Politics [Ujasiriamali wa Kisiasa], yaani kuchanganya siasa na ujasiriamali. Kwa hiyo watu wanaingia katika siasa lakini kwa nia ya kwamba wapate faida binafsi katika siasa. Na jambo hili likitokea mara nyingi inatokea watu kutafuta ujanja ujanja wa kuweza kupata pesa. Na kama utatazama mambo yote yaliyofanyika zamani: Uuzaji wa nyumba za Serikali, unawapa watu wafanye uamuzi, watu ambao wao wenyewe ni beneficiaries [wafaidikaji]; hiyo ni moja katika mfano wa political entrepreneurship [ujasiriamali wa kisiasa]. Ukitazama lile suala la uchukuaji wa pesa za Benki Kuu ya Tanzania, ni ishu hiyo hiyo ya political entrepreneurship, watu wanachanganya faida binafsi na maamuzi ambayo wanatakiwa kufanya katika ofisi za Serikali. Jambo hilo tukishindwa kulidhibiti matatizo haya huenda yakawa mengi zaidi. Na tunafikiri kwamba katika kipindi hiki Mungu amejalia tupo sisi tutalisemea zaidi jambo hilo."

Ujasiri huo wa Profesa haukuishia huko 'nje'. Wakati wa sakata la Escrow, alinukuliwa na Shirika la Taifa la Habari (TBC) akisema:


Baada ya aliyekuwa Rais, Dakta Jakaya Mrisho Kikwete, kuagiza iwekwe wazi tuisome, wadadisi wa mambo tukatoa muhtasari wa 'Tuwaonao katika Ripoti ya CAG kuhusu Escrow'. Mjadala mkali uliozuka ulitufanya tuihoji iliyokuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kama CAG alilegeza kamba katika sakata la Escrow. Pamoja na hayo yote, niliendelea kuwa na imani na CAG.

Sasa umezuka tena mjadala mwingine mkali kuhusu ripoti ya uhakiki wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (NSSF) uliofanywa na CAG.  Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Chiristopher Ole Sendeka, ameuchochea mjadala huu pale alipotoa tuhuma kali dhidi ya Mwenyekiti wa zamani wa PAC, Zitto Zuberi Kabwe. Lakini chanzo cha mjadala huu kuibuka upya ni mkutano wa NSSF na PAC, ambayo sasa inaongozwa na Naghenjwa Kaboyoka wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Mkurugenzi (mpya) wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara amekiri kuna utata na unashughulikiwa. Naye Mwenyekiti (mpya) wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Profesa Samwel Wangwe, naye amenukuliwa na gazeti la Serikali, Daily News, akisema mradi huo ulikuwa na walakini. Watetezi wa safu ya zamani ya NSSF kwenye mitandao ya jamii, nao wanadai kwamba hivi ni vita dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa NSSF, Dakta Ramadhani Kitwana Dau ambaye hivi karibuni ameteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa Balozi wetu nchini Malaysia.

 Chama Cha ACT-Wazalendo nacho kimetoa tamko. Wadadisi wa mambo tumeshangaa ni kwa nini chama hicho makini tena chenye mshauri aliyebobea, Profesa Kitila Mkumbo, hakikumtumia Katibu Mwenezi wake mahiri, Ado Shaibu, kutoa tamko hilo. Badala yake tamko limetolewa na Habib Mchange ambaye Zitto Kabwe aliwahi kukiri "ndiye alikuwa CEO wa Leka Dutigite company." Kampuni hiyo ilifaidika kwa namna moja au nyingine na fedha kutoka katika mashirika ya Umma ya NSSF na la Hifadhi za Taifa (TANAPA).


Kwa wachambuzi wa masuala ya migogoro ya maslahi, kitendo cha huyo (aliyekuwa) Mkurugenzi wa Leka Dutigite kutoa matamshi yafuatayo kama Katibu wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa wa ACT-Wazalendo kunaibua maswali mengi kuliko majibu:

"Na mnafahamu tuhuma zote za kifisadi katika Taifa hili, kuanzia Escrow, kuanzia EPA, Kagoda, Meremeta - zote ziliibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Kwa hiyo, kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amekagua NSSF ambayo ilikuwa ni moja katika mashirika ya Umma ambayo yalisimamiwa na PAC. Ripoti yake hii hapa ambayo sisi tunayo... ya tarehe 24 Oktoba .... na taarifa ya Barua ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Mkuu wa Serikali - Management Letter - kwenda kwa Kamati ya Bunge na PAC... hii taarifa ya juzi .. haioneshi kwamba kuna tuhuma za NSSF kulipwa.... kununua hizo eka kwa milioni 800, maanake hii ndiyo taarifa ya NSSF,  hii, haisemi, hii ni taarifa ya CAG, hii, haisemi. Sasa unahangaika vipi na Zitto aliyekuwa Mwenyekiti wa PAC.... Lakini ninyi mnajua kwamba huwezi kuwa Mkurugenzi wa shirika kama NSSF Tanzania, shirika kama TANAPA, usiwe mwanachama wa CCM. Haiwezekani. Lazima uwe mwanachama wa CCM. Wanasema, hawasemi huwezi... Na mnajua Mwenyekiti wa CCM ni Magufuli.... sasa Mwenyekiti wa CCM kamteua aliyekuwa Mkurugenzi wa NSSF leo, kampa ubalozi.... Mwenyekiti wa CCM anayepambana na Ufisadi, mwenye Usalama wa Taifa, mwenye Polisi, mwenye jeshi, mwenye taarifa zote nyeti anashindwa kupambana na fisadi mmoja anayesemwa na Ole Sendeka anahusiana na Zitto .... mpaka anamtuma kuwa Balozi wa Malaysia? Hilo sisi hatumjibii.... Kwa mujibu wa barua ya CAG kama nilivyoeleza hapa, imeeleza hakuna shida...."
Tamko la kimaandishi 'lililowasilishwa' na Mchange linashangaza zaidi hasa ukizingatia haya maneno yake yanafanana na ya gazeti ambalo limekuwa likidaiwa kuandika taarifa nyingi za chama chao:

"ACT Wazalendo tunayo taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG. Kupitia taarifa husika CAG ametoa Hati safi Kwa Shirika la NSSF Kwa hesabu za mwaka 2014/15. Hajaona ufisadi wowote ule. Sijui msemaji wa CCM anatumia taarifa ipi ya CAG kusema kuwa NSSF ilinunua Ardhi Kwa bei ya Shilingi Milioni 800 aliyomhusisha nayo Kiongozi wetu. Kwa mujibu wa barua ya CAG Kwa Uongozi wa NSSF (Management letter), Shirika hilo halijanunua ardhi yoyote Kigamboni, bali Shirika limeingia ubia wa Ardhi Kwa Hisa (Land for Equity). Hivyo ni vizuri mbwatukaji huyo wa Chama tawala akaeleza kwa undani Ufisadi anaousema juu ya manunuzi ya ardhi kwa kunukuu ripoti ya CAG kaitoa ukurasa namba ngapi katika ripoti husika. Labda chama chake kina taarifa nyengine ya CAG tofauti na iliyowasilishwa kwenye Kamati ya PAC.  Rais Magufuli, ambaye ni Mwenyekiti wa chama tawala, amemteua aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kuwa Balozi. Kauli za Msemaji wa chama tawala alizozitoa jana zikiaminiwa zina maana kuwa Rais na Mwenyekiti wa chama chake anateua mafisadi kuwa mabalozi. Ni vizuri nyie wanahabari muulize juu ya hili jambo."
Ukaribu wa NSSF (wa enzi hizo) na baadhi ya vyombo vya Habari, wahariri na wanahabari siyo jambo jipya. Katika maadhimisho ya miaka 50 ya wadau wake mnamo mwaka 2014 huko Arusha, ripoti ya NSSF ilikuwa na haya ya kusema kuhusu mahusiano hayo:

"[Then] Chairman of Tanzania Editors Forum (TEF) Mr. Absolom Kibanda thanked, on behalf of other Forum members, the management of NSSF for coming closer to media professionals. Kibanda showered his heartfelt thanks to the [then] Funds Director General for his commitment to work closely and friendly with the media, saying such a scenario was a commitment by the Fund’s management to be closer to Tanzanians. The Kigamboni editors encounter is a continuation of annual such gatherings between editors and the NSSF management, aimed at brainstorming and updating the media of various developments achieved or being implemented by the Fund. Editors and NSSF encounter is as well, aimed at bringing together the media and the Fund so as to cement a good relationship, hence bringing closer media professionals in Tanzania to the Fund’s management and its stakeholders [(Aliyekuwa) Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bwana Absalom Kibanda aliishukuru, kwa niaba ya wanachama wa Jukwaa hilo, Menejimenti ya NSSF kwa kuwa karibu na wanataaluma wa habari. Kibanda alitoa shukrani hizo za dhati kutoka moyoni kwa (aliyekuwa) Mkurugenzi wa Shirika kwa kujitoa kwake kufanya kazi kwa ukaribu na urafiki na vyombo vya habari, na kusema kuwa hali hiyo ni ya kujitoa kwa Menejimenti ya Shirika kuwa karibu na Watanzania. Mkutano wa Kigamboni kati ya wahariri ni mwendelezo wa mikutano ya kila mwaka kati ya wahariri na Menejimenti ya NSSF yenye lengo la kubunga bongo na kupeana taarifa mpya kuhusu maendeleo mbalimbali yaliyofanikishwa au yanayotekelezwa na Shirika. Wahariri kukutana na NSSF pia kunalenga kuvileta karibu vyombo vya habari na Shirika ili kujenga mahusiano mazuri, hivyo, kuwaleta karibu wanahabari na Menejimenti ya Shirika na wadau wake ]"
Kama kuna mtu ambaye anapaswa kuzijua akaunti za NSSF kwa undani basi ni CAG. Kwa mujibu wa Taarifa za Mwaka za Hesabu za NSSF za mwaka 2010/2011, Profesa Assad alikuwa "Trustee" [Mdhamini]" wa NSSF ambaye alishiriki 'kupitisha' hesabu za shirika hilo baada ya kuhudhuria vikao vyote 12. Pia alikuwa mjumbe wa "The Finance and Investment Committee" [Kamati ya Fedha na Uwekezaji]" aliyehudhuria vikao vyote 4 bila kukosa. Taarifa kama hiyo ya mwaka 2005/2006 inaonesha uteuzi huo wa Profesa Assad ulianza lini na  Wasifu wake wa Kitaaluma (CV) una muhtasari huu kuhusu yaliyokuwa majukumu yake kwa NSSF:

Kwa uzoefu huo, ni vigumu kuamini kwamba CAG hakuona shida yoyote katika hesabu za NSSF labda kama alikuwa na 'mgongano wa maslahi' kutokana na majukumu ya awali. Nadiriki kusema hivi kwa sababu "MANAGEMENT LETTER ON THE AUDIT OF FINANCIAL STATEMENTS OF NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) FOR THE YEAR ENDED 30 JUNE 2015" [Barua ye Menejimenti kuhusu Ukaguzi wa Hesabu za Shirika la Hifadhi ya Taifa (NSSF) kwa Mwaka Unaoisha Tarehe 30 Juni 2015] ya tarehe 17 Desemba 2015 itokanayo na ushirikiano wa kikaguzi na Wakaguzi wa Ernest & Young ina maneno haya nitakayoyatafsiri:

 "The question here remains how a contract or agreement be signed and land ownership in a Public entity without agreed value of each piece of land? Also there was no verification and documents from Land Office provided that Azimio Housing Estate Limited owns 20,000 acres of land at Kigamboni for development. Therefore the signed agreement is not legal and void. Also the agreement was not vetted by the Attorney General (AG) which makes the matter more questionable...The audit scrutiny of such joint venture project revealed the following issues:...i. Overvalued price of Land to a tune of TZS 835,956,806 per Acre...ii. NSSF own land plot of 267 acres acquired for TZS 4,500,000...iii. The amount contributed by Azimio housing is questionable... iv. Financial capacity of Azimio Housing Estates Limited is questionable by having an issued and paid up share capital TZS 10,000,000...v. Lack of evidence for due diligence done with respect to Azimio Housing Limited and its affiliates...vi. NSSF awarded three tenders to owner of Azimio Housing Estates Limited who owns another Company called ZAK Solutions (Tanzania) Limited with tune of TZS 10,243,547,619.2... In addition, we were not availed with any documentation or title to substantiate that Azimio Housing Estates owns additional 19,700 acres of land.... [Swali linalobaki bila jibu ni jinsi mkataba au makubaliano yalivyosainiwa na umiliki wa ardhi na taasisi ya umma bila makubaliano kuhusu thamani ya kila kipande cha ardhi. Pia hakukuwa na uhakiki na taarifa katika Ofisi ya Ardhi inayotolewa kuonesha kuwa kampuni ya Azimio Housing Limited Estate inamiliki ekari 20,000 za ardhi Kigamboni kwa ajili ya kuendelezwa. Hivyo, mkataba uliosainiwa ni batili na haupo kisheria. Hali kadhalika mkataba huo haukupitiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) hivyo kulifanya suala hilo kuzidi kuwa tata. Ukaguzi wa mradi wa ubia umeibua masuala yafuatayo....i. Ardhi imethaminishwa kwa kiwango kikubwa mno cha TZS 835,956,806 kwa ekari...ii. NSSF inamiliki kitalu cha ardhi cha ekari 267 ambazo zilipatikana kwa TZS 4,500,000...iii. Kiwango ambacho Azimio Housing imekichangia kina utata...iv. Uwezo wa Kifedha wa Azimio Housing Estate Limited una utata ukizingatia imetoa na kulipa mtaji wa hisa wa TZS 10,000,000...v. Hakuna ushahidi unaoonesha kuwa Azimio Housing Limited na Washirika wake walifanyiwa uchunguzi ili kujiridhisha....vi. NSSF ilitoa zabuni tatu za TZS 10,243,547,619.2 kwa mmiliki wa Azimio Housing Limited ambaye pia anamiliki kampuni nyingine inayoitwa ZAK Solutions (Tanzania).... Zaidi ya hayo, hatukupewa taarifa au hati yoyote inayothibitisha kwamba Azimio Housing Estates inamiliki ekari 19,700 za ardhi za ziada]"
Wadadisi tunapata shida zaidi tunapoisoma 'RIPOTI YA MWAKA YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KUHUSU UKAGUZI WA HESABU ZA MASHIRIKA YA UMMA KWA MWAKA WA FEDHA WA 2014/2015' ya tarehe 28 Machi 2016. Pengine kwa sababu siyo ripoti ya ukaguzi wa NSSF peke yake, humo hatuoni maneno yote yaliyopo kwenye hiyo ripoti ya CAG na Ernst & Young. Labda kwa sababu majibu mengine yalishapatikana katika kipindi hicho kifupi cha miezi mitatu ndiyo maana tunaliona tena suala hili hili lililokosa jibu:

 "Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii limeingia ubia na Kampuni ya Azimio Housing Estates kuanzisha kampuni maalumu kwa jina la Hifadhi Builders Limited. Katika mkataba huo, Azimio Housing Estates itatakiwa kuendeleza ekari 20,000 za ardhi zilizopo Kigamboni ambapo kwa hatua ya awali itaanza na ekari 300. Katika ubia huu, Shirila la Hifadhi ya Jamii inamiliki asilimia 45 ya hisa wakati Azimio Housing Estates inamiliki asilimia 55 ya hisa. Jumla ya gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 653.44 na utaratibu wa uchangiaji mtaji ni kuwa shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii litatoa fedha zenye thamani ya asilimia 45 ya gharama za mradi na Azimio itatote fedha zenye thamani ya asilimia 35 ya gharama za mradi pamoja na ardhi ambayo itathaminishwa kuwa aslimia 20 ya gharama za mradi. Ukaguzi wa hatimiliki umeonesha kuwa Azimio Housing Estates inamiliki viwanja viwili, kiwanja chenye hatimiliki Na. 81828 kiwanja chenye ukubwa wa hekta 1.98 na chenye hatimiliki Na. 105091 chenye ukubwa wa hekta 114.11. Viwanja vyote vinapatikana eneo la Rasi Dege ambavyo kwa pamoja vilihamishiwa kwa Hifadhi Builders kutokwa kwa Azimio Housing Estates kwa ajili ya Awamu ya Kanza ya mradi. Kwa kutumia kizio cha ekari 2.47 kwa hekta, hatimiliki hizi zitakuwa na ukubwa wa jumla wa ekari 286.74, pungufu ya ekari 13.26 kutoka kwenye ekari 300 ambazo zilipangwa kwa ajili ya Awamu ya Kwanza ya mradi. Sijaweza kupatiwa hatimiliki za ardhi ambayo Azimio aliahidi kutoa kama uchangiaji wa mtaji. Hivyo imekuwa vigumu kwangu kuthibitisha uwepo wa viwanja hivyo. Kwa kukosekana kwa hatimiliki, umiliki wa ekari 19,700 za ardhi ambazo sehemu ya mtaji wa Azimio Housing Estates kwa asilimia 20, fedha za shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii zinakuwa kwenye hatari ya kupotea. Menejimenti inashauriwa kuwasiliana na Wizara ya Ardhi ili kuhakiki umiliki wa heka 19,700 za Azimio Housing Estates katika eneo la mradi. Pia, hatimiliki za ekari 13.26 zilizokuwa pungufu kwenye Awamu ya Kwanza ya mradi zinahitajika kuonekana."
Haya ndiyo masuala yanayohitaji ufafanuzi wa kina. Je, uhakiki wa wamiliki halisi wa AZIMIO na uwezo wao wa kiuwekezaji katika huo ubia wao na NSSF umeshafanyika? Na umiliki wao wa ardhi umethibitishwa? Kama yote haya bado hayajafanyika, wanufaikaji wa 'miradi' na 'nyumba' za NSSF wanapata wapi uwezo na utashi wa kudai kuwa eti CAG ameshahitimisha kwamba hakuna "shida" wala "ufisadi" katika mradi wa NSSF huko Rasi Dege, Kigamboni?

Isije ikawa ni aliyoyasema Profesa Assad: Ujasiriamali wa Kisiasa!

Sunday, October 30, 2016

A Tale of Two CAG Reports on NSSF?


"The question here remains how a contract or agreement be signed and land ownership in a Public entity without agreed value of each piece of land? Also there was no verification and documents from Land Office provided that Azimio Housing Estate Limited owns 20,000 acres of land at Kigamboni for development. Therefore the signed agreement is not legal and void. Also the agreement was not vetted by the Attorney General (AG) which makes the matter more questionable...The audit scrutiny of such joint venture project revealed the following issues:...i. Overvalued price of Land to a tune of TZS 835,956,806 per Acre...ii. NSSF own land plot of 267 acres acquired for TZS 4,500,000...iii. The amount contributed by Azimio housing is questionable... iv. Financial capacity of Azimio Housing Estates Limited is questionable by having an issued and paid up share capital TZS 10,000,000...v. Lack of evidence for due diligence done with respect to Azimio Housing Limited and its affiliates...vi. NSSF awarded three tenders to owner of Azimio Housing Estates Limited who owns another Company called ZAK Solutions (Tanzania) Limited with tune of TZS 10,243,547,619.2... In addition, we were not availed with any documentation or title to substantiate that Azimio Housing Estates owns additional 19,700 acres of land...." 


CF.

"NSSF entered into a Joint Venture with M/s Azimio Housing Estates to form a Special Purpose Vehicle Company, M/s Hifadhi Builders Limited. Under the contract, M/s Azimio Housing Estates would be responsible to develop 20,000 acres of land situated at Kigamboni of which the First Phase covers 300 acres. In this Joint Venture, NSSF holds 45 percent while M/s Azimio Housing Estates holds 55 percent shares. The total estimated cost of the project was USD 653.44 million and the terms of capital sharing is that, NSSF will fund 45 percent of total project cost and M/s Azimio Housing Estates will fund 35 percent cash plus the value of land which will be regarded as 20 percent. A review of title deeds submitted indicated that M/s Azimio Housing Estates owns two plots with title deeds number 81828 and 105091 for lands which are both located at Rasi Dege measuring 1.98 and 114.11 hectares respectively which were transferred to Hifadhi Builders by M/s Azimio Housing Estates for the First Phase of the project. Using a standard conversion rate of 2.47 acres per hectare, the two tittle deeds give a total of 286.74 acres which is 13.26 acres below the total land required for the First Phase of 300 acres. I have not been availed with title deeds for M/s Azimio Housing Estates contribution which made it difficult to substantiate existence of the plots. In the absence of title deeds, ownership of 19,700 acres being 20 percent contribution by M/s Azimio Housing Estates cannot be substantiated, therefore NSSF money might be subjected to risk of loss. Management is advised to communicate with the Ministry of Land to establish the legal ownership of 19,700 acres of land by M/s Azimio Housing Estates in the project area. Title deeds for the remaining 13.26 acres should be availed" -

Saturday, October 22, 2016

What Would Mwalimu Nyerere Do?

The King is Coming: What Would Mwalimu Nyerere Do?

Chambi Chachage


What would Mwalimu Nyerere do? Barely a fortnight after commemorating Nyerere Day, the government of Tanzania is about to host the King of Morocco. This is a glaring foreign policy shift from a country that is known for supporting liberation struggles.

Tanzania's solid stance against Morroco's colonial occupation of Western Sahara was inculcated in our consciousness as we grew up in the twilight of Mwalimu Nyerere's regime. I still remember how Willy Gamba, a character in a popular novel, Njama, that the late Aristablus Elvis Musiba published in 1981, moved us when he thus described another tough character known as Veronica Amadu:

 "Anajulikana kuwa msichana mwandishi jasiri sana, amewahi kusafiri na majeshi ya Chama cha wapigania uhuru wa Sahara Magharibi kiitwacho "The Popular Front for the Liberation of Saguiet el-Hamara na Rio de Oro" yaani "POLISARIO", katika mapambano yao dhidi ya majeshi ya Morocco ambayo yameshika sehemu hiyo, inasemekana mwandishi huyu alikaa na majeshi haya na kuandamana nayo katika uwanja wa mapambano kwa muda wa miezi sita na kuwa mwandishi wa kwanza kuandika habari kamili za mapambano haya akiwa shahidi wa macho. [She is known as a brave journalist, she has travelled with the army of POLISARIO freedom fighters in their battle against the army of Morocco that occupy their land, and it is said that she marched with them for six months, becoming the first journalist to write a firsthand account]."

Two years earlier, in 1979, Mwalimu Nyerere was among the then Organisation of African Unity's (OAU) "wise" leaders who met in Monrovia to seek an an end to the war. However, the then King of Morocco boycotted. Nevertheless, they "unanimously called for Morocco to call a cease-fire and withdraw from the disputed area." 

A confidential briefing in the US thus captured our clear stance: 

The briefing also observed that Tanzania viewed Morocco as the chief impediment to the resolution. It also noted that Mwalimu Nyerere was committed to persuade the King. Yet it concluded:Despite all these diplomatic efforts, Morocco quit the OAU in 1984 immediately after Mwalimu Nyerere was elected the chair of OAU. Mobutu's then Zaire supported it. According to Clifford D. May of the New York Times, Nyerere "made no comment". He must have been so disappointed because of the failure to resolve the question. 
It is thus ironic that now Mwalimu Nyerere is long gone, Tanzania is embracing Morocco and abandoning Western Sahara. Although they signed a cease-fire agreement in 1991, the question remains unresolved. One only needs to compare this conclusion to a speech the Tanzania's former Minister of Foreign Affairs, Bernard Membe, delivered to the Parliament in 2013 with our current dispensation:

Mheshimwa Spika, Tanzania haina uhasama na Morocco lakini inapinga kitendo cha Morocco kuendelea kuikalia Sahara Magharibi kimabavu. Tanzania inaendelea kuishauri Serikali ya Morocco kurejea kwenye Umoja wa Afrika ili suala hili lijadiliwe na wao wakiwa kama sehemu ya Umoja huu. Aidha, tunazidi kuisihi Morocco itekeleze pendekezo la kura ya maoni ili wananchi wa Sahara Magharibi waamue hatima yao wenyewe [Honorable Speaker, Tanzania has no dispute with Morocco but it is against Morocco's occupation of Western Sahara. Tanzania continues to advise the Government of Morocco to rejoin the Africa Union so this issue can be discussed while they are members. We also plead with Morocco to implement the recommendation regarding a referendum so that the people of Western Sahara can determine their own destiny]
Membe's successor, Dr. Augustine Mahiga, seems more interested in Tanzania pending investment agreements with Morocco of about two billion US dollars. After his UN speech on behalf of President Magufuli which called for the decolonization of Western Sahara, he is now preoccupied with how much we can get out of 150 or so Moroccan delegates. His press statement of October 20th is quoted in a government newspaper, Daily News, as saying: "We welcome them and we have no reason of not endorsing our support"
Little wonder the leader of the  ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, is convinced that Morocco is lobbying Tanzania as it attempts to ensure that SADR is kicked out of the African Union (AU) to pave the way for Morocco. His fledgling party has issued a statement, seeking some clarifications and asserting its would march against the King's visit. The embryonic Tanzania-Sahrawi Solidarity Committee (TASSC) is also using this moment for its advocacy.

Tuesday, October 18, 2016

Swahili Ally: Tanzania Misses Its Culture

 An Interview with Swahili Ally 


"A country which has no culture is not free," says Tanzanian musician Swahili Ally a.k.a Digo.


Swahili, you are based in Dar es Salaam, the Mecca of the Tanzanian music scene. Which problems do you have as a musician in Dar?

I face several problems and challenges. First of all, it's hard to get space to present my music. And the people still do not believe that traditional music is good music which needs to get attention. You need to cultivate your own culture. You know, a country which has no culture is not free.

You are saying Tanzania misses its culture?

Yes, Tanzania misses its culture! Songs of our culture and our culture as a whole are not been given space. The commercial music has taken over the whole country and we as traditional musicians, representing and cultivating our culture, have been left out.
What do you think where does that come from?

I think it has to do with commercial musicians who are seen as examples nowadays. I think the current society does not know about traditional musicians who were successful. I mean there are legendary ones like Tatu Nane who among the first ones to successfully present traditional music even far away. And they were being loved for that. Nowadays young musicians heavily copy western music and it seems like this is the music which gets attention and with which you can make more money. Local music is said to be music which is difficult to listen to. But if people would listen more to local traditional music they would get more used to it.

Can the government improve the situation of traditional music in Tanzania?

The government and the media need to bring back musical infrastructure so that people can rediscover their own society. People need to hear songs from former times. And the government needs to open up much more music academies. Then people will be able to know traditional music instruments and to create their own music. Without this it will be difficult, because the society has forgotten its origins. People have forgotten what is part of their own African identity. Now they need to get food which is not yet there, but which they need to know. 


You play the Kora, a typical West African instrument even though you come from Tanga, a city close to the Kenyan border. How did this come about?

You're right, the Kora comes from West Africa. But I met a European musician who played the Kora and that inspired me. I wanted to play the Kora and to mix it with my own music, because it matches perfectly with my own voice and my own style of music. Also originally the Digo people migrated from West Africa long time ago, so my family roots have kind of a West African origin.

Where did you learn to play the Kora? 

I was lucky to be taught to play the Kora by Ebrima Mbye from Gambia when he was staying on Zanzibar for six months. He worked as a volunteer at the Dhow Music Academy and I had the opportunity to stay there as well. He taught me how to play Kora in a typical Gambian way, which is the original one. It therefore dominates my own style of playing the Kora nowadays. 

Storytelling is an important element of the Digo culture as well as of the Kora culture. Do you see yourself more as a musician or as a storyteller?

I see myself as a musician who tells stories. In my music I talk about where we come from, where we are and where we are heading to. Through the way I am doing this I try to remind the society of its own people and ethnic groups and to show them that they still exist and that they are still able to influence things. 


Your grandparents introduced you to the world of Digo music and passed you on the knowledge about it. What role do your grandparents have and how do they influence you nowadays? 

My grandparents still influence my music even though they are no longer there. I still draw on the advices they gave me – they make me unique, they help me to be different. When I composed my melodies my grandfather gave me some assistance sometimes: he told me what to do and what to change. When I wrote my lyrics he told me when I did mistakes and corrected them. He is therefore a person who is an important part in my life. He pushed me and made me understand many things.

Thursday, October 13, 2016

Tuzo ya Andika na Soma


Public Talk and Book Signing with Andrew Coulson


Wednesday, October 12, 2016

Tanzania-Germany: A Shared Memory and Legacy?

"Will there be giving back or returning the cultural objects loot which is stashed in almost all ethnological museums in Germany? I met a German lady working at the national museum in Berlin and she told me that some few years ago the best German lawyers were convened to make sure that they improve the rules, regulations and laws which protect German’s interests in keeping all what was collected during colonialism. It may be considered a mere coffee table talk she was making with me, but is there a political will from the German side to realize the objectives of this project? So far these objects in German museums serve as commercial products through which museums make profits from visitors charges, how are the profits generated in such activities shared to Tanzanians? Is there hope that there will be a day when Tanzania will see some 4000 cultural/archaeological objects are given back to enrich its collection of its pre-colonial generations? Is there any logical explanation from German to justify the need to keep the loot from the small communities they extinguished in Tanzania? Why not give back everything they have taken from these small people after all the suffering which has been caused?" - Dominicus Makukula
Cf.

Sunday, October 9, 2016

Taharuki ya Walimu: Mitandao ya Jamii Ipongezwe?

Jamhuri ya Mitandao ya Kijamii na Sakata la Walimu Mbeya

Richard Mbunda


Hali imekuwa tofauti sana na kipindi sisi tunakua kule Utiri, Mbinga ambapo taarifa yoyote utaipata kwa kusimuliwa. Kuona picha ilikuwa nadra, na sijui ni lini nilianza kuongea kwa simu tena zile za mkonge! Sasa mambo yamebadilika sana. Unapata taarifa kutoka sehemu yoyote ya dunia kiganjani kwako na unaweza kusambaza taarifa kwa kasi ya mwanga, ili mradi tu umetandaa. Haya si ndiyo maendeleo ndugu zangu?

Miaka kadhaa iliyopita mwandishi wa habari alinipigia simu kuuliza maoni yangu wakati muswada wa sheria ya mitandao ya kijamii ulipokuwa unaandaliwa. Kwa maoni yake yeye [naamini pia ni maoni ya nchi za magharibi], sheria hii ingekandamiza maoni ya wananchi. Mimi nikamjibu, kwa kasi hii ya kutandaa kwenye mitandao ya kijamii, naamini tungehitaji taratibu za kutuongoza. Nilimwambia; ‘pale ambapo uonevu utakuwepo tutapaza sauti kwenye mitandao ya kijamii’. Ndugu msomaji, nataka utambue kuwa upekee wa mitandao ya kijamii ni uwezo wake wa kujitetea. Na huwezi kuuondoa upekee huu.

Ingawa sheria hii imeshawatia hatiani watu kadhaa kwa uchochezi na wengine bado wanahitajika mahakamani [huenda sisi wote ni watuhumiwa watarajiwa], lakini mitandao ya kijamii haijaacha kuiteka nchi. Naam, ingawa siyo nchini kwetu tu, ni dhahiri sasa Tanzania tumekuwa Jamhuri ya Mitandao ya Kijamii.

Ukiachana na hizo mbwembwe za hapo juu, dhumuni la andiko hili ni kutoa maoni yangu kuhusu sakata la walimu kumpiga mwanafunzi Mbeya. Naam, nimesononeshwa na mambo mengi katika sakata hili kwa mantiki ya uzito wa jambo lenyewe, uwajibikaji, uongozi na taathira ya muda mrefu ya maamuzi yaliyochukuliwa na taasisi mbalimbali za kiserikali.

Uzito wa Makosa kama yanavyoonekana kwaye Video

Hakuna maswali, na mimi nataka kusisitiza, wakati video hii ikisambaa, sikuwahi kumuona mtu yeyote akikubaliana na kilichoonekana kwenye video. Walimu walikuwa wanapiga kwa kukomesha kama majambazi na sio kufundisha kama kanuni zao za kazi zinavyowataka. Mimi nataka nimpongeze mchukuaji wa video kwa jinsi alivyo mahiri kwani amefanikiwa kutuonesha sehemu muhimu zaidi ambayo ndiyo msingi wa mihemko yetu na maamuzi yaliyochukuliwa. Kitendo cha walimu hawa hakiwezi kufumbiwa macho na kwa namna yoyote lazima vyombo vya dola vichukue hatua stahiki. 

Maamuzi ya Viongozi wa Serikali

Mara baada ya video kusambaa, na kwa bahati nzuri viongozi wetu ni sehemu ya mitandao hii, hatua mbalimbali zilichukuliwa. Napenda kupongeza hatua iliyochukuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba. Kwanza kabisa aliutaarifu umma kuhusu tukio: wapi limetokea, nani wanahusika tathmini ya awali za chanzo cha tukio. Pili, alilaani kitendo hiki ili kuonesha kutokukubaliana nacho. Tatu, aliliagiza Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka kuwatafuta watuhumiwa hawa na kuwafikisha katika vyombo vya sheria. Nampongeza pia kwa kuwa alitumia mitandao ya kijamii ili kufikisha taarifa hizi haraka iwezekanavyo. Katika nchi inayofuata msingi ya sheria, hatua hii ya Waziri wa Mambo ya Ndani ndiyo haswa iliyotakiwa kuchukuliwa, na Mheshimiwa huyu alitumia madaraka yake vizuri sana.

Lakini, baada ya hatua hizi zilizochukuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, palifuata hatua zingine lukuki ambazo zimenichanganya sana, na huenda ndizo zilizonifanya nichukue kalamu. Kila Mtanzania alilaani vitendo hivi kwa nafasi yake, na hata kwenye mitandao ya kijamii kuna waliohukumu na hata kutekeleza hukumu zao mara tu baada ya kuona video. Hata hivyo, katika Habari za Mikoani TBC, iliripotiwa kuwa WAZIRI wa ELIMU na MAFUNZO ya UFUNDI alitamka kuwafukuza chuo walimu (wanafunzi wa chuo) waliohusika na tukio la kumpiga mwanafunzi kama ilivyoonekana kwenye video. Hii ilinishangaza sana. Waziri kaona video tu amehemka na kufukuza watu chuo hata bila taratibu zingine kufuatwa! 

Ingawa wanastahili kuwa jela, na kufukuzwa lakini tunazungumzia walimu watatu, ambao tayari Serikali imeshawekeza pesa na ni nguvukazi ya taifa, hivyo basi, lazima Waziri huyu awe amejiridhisha siyo tu kuchukua maamuzi ya papo kwa hapo. Hoja yangu ni kuwa utaratibu wa kisheria haukufuatwa na hao Walimu-Wanafunzi walikuwa bado ni watuhumiwa tu. Kama vile wanavyotoa vifungu vya kisheria kuhalalisha mamlaka zao za uteuzi, Waziri pia alipaswa kutuambia anatumia vifungu vipi vya kisheria vinavyompa mamlaka hiyo ya kufukuza wanafunzi chuo ili umma utambue kazingatia taratibu na sheria za nchi. Vinginevyo hatua hii aliyochukua haina tofauti na mama mmoja kwenye Basi la Mwendokasi aliyetaka wanafunzi hawa wafungwe moja kwa moja bila mahakama kuwasikiliza kwa kuwa alipoona video tumbo la uzazi lilimcheza.

WAZIRI WA NCHI- TAMISEMI aliandika barua akaisaini na ikatufikia kwenye mitandao ya kijamii. Waziri huyu anaandika barua yake kuwa amemtuma Mkuu wa Mkoa kufuatilia na mahojiano yanendelea. Lakini cha kushangaza anamhukumu Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kuwa hakutoa taarifa ya tukio, na bila hata kumsikiliza au kupokea/kudai maelezo yake anaagiza avuliwe madaraka yake ya ualimu mkuu! Hii imenishangaza sana. Mwalimu huyu alipaswa kusikilizwa na Waziri huyu ajiridhishe bila wasiwasi kuwa mwalimu alificha tukio hili ndipo hatua kama hii ingechukuliwa. Je, kama tukio hili halikufika ofisini kwa Mwalimu Mkuu ma liliishia 'staff room' tu? Halafu, huwezi kuagiza uchunguzi wakati huo huo unatoa hukumu, nadhani hukumu hii ilizingatia mihemuko ya jamii kwenye mitandao na siyo uongozi bora unaohitaji uvumilivu na utulivu kabla ya kuamua.
Mwisho katika mlolongo huu wa viongozi na Taasisi ni Bodi ya Mikopo. Ikiwa imevutwa katika mhemko wa tukio hili, Bodi hiyo iliandika barua tarehe 7/10/2016, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji, Abdul-Razaq Badru ,kuutarifu umma kuwa Bodi imesitisha mikopo kwa wanafunzi wanne waliohusika katika sakata hili, kitu ambacho sioni msingi wake. Je, bodi ya mikopo ilitaka kujitangazia tu mamlaka yake kupitia mgogoro huu wa video? Cha kushangaza zaidi ni pale wanapowataka wanafunzi hawa kurejesha mikopo waliyokopa mara moja, kana kwamba walikuwa wana uwezo wa kujilipa na wana pesa ila Bodi ilikuwa inawapa motisha tu ili wasome! Bodi ya Mikopo ilikuwa na uhalali gani wa kutoa tamko hili? Au ndiyo maana imeweza kuagiza makato ya wafanyakazi wa umma hasa katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) katika mishahara yao na kuwaongezea madeni hata kama walishamaliza tangu 2012! 

Kupost Video zinazoleta Taharuki

Pamoja na pongezi alizomiminiwa mtu aliyechukua tukio hili na kuposti video yake, lakini binafsi naona limeleta taharuki. Mchukua video hii, anayesadikiwa kuwa ni Mwalimu pia [na Mh. Mwigulu Nchemba amemtaja mpaka jina], alisononeshwa na tukio hili ndipo akaamua kulirekodi. Mwalimu huyu alipaswa kwanza kuipeleka video hii polisi ili sheria ichukue mkondo wake na labda hilo likishindikana ndiyo atumie mbinu hiyo ya 'ulipuaji' mitandaoni.

Madhara ya video hii yamekuwa makubwa. Kuna mama mmoja anasikikika akiongea na mtoto wake kuhusu video hii ambayo ilimtia hasira sana mtoto huyo wa takribani miaka sita au saba hivi. Mama huyu alirekodi mazungumzo hayo kwenye video ikionesha akilia kwa hasira na kutishia kwenda kuwaua walimu. Je, tunatengeneza kizazi cha aina gani na kiwe na uhusiano gani na walimu?
Pia naamini, pamoja na kuwa walimu hawakupendezwa na tukio hili la walimu-wanafunzi kumpiga mwanfunzi pasipo utaratibu, lakini huenda wametatanishwa na hatua zilizochukuliwa na kejeli walizozipata kutoka kwa jamii mara tu baada ya video hiyo kuwekwa hadharani. Nimeona video nyingine walimu wakiwarekodi wanafunzi waliowakuta na pombe kwenye viroba na bangi ili tu kuonyesha aina ya wanafunzi wanaodili nao kila siku wakiwa kazini. Posti hii pia haikubaliki kabisa, kwa kuwa video hizi zitaendelea kubaki mitandaoni kwa muda mrefu sana. Najaribu tu kuwaza kama walimu wa zamani wangekuwa wanaturekodi na kuposti video kwa umma sijui ni viongozi wangapi tulionao leo hii wangeathirika na jambo hilo! Huenda wengine wao wasingepata hata uthubutu wa kugombea nafasi walizonazo sasa.

Vilevile naona video hii imehamasiha uhasama kati ya walimu na wanafunzi. Najaribu kufikiri, idadi kubwa ya wanafunzi wapo shule za serikali na walimu wao wamekuwa walalamikaji wakubwa wa mazingira magumu ya kazi na hata mafao yao kutokuridhisha. Tukiwaongezea mzigo wa wanafunzi wakorofi kwa kuwa wakiadhibiwa watarekodi na kuwafukuzisha kazi walimu tunaweza kutengeneza kada ya walimu ambao watasusia kazi muhimu ya kuandaa nguvukazi hii ya baadaye. Wapo watoto wa siku hizi wanaovuta bangi, unga, walevi na wavivu. Hatupaswi kuwakatisha tamaa walimu wetu hata kidogo.

Mwisho, video hii ningependa iwe mwanzo wa mfumo mpya. Natamani video zinazoleta taharuki kama hizi zisiwekwe mitandaoni (kwanza) ila kupelekwa katika vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake. Pale hili linaposhindikana ndipo tuziweke mitandaoni ili kushinikiza vyombo vya dola vichukue hatua. Nataka utaratibu wa kutoa adhabu kwa wanafunzi ambao upo, uhimizwe ili kuhakikisha kuwa unafuatwa na pale ambapo mwalimu anakuwa amekosea hatua stahiki zichukuliwe. Video hii pia itufundishe kuwa watulivu na kujizuia kuchukua maamuzi ya haraka huku tukiziacha taaratibu husika kufuata mkondo. Tukichukua hatua kwa mihemko hatutakuwa na tofauti na wale wanaoua vibaka kwa kuwachoma moto au wale wanakijiji waliowachoma watafiti kwa kuwa tu walidhani ni wanyonya damu waliotishia maisha yao. Haya ni maoni yangu yenye nia ya kuleta utengamano wa kijamii. Maoni yangu siyo sheria na ninawajibika kuyatetea.

Friday, October 7, 2016

Afrika katika Tafsiri-Africa in Translation:21/10/16


Tuesday, October 4, 2016

Lest We Forget: A Tale of Two Land Policy Reforms

1999 Land struggles. As NGOs discuss the new draft land policy,they should pay heed & learn from the past.

Cf.

Azimio La Uhai: Declaration of NGOs and Interested Persons on Land


Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP