Wednesday, November 30, 2016

Makonda Anza Upya - Omba Msamaha

MAKONDA AANZE UPYA, AOMBE RADHI

Muhidin J. Shangwe

Tangu Paul Makonda akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni nilikuwa na wazo la kuandika makala yenye kichwa, “MAKONDA ANAPENDA SIFA AU TUNAOGOPA KUMSIFU?” Ilikuwa ni baada ya mwanasiasa huyu kijana machachari “kuteka” vichwa vya habari kwa matamko na hatua mbali mbali za kiuongozi alizochukua kwa nafasi yake hiyo. Kwa sababu wakati haurudi nyuma, na kwa uzembe wangu wa kutoandika makala hayo wakati ule, nitaeleza kwa kifupi sana nilichotaka kuandika juu ya ndugu Makonda. 

Nikiri kwamba nimejikuta nikimtetea Makonda mara kadhaa katika vijiwe na majukwaa ya mitandao ya kijamii. Mara nyingi nimekuwa nikitofautiana na wakosoaji wake wanaodai mwanasiasa huyu anapenda sifa kupindukia! Huwa najiuliza, ni kweli ama ni sisi tunaoogopa kumsifu? Binadamu, kihulka, sote tunapenda kusifiwa. Sifa tu pekee ni ishara ya mafanikio kwa upande wa anayesifiwa. Na penye mafanikio hapakosi wivu - hulka nyingine ya kibinadamu ambayo aghalabu hatupendi kuhusishwa nayo lakini hilo haliondoi ukweli wa kuwa nayo. Wakati mwingine mtu akimwagiwa sifa “tunaogopa” kwamba sifa hizo zisije kumfanya akafanikiwa! Kama ni hivi basi tunakuwa na wivu. Hakuna namna nyingine ya kulielezea jambo hili. Lakini wakati mwingine tunasita kumsifu mtu kama tahadhari kwamba kufanya hivyo kutamfanya alewe sifa. Mlevi wa sifa huharibu. Amelewa. Kazi ya kufikiri kwenye ubongo wake inaathiriwa na kilevi hicho. Msemo wa Kiswahili unafafanua kwa ufasaha: 'Mgema akisifiwa tembo hulitia maji!' Mimi si mwanasaikolojia, nakosa maneno mwafaka ya kuelezea jambo hili kwa kirefu. 
Hulka yetu ya kupenda sifa huonekana tangu tukiwa wadogo. Mtoto mdogo ukimsifu hata kwa sifa ambazo hana hucheka na kufurahi. Kwa watu wazima inatia faraja kibinadamu kama utafanya jambo unaloamini ni la heri na kisha watu wakakusifu. Faraja hii wengine huionesha wazi wazi, wengine hubaki nayo moyoni. Matatizo huanza pale matendo na tabia ya mtu vinapoongozwa na lengo la kupata sifa katika kufanya jambo fulani badala ya kufanya jambo kwa sababu ni vizuri kufanya jambo hilo. Hapa kuna shida. Sifa inatakiwa iwe ni matokeo, isiwe ndiyo dhamira ya kufanya jambo. Lakini nadhani suala si kupenda sifa bali tunasifiwa kwa lipi? Kama jambo ni zuri kwa nini mtu asisifiwe? 

Nakumbuka ndugu Makonda alipokuja na wazo lake la walimu wa wilaya yake ya Kinondoni kutumia usafiri wad daladala bure. Wakosoaji wake walinga’aka, walimdhihaki, wakadhihaki wazo lenyewe na kuhitimisha kwamba anakurupuka kwa sababu anapenda sifa. Wapo waliomtaka ashughulike na madai ya stahiki za walimu za miaka nenda rudi badala ya kukomalia “jambo dogo” la usafiri wa walimu wa wilaya yake. 

Mimi nililichukulia wazo lile tofauti kabisa. Nililiona kama wazo zuri la kiongozi kijana mwenye uthubutu. Kiongozi huyu hakuwa Waziri wa Elimu, alikuwa Mkuu wa Wilaya tu. Wazo lake lingeweza kuazimwa na kuboreshwa ngazi ya mkoa na hata kitaifa juu ya namna ya kuwaondolea kero ya usafiri walimu wetu. Lakini la, alinangwa kwa kupenda kwake sifa. Majuzi nilifarijika sana nilipoelezwa na watu kadhaa kwamba kumbe wazo lile linafanya kazi. Kwamba baadhi ya walimu wetu wanatumia usafiri wa daladala bure kabisa, mradi wawe na kitambulisho maalumu. Awali nilihofu kwamba walimu wetu wasingechangamkia utaratibu ule hasa kutokana na kejeli zilizosindikiza wazo lenyewe, zikichagizwa na wapinzani wa kisiasa wa Makonda. 

Hayo yalikuwa ya wakati ule ambayo kwa uzembe tu sikuyaandika. Tuyaache. 
Hivi karibuni ndugu Makonda amerudi tena “kwa fujo” kwenye vichwa vya habari. Lakini sasa si Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni tena, ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kabla ya matukio ya karibuni, yapo ambayo ameyatolea kauli ambazo zilizua gumzo. Moja ya kauli hizi ni pale alipowakataza wananchi wa mkoa wake wasiwafuate (follow) mashoga kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram na Twitter kauli ambayo kimsingi haitekelezeki! Pia amesikika akiashiria hadharani kwamba Kamishna wa Polisi Kamanda Sirro amehongwa na wafanyabiashara wa shisha, kauli ambayo ilijibiwa na Waziri Mkuu kwa kumkumbusha kwamba hilo liko chini ya mamlaka yake na alishughulikie (badala ya kulalamika!) Nimesikia pia kwamba ametoa kauli tata za kudai kwamba ofisi yake imejaa wafanyakazi mizigo ambao hawana sababu ya kuwa hapo, na akapendekeza wapunguzwe. Unaweza kudhani yeye ndiye Waziri anayehusika na Utumishi!

Lakini sasa Mkuu wa Mkoa huyu anatajwa kwa mengine. Kwa muda wa siku kumi amekuwa akifanya mikutano na wananchi wa Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuzifahamu kero za wananchi wake na kuzitafutia ufumbuzi. Kwa mara nyingine kiongozi huyu kijana anathubutu. Anataka kuwa mtu wa vitendo. Anataka kuongea na wananchi ana kwa ana, anataka kuwasikiliza na kusaidia kupata ufumbuzi wa kero zao. Jambo zuri kabisa hili la kupigiwa mfano wakati huu ambapo uwajibikaji wa viongozi wetu umekuwa kitu cha kutamaniwa! 
Kwa sababu za kimazingira na ratiba, sijaweza kusikiliza na kufuatilia mikutano yote kasoro mmoja tu. Hata hivyo nimekuwa nikipata taarifa za yanayojiri mikutanoni, shukrani kwa teknolojia ya mawasiliano. Ni hapa nilipogundua kasoro kadhaa za mtindo anaotumia Makonda. Nimesema kwamba siku zote nimemchukulia Makonda kama kiongozi machachari. Umachachari uko wa aina nyingi lakini ninaomaanisha hapa ni ule wa kujiamini (wakati mwingine kupita kiasi), kuthubutu, kutokuwa muoga, na “ubishi” wa kukomalia jambo analoamini (hata kama anakera watu wengine). Wakati Makonda alipojitokeza hadharani na kuutangazia umma wa Watanzania kwamba aliyekuwa kada mwenye ushawishi ndani ya chama chake cha CCM, ndugu Edward Lowassa, ni fisadi, na kwamba anahonga viongozi wa dini makanisani na misikitini ili aukwae urais, wengi walichukulia kitendo hicho kama ishara ya ujasiri. Huyu alikuwa kijana na kiongozi mdogo ndani ya CCM, anajiweka mstari wa mbele kumnanga kada mkongwe wa chama chake, mtu ambaye alikuwa na uwezekano mkubwa si tu wa kuwa mwenyekiti wa chama bali rais wa nchi! Ujasiri ulioje! 

Lakini kupitia mikutano yake ya siku za karibuni umachachari wa Makonda umeonekana katika sura mpya ya hasira, ukali usiohitajika na mihemko. Kwa kutumia lugha ya mashabiki wa mpira wa miguu, ameonekana ni mtu wa “kucheza na kelele za jukwaani!” Mchezaji mwenye kusikiliza kelele za mashabiki jukwaani ni hatari kwa timu yake, akiambiwa butua anabutua, akiambiwa kata mtama anakata! Anaweza kusababisha “penati” au hata kujifunga kwa 'kata funua'. Hasikii tena maelekezo ya kocha, ingawa kwa hili la Makonda inaweza kusemwa kocha wake “amempa rungu” la kubutua na kukata watu mitama!
Nimeona picha za video akiwauliza watumishi wa wilaya kwa nini hawahamishwi, kana kwamba suala hilo lipo kwenye mamlaka yao! Mtumishi anajuaje kwa nini hahamishwi? Ni jukumu lake kuhama?

Nimeona akimnanga mtumishi aliyemuomba arejee swali lake baada ya kutoeleweka. Badala ya kurejea swali yeye aliamua kumshushua na kuhoji anafanya nini mkutanoni kama hasikilizi yanayojiri. Nilijiuliza mheshimiwa huyu anakosa uvumilivu kiasi gani hata ashindwe kurejea swali lake alilouliza? 
Nimeona pia Makonda akitafuta suluhisho la kero za wananchi kwa namna ya chemsha bongo. Ni mtindo kwa “kipusa”- kwa wale wanokumbuka kipindi cha Misanya Bingi wakati ule akiwa Radio One Stereo. Kero inaelezwa, mtendaji anatakiwa kutoa majibu papo kwa hapo. Wakati mwingine mwanya unatolewa kwa watendaji kupata majibu na kushughulikia kero fulani, wakati mwingine mwanya huo hautolewi. Mtendaji anatakiwa awe na majibu yote papo kwa hapo. Akikosa jibu na kuomba apewe muda anakaripiwa, anatishwa. 

Lakini yote tisa, kumi ni pale nilipomsikia Makonda akimtukana afisa wa serikali hadharani kwa kumuita kichaa! Hakuishia hapo, alitishia kuwaweka rumande maafisa wa ardhi wilaya ya Kinondoni huku akionya kwamba hilo likitokea hapatakuwa na mtetezi wao. Kama vile haitoshi akaongeza kwamba aliposimama yeye ndipo Mungu aliposimama! Ni hili lililonifanya kuandika makala haya. 
Wapo wanaodhani kwamba “jeuri” hii ya Makonda imetokana na “kuvimba kichwa” baada ya kusifiwa na rais kwa njia ya simu akiwa katika moja ya mikutano yake. Sina hakika na hoja hii kwa sababu huko nyuma Mkuu wa Mkoa huyu amewahi kutoa kauli zinazoshabihiana na hizi za karibuni. Lakini lazima isemwe kwamba hili la kupigiwa simu na kupongezwa hadharani kwa kazi anayoifanya halijasaidia kumrekebisha Makonda kwa kumfanya awe kiongozi mwenye staha, hekima na busara mbele za watu. 

Toni ya lugha yake wakati akimhoji afisa yule ilikuwa ya mtu mwenye hasira, mtu anayemaanisha anachozungumza, mtu asiyeogopa taratibu za kisheria zinazowalinda watumishi wa serikali, mtu mbabe. Ni toni inayoogopesha, licha ya kwamba mtumishi yule aliyejitambulisha kwa jina la Rehema Mwinuka alijitahidi kuhimili na kutoa maelezo ambayo hata hivyo Mkuu wa Mkoa wake hakuwa tayari kusikiliza! “Hawa ndiyo vichaa tunaohangaika nao, toka hapa!” alifoka ndugu Makonda huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo. 
Hili la kushangiliwa nalo linahitaji maelezo. Moja kati ya kero kubwa za wananchi ni watumishi wa umma. Ndiyo, baadhi ya watumishi hawa ni kero. Wako wanaojihusisha na rushwa, wako wazembe na wavivu, wako wenye dharau, wako wasiosimamia maadili ya kazi zao, na wako wanaojiona na miungu-watu. Hawaambiliki, hawana unyenyekevu na, mbaya zaidi, hawana ufahamu mpana wa majukumu yao. Siku chache zilizopita nilisoma mahali kuhusu muuguzi mmoja aliyemuambia mgonjwa eti “ataisoma namba” kwa kuichagua CCM. Muuguzi wa aina hii ni fedheha kwa fani ya uuguzi na ni kero kwa wananchi. 

Kwa sababu hizi, wananchi wamejenga hasira dhidi ya watumishi wa umma kiasi kwamba inapotokea mmoja anadhalilishwa hadharani wao hushangilia. Ni wazi Makonda analijua hili, na pengine anatumia mwanya huo kuhalalisha kauli na matendo yake. Hili haliwezi kuwa jambo jema hata kidogo. Si tu kwamba linaleta chuki baina ya wananchi na watumishi, lakini linakatisha tamaa wale watumishi wachapakazi na waadilifu wanaodamka kila asubuhi kwenda makazini kuhudumu wananchi. Ni hapa busara ya kiuongozi inapohitajika kuepusha hili kutokea, busara ambayo kwa kauli za Makonda ni wazi imekosekana. Hapahitajiki ushahidi mwingine kuthibitisha hili. 
Mfululizo wa kauli na mwenendo wa Makonda umetuweka katika wakati mgumu wale tuliokuwa tukimtetea kwamba eti hana lolote zaidi ya kupenda sifa! Lakini pia umeitia doa kubwa ziara yake ambayo kama nilivyoeleza awali ni jambo zuri sana katika kuongeza ufanisi, uwajibikaji na mawasiliano kati ya watendaji wa serikali na wananchi. Katika mkutano ambao niliusikiliza redioni, kwa kiasi kikubwa ulifanyika kwa utulivu, wananchi na watendaji wakiwasiliana vizuri na kwa uungwana. Lakini mazuri haya yote sasa yanagubikwa na dosari zilizojitokeza, dosari ambazo zingeweza kuepukika kama busara, staha na uungwana vingetiliwa maanani.

Bado naamini Makonda ana nafasi ya kutuondolea fedheha hii sisi ambao tuliamini ana mengi ya kunufaisha zaidi ya kile kinachoitwa kupenda sifa. Lakini kufanikiwa hilo atahitaji kujirekebisha na hakuna namna ya kipekee kabisa kuanza safari hiyo zaidi ya kuomba radhi wale wote ambao walikuwa wahanga wa kauli zake za ukali, ubabe, na umungu-mtu wake wakati wa hii ziara yake ya siku kumi katika jiji la Dar es Salaam. Na zaidi ni kwa mtumishi huyu aliyeitwa kichaa! Makonda aanzie hapo, atakuwa amepiga hatua kubwa kwenye safari ndefu ya kuelekea kwenye uungwana, hekima na busara za kiuongozi. 
Sitaki kuamini baada ya joto la kuhemka kushuka Makonda anaweza kulala usingizi mzuri wa amani akikumbuka tukio lile. Na wala sitaki kuamini rais aliyempigia simu na kumpongeza kwa kazi nzuri amefurahishwa na tabia ya Makonda kwenye hili. Mtumishi yule ana familia, pengine ana mume, watoto, na wazazi ambao wamemsomesha kwa tabu kufika hapo alipofika. Kumuita kichaa mbele ya kadamnasi ni kumsababishia majeraha yeye, familia yake, watumishi wenzake na waungwana wote. 
Hata kama yapo makosa tunataka ithibitike bila chembe chembe za shaka kwamba alikuwa na kosa. Na kama kosa lipo, kuna lugha inayokubalika ya namna ya kumueleza, kuna taratibu za kiutumishi pia za kumuadhibu. Kwa kumuita kichaa, kwa kutishia kuwashughulikia watumishi wa umma hadi wajute kuzaliwa, kwa kujipa umungu kwamba uliposimama ndipo Mungu alipo ni makosa. Kama watumishi wale wamekosea (na tutajuaje kama wana makosa wakati hawasikilizwi?), Mkuu wa Mkoa naye amekosea. Makosa mawili hayaleti usahihi. 

Makonda aanze upya. Aombe radhi. Haya yako ndani ya uwezo wake. Hatua zaidi za kisheria na kiutawala dhidi yake zipo nje ya uwezo wake.

Saturday, November 26, 2016

Castro Came to Tanzania: Karibu na Kwaheri Fidel

A Tribute by Richard Mabala:

Oh my, 
My heart is shaken
Trembling beneath the crash of another mighty tree
It stood firm for so long
Withstanding tempests no other could stand
Unmoved
Unbowed
Protecting, sheltering,
Nurturing so many
As its branches spread out far and wide
Withering only in the face of age
Gnarled in body 
But still inwardly strong
Only age could conquer him
And now it has
Another hero gone
Another inspiration
Taken from us
Like Nyerere
Cabral
Fanon
Samora
Malcolm
Che
And so many others
Hamba Kahle camarada
Buen viaje
Safiri salama
We are poorer 
Diminished without your presence
But still we rejoice in your life
Enriched by your work
Strengthened by your example
Not victory or death
But victory despite death
A luta continua

Statement of Cuba/Tanzania Friendship Society on Commandante Fidel's Death:

The Tanzania/Cuba Friendship Society wishes to convey our heartfelt condolences to the people and government of Cuba following the death of the beloved historic leader of the Cuban Revolution Commandante Fidel Castro Ruz. We have been aware of and followed with great concern comrade Fidel's  failing health for a long while since 2006 when he underwent a major surgery. Although he was not in direct control of Party and State affairs,his physical presence in the background Cuban scene was like a bright star shining and providing light and guidance to the political,socio-economic trajectory of the heroic Cuban society.    

Now that he has passed away that star has inevitably dimmed but not faded away completely.For he has bequeathed to history and generations an enduring  lasting legacy in the form of his exemplary intellectual capacity,dedicated selfless leadership and inspiring revolutionary credentials.He leaves behind a potent lesson and a message to all struggling humanity against indignity,exploitation and social oppression to firmly adhere to steadfastness,resistance and unwavering commitment to principles.His nemesis western and US imperialism in particular as expected has greeted his death with euphoria and a sense of infantile celebration.We know they will as usual continue to use their mainstream media to lie,distort,cover-up the pernicious effects of US economic blockade on Cuba and other anti-Cuba wrong-doings (including the 600 criminal assassination plots targeting Fidel) as well as slander his personality while denying his achievement in ensuring the sustainability and survival of the Cuban revolutionary project despite the unrelenting hostility of the US empire.   

The Tanzanian/Cuban Friendship Society solemnly calls on the Cuban people to hold high Fidel's banner and spirit of eternal combat against injustices spawned by the born-again neo-liberal predatory capitalism as we join hands to mourn the physical demise of the indefatigable son of Cuba comrade Fidel Castro. Patria O Muerte, VENCEREMOS!

SALIM MSOMA  

CHAIRMAN, TANZANIA/CUBA FRIENDSHIP SOCIETY.

Cf.

Magufuli and the Politics of Information Sharing

Magufuli and the Politics of Information Sharing 

Chambi Chachage

On November 20, 2016 the President of Tanzania, Dr. John Magufuli, sacked the chair of the Tanzania Revenue Authority (TRA) Board, Bernard Mchomvu. According to The Citizen, the "sacking  was announced through a State House statement, which, however, did not specify the reasons for his removal." The 'rumor mills' in a city that was once dubbed 'Rumorvsille' took over.
Five days later, Daily News reported that the President revealed that Tsh 26 Billion were "allocated for TRA’s expenditure but the board approved a decision to deposit the funds in fixed accounts in three different commercial banks." So, he directed that the money should be returned, fired the chair and dissolved the Board. Informative.

"When the President gives out reasons on matters like these on [the] dissolution of TRA board openly", affirms a comment on the Daily News report, "it therefore puts to rest any speculations and unnecessary rumours!" And that, it concludes, "is what should always be whenever an issue elicits much interests in our streets."
However, for those who tend to argue that there is more than one side to any story, the presidential revelation is necessary but not sufficient. They want to know when did this Board meet. Who was there? Was their decision tied, in any way, with the actions of TRA officials who were fired last year and the one who was transferred earlier this year after a computer was reported as stolen? More significantly, what 'professional rationale' informed their decision?

The 'inquisitive' among them have gone out of their way to read the Tanzania Revenue Authority Act. Therein, they found out that the TRA Board 'shall consists of" a chair "appointed by the President on the recommendation of the Minister"; "the Permanent Secretary of the Ministry of Finance of the Union Government"; "the Principal Secretary of the Ministry of Finance of the Zanzibar Government"; "the Governor of the Bank of Tanzania [BOT]"; "the Commissioner-General of the Authority"; "the Permanent Secretary of the Ministry of Planning". Who else do they find in there?

Well, "and four other members appointed by the Minister with professional knowledge and experience in finance, commerce, economics or law from among institutions of financial, commercial, legal or economic nature having no vested interests in the Authority." Hence the question: If all of these were there, what financial 'professionalism' and fiduciary 'prudence' informed them?
Curiously, The Governor of BOT, Professor Benno Ndulu, has just been (mis)quoted in Mwananchi as saying that there is nothing (legally) 'wrong' with putting money in a fixed deposit account. One cannot help but wonder whether he was also part and parcel of TRA's Board meeting that approved the depositing of the Tsh 26 Billion. What is more puzzling is whether, 'technically speaking', the dissolution of the Board has to do with the chair and "four other members"given that the other senior government officials have not been fired from their other posts. This query is particularly relevant given that the second schedule of the TRA Act stipulates that "five members shall form a quorum for a meeting of the Board."

Such questions brings us back to where we began. If public information sharing is anchored on informing the citizenry about important matters in our polity as aptly provided in Article 18 of the Constitution of the United Republic of Tanzania, why should it remain fragmented? Is it because some issues are 'too sensitive' and hence disclosing them is 'a matter of national security'? How does one decide what information is for 'public consumption'? Does the government's communication strategy include a set of clear criteria for sharing information that is for 'public interest' in a timely way?

Or do we simply have to rely on the good will and discretion of the personality in the presidency? Must access to public information  depend on whenever he/she feels like revealing the 'truth', be it in the middle of a celebratory speech on a graduation ceremony or anywhere else? Is it a matter of spontaneity or constitutionality?
Interestingly, yesterday we had a chance to listen, 'live', to a phone call between President Magufuli and Dar es Salaam's Regional Commissioner, Paul Makonda. Populist rhetorics and stunts aside, this public event underscored the need for 'clear communication'.  When they were closing their conversation, the President said: 

"Kwa sababu saa zingine, ufafanuzi huu ungekuwa umeshatolewa mapema, wananchi wasingekuwa na sababu ya kuja kuuliza haya maswali" [Because, alternatively, if such clarifications were presented earlier own, citizens would not had any reasons to come and ask these questions]

That is exactly what we need from the Presidency: Clarity.
 

Saturday, November 12, 2016

Kioo cha Trump Hakidanganyi!

KIOO CHA TRUMP HAKIDANGANYI!

Muhidin J. Shangwe

Watanzania kama walivyo watu wengine duniani tumefuatilia uchaguzi wa Marekani ambao umemalizika kwa mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump, kumshinda mpinzani wake Hillary Clinton wa chama cha Democrats. Shauku na wajibu wa kufuatilia uchaguzi wa Marekani hutokana na sababu kadhaa, lakini kubwa ni kwamba utawala wa Marekani una athari kwa dunia nzima. Kwa mfano, mara tu baada ya Trump kutanganzwa mshindi tayari kuna hofu juu ya hatima ya Mkataba wa Hali ya Hewa wa Paris ambao umeungwa mkono na mataifa makubwa ikiwemo Marekani. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema lau kama Watanzania tungekuwa na nafasi ya kupiga kura Marekani basi tungeichangamkia kwa sababu matokeo yake yana athari kwetu! 

Lakini kuna sababu nyingine. Marekani ni taifa kubwa na la kupigiwa mfano katika nyanja mbali mbali hasa maendeleo ya kiuchumi, kijeshi, kisayansi na kiteknolojia. Marekani pia hupigiwa mfano kwa mfumo wake wa kidemokrasia ambao unaonekana umejengwa katika misingi ya haki na uhuru wa raia wake. Ni kwa sababu hizi, na nyinginezo, nguvu-laini (soft power) ya taifa hili ni kubwa. Nguvu-laini ni uwezo wa nchi fulani kuvutia nchi nyingine kwa sababu tu mifumo yake ya kisiasa, mienendo yake ndani na nje, na utamaduni wake huwafanya watu na serikali za mataifa mengine kuvutiwa hata kuwa tayari kuyafanya yale ambayo yanainufaisha nchi hiyo - wakati mwingine bila hata kuombwa kufanya hivyo! Nguvu-laini hii ni tofauti na nguvu-ngumu (hard power) ambayo ni matumizi ya nguvu za kijeshi au uchumi kufikia malengo - kwa maana ya kushurutisha wengine wakubaliane nawe hata kama hawapendi. 
Marekani ina vyote, nguvu-laini na nguvu-ngumu, hivyo basi, tunalazimika kufuatilia kinachojiri maana taifa hili ni kama “tembo ndani ya chumba” (elephant in the room) - huwezi kujifanya eti humuoni! Na kama kawaida, panapo washindani wawili basi “mashabiki” hugawanyika katika kambi mbili. Kinachofuata ni “ligi” isiyo rasmi kati ya “timu” mbili: kwa muktadha huu, ni Timu Trump v Timu Clinton. Hata kwa wale ambao ni neutral, kwa maana ya kutounga mkono upande wowote, kiuhalisia na kiubinadamu, hujikuta moyoni wakiunga mkono moja ya pande mbili. Kwa wale wenye “timu” wakati mwingine si kwamba wanavutiwa sana na mgombea mmoja bali wanaogopa zaidi matokeo ya mgombea mwingine kushinda. 

Ni kweli kwamba kampeni za uchaguzi wa Marekani mwaka huu zimekuwa ni kioja kifananacho na vipindi vya televisheni vyenye mzaha mzaha. Mapungufu ya wagombea wawili, Clinton na Trump, yameifanya Marekani kudharaulika kwa kiasi fulani na pengine kupoteza sehemu ya nguvu-laini yake duniani. Na kwamba sasa Trump ameshinda uchaguzi huo ni kioja kikubwa zaidi. Hapa China, Trump amekuwa akitumika kama kielelezo cha udhaifu wa mfumo wa demokrasia. Kwamba unawezaje kuwa na mfumo unaoruhusu mtu wa aina ya Trump kuwa mgombea wa urais, achilia mbali kushinda na kuwa rais? Swali hili naamini linaulizwa kwingineko duniani. 
Sababu za kuunga mkono “timu” moja hutofautiana. Siku mbili kabla ya uchaguzi nikiwa katika mkahawa wa chuoni kwangu kijana mmoja wa kizungu kutoka Canada alikuja kukaa nami meza moja. Tunafahamiana. Ni kijana mdogo tu wa miaka 21. Katika mazungumzo aliniuliza kuhusu uchaguzi wa Marekani na kama ninafuatilia yanayojiri. Nilimueleza kwamba, naam, nafuatilia. Kisha akaniuliza kuhusu Trump. “Unamuonaje?” Nikamjibu juu juu kwamba, he is not presidential, nikiwa na maana kwamba hana sifa za kuwa rais. Kisha nikamuuliza yeye swali hilo hilo, akasema yeye anataka Trump ashinde. Nilipohoji kwa nini akasema anampenda Trump kwa sababu "he does not give a f**k!" Hapa alikuwa anamaanisha kwamba Trump hajali!

Katika mazungumzo yetu pia aligusia hulka ya kutojali waliyo nayo watu wa Magharibi ya Mbali, akimaanisha Canada na Marekani. Akasema amejifunza mambo mengi tangu aje China, kwamba, kumbe dunia ni kubwa! Akasisitiza kwao dunia ni Canada na Marekani! 
Baada ya jibu hilo nikaona kuna umuhimu wa kumueleza kwa nini niliona Trump hafai kuwa rais. Nilimweleza kwamba kwanza kabisa ameonesha ni mtu asiye na ufahamu wa mambo mengi ya kisera kupitia mijadala mbali mbali aliyoshiriki. Ni mtu wa kusema jambo lakini hana mkakati wa kufanya jambo hilo, na wakati mwingine akibanwa hukimbilia kusema hiyo ni siri yake. Lakini kingine ni yale ambayo yalitoka kinywani mwake. Ni kauli nyingi za kuudhi na ukosefu wa heshima dhidi ya wanawake, watu wa mbari tofauti na wazungu, Waislam na hata watu wa tabaka la chini. Mawazo yake juu ya wahamiaji yanachefua, na ujenzi wa ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico ni wazo la kijuha! Ukuta ni alama ya utengano. Zipo kuta zisizoonekana kama ubaguzi wa rangi, kitabaka na kadhalika. Lakini ukuta huu wa Trump utaonekana, ukitaka kuushika utaushika. Kweli ni mtu asiyejali! 

Tukaishia hapo. 
Uchaguzi umefanyika. Toba! Donald Trump ndiye Rais-Mteule wa Marekani sasa. Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Van Jones, kutoka Shirika la Habari la CNN kwa usahihi kabisa anasema ushindi wa Trump hautokani na sababu moja. Zipo sababu za kiuchumi zitokanazo na kushindwa kwa mradi wa utandawazi, kitu ambacho kimewafanya watu wengi kukosa ajira na maisha kuwa magumu kwa ujumla. Wengine wamesema imetokana na wanasiasa wa Washington kushindwa kutimiza wajibu wao. Watu wamechoka. Wana hasira. Wameamua kutuma ujumbe kwa kumchagua mtu ambaye si mwanasiasa. Lakini kwa sababu Marekani ni jamii ya kimbari, suala la ubaguzi wa kimbari pia limetajwa. Imesemwa sasa wazungu wameamua kuchukua nchi yao! 

Isemwe pia kwamba kampeni ya Trump imeamsha hisia kali za utaifa wa Kimarekani ambao pia umechangia hisia za kibaguzi dhidi ya “wakuja” au kwa lugha nyingine wahamiaji. Vikundi vidogo vya kibaguzi vinavyojiita vya kizalendo vimepata nguvu kubwa wakati huu, shukrani kwa Trump ambaye amewaahidi “kuwarudishia nchi yao.” Moja ya vikundi hivi ni kile cha “Asimilia Tatu” ambacho kinaamini ni asilimia 3 tu ya Wamarekani wa sasa ndiyo damu yao ilishiriki vita vya ukombozi dhidi ya utawala wa Waingereza. Maana yake hao ndiyo “Wamarekani zaidi.” Wafuasi wa “Asilimia Tatu” wamekuwa wakifanya mazoezi ya kivita kuwa kutumia silaha nzito wakijiandaa kwa lolote ikiwemo kile kilichodaiwa na Trump kwamba kuna njama za yeye kuibiwa kura! 
Na Trump hajawaangusha watu wa aina ya Asilimia Tatu. Alitangaza siku ya uchaguzi kama siku ya uhuru wa Marekani, na wao wakaitika “we are taking our country back!” (tunairudisha nchi yetu mikononi mwetu!). 

Kaulimbiu kuu ya kampeni ya Trump ilikuwa kuirudisha Marekani katika hadhi yake ya ukuu (Make America Great Again!). Yapo maswali: Ni lini Marekani ilikuwa na ukuu? Kama ni miaka 30-50 iliyopita, nini ilikuwa hadhi ya watu wa makundi mbali mbali katika jamii ya Marekani kama vile wanawake na watu weusi? Je, kuifanya Marekani kuwa kuu tena kuna tafsiri gani kwa makundi haya na yale ya kihafidhina na kibaguzi? Maswali haya yatapata majibu kadiri muda unavyokwenda. 
Ushindi wa Trump umepokelewa kwa hisia tofauti na Watanzania. Wako waliofurahi na wako waliofurahi kupindukia! Hali kadhalika wapo waliofedheheshwa. Mimi ni mmoja wa waliofedheheka. Nimetaja sababu za maana ya uchaguzi wa Marekani kwa dunia. Baadhi yetu tuliamini taifa hili ambalo linaonekana limejengwa kwa misingi ya uanuwai (diversity), misingi ambayo imepata nguvu miaka ya karibuni kwa kumchagua Rais mwenye asili ya Afrika, watu wake wasingechagua mtu ambaye misimamo yake inaenda kinyume na uanuwai huo. Ni mtu ambaye aghalabu ametoa kauli zenye chembe chembe za kibaguzi, kejeli, dharau, ubabe, na mwenye kauli za kunyanyasa kijinsia. Lakini ah! Tulikosea. Wengine wametafsiri hatua kama hatua moja nyuma kwa nchi ambayo ilikuwa inaelekea kwenye mabadiliko makubwa ya kijamii. 
Baada ya ushindi wa Trump nimeanza kuwaza kuhusu Watanzania ambao wanamshabikia Trump. Je, kwa sababu ni mtu asiyejali? Ni kwa sababu wanapenda “sera” zake za kujenga ukuta kutenganisha Marekani na Mexico? Au ni kwa kudhibiti uhamiaji wa Waislam kuingia Marekani? Au wanasuuzwa moyo na kauli na mienendo yake ya kidume dume dhidi ya wanawake? Katika jamii yenye hulka za mfumo-dume, hii ni sababu ya kuvutia sana! Au ni ubabe na dhihaka dhidi ya watu wenye ulemavu? Au sasa wanaamini sera ya Marekani kwa Afrika na dunia itakuwa ya manufaa? 

Moja kati ya majibu niliyopata ni kwamba Trump “atatunyoosha” Waafrika! Ati wale viongozi wababe wa Kiafrika sasa wamepata kiboko yao na watakiona! Kumekuwa na kauli zinasombaa katika mitandao ya kijamii kwa muda mrefu sasa zikidaiwa kutoka kwa Trump, ikiwemo ile ya kwamba Waafrika ni wavivu, hawajiwezi na hivyo wanatakiwa kutawaliwa tena! Niseme kwamba sijawahi kuamini kauli hizi kwa sababu, pamoja na uzito wake, sijawahi kuziona zimeripotiwa na chanzo cha uhakika zaidi ya vyanzo vya kidaku. Kwamba Trump labda hakutoa kauli hizi lakini amesuuza waumini wa sababu hii ni kilelezo kingine cha matatizo tuliyonayo katika uwezo wetu wa kuchambua mambo! 
Lakini wapo wanaosema wanavutiwa na msimamo wa Trump na chama chake cha Republican kupinga masuala kama ya utoaji mimba na ndoa za jinsia moja. Hoja hii ya kihafidhina inasemwa kwamba ni miongoni mwa sababu zilizompa ushindi Trump baada ya kuvutia kura za waumini wa makanisa ya Kiinjili (Evangelicals). Pia kuna kundi la watu ambao “hawana habari,” wao wanampenda Trump kwa sababu tu ni wa chama pinzani na wao ni wafuasi wa vyama vya upinzani kwetu! Na wako pia wanaodai kwamba ni jambo zuri Trump kushinda kwa sababu unafiki na ujinga wa Wamarekani sasa utaonekana! Katika muda na sehemu tofauti, nami pia nimwahi kutamka sababu hii lakini si kama sababu ya msingi kumuunga mkono Trump bali kama namna ya “kufuta machozi” iwapo angeshinda. 

Ni wazi sasa kupitia Trump na mapokeo ya ushindi wake tunaweza kuona taswira yetu - ya kwamba sisi ni watu wa aina gani na tunaamini katika misingi ipi. Nihitimishe kwa kusema kwamba, kwa kupitia taswira hii tunayoiona kupitia kioo cha Trump, upo uwezekano wa akina Trump wetu kushinda chaguzi zijazo kwa kishindo! Si mwanamuziki Diamond Platinumz kaimba kwamba 'kioo hakidanganyi'?

Tuesday, November 8, 2016

Conference on African Culture and Society


Saturday, November 5, 2016

From Obama to Clinton: Déjà vu?

"For the first time having a black president coming to power, in arguably the most powerful nation, there was that sense of belief, pride. In that regard, there will be a positive legacy that here is someone who is as black as Africans who managed against all odds to get up there.... But then there is also a negative aspect, the US is still a global military power and in a way, Obama hasn’t really managed to change that. The US is still a bully, bullying people all over the world. In as much as we Africans had a black person over there, he hasn’t been able to shift the global dynamics and again what can one person do? Even some of the things that they are trying to achieve in Africa like the power lighting in Africa.... If you look at it, it is really a corporate affair  – all these American companies coming... in the case of my country Tanzania – how on earth does a small place like Ubungo, a suburb in Dar-es-Salaam where I grew up manage to host Hillary Clinton, Barrack Obama, within a space of 5 years or so? Bill Clinton, George Bush - all of them have been coming. It makes you wonder what is so special about this place. Is it really about lighting Africa, empowering Africa.... But I believe for the young black people in the US, and elsewhere in Africa, the Obama Moment will always be significant. I was following the hashtag #ObamaAndKids, you can see that the level of inspiration... even in my case I have always had a mixed feelings about the US but in the case of Obama – but with Obama it has been very different – in some instances, you had to sympathise with him – no American President has suffered the kind of racism that Obama has suffered. So, I will always have that feeling that here was someone black, inspirational, but again, he was leading a nation that is spearheading military occupations and corporate incursion into our places. My expectations at the moment are not so positive because the candidates that the US got as TOP candidates have got a lot of problems. Trump as you can see is sexist and racist. The situation – I mean the future of America seems very bleak for me. He is coming from the corporate world where whatever he is going to do if he comes into power will be along those lines – corporate imperialism, racism, sexism. They will always tend to go hand in hand in marginalizing a lot of people who don’t fit into the mainstream. Hillary seems to be relatively better than Trump but, again, if you look at all these major projects that I was talking about, the ones that have been spearheaded in Africa and elsewhere - Hillary was instrumental in them. She came to Dar-es-Salaam to push for the American companies to get this power – electricity deal in Africa. Of course, the underlying argument is that they want to light Africa but if you are lighting Africa why does it have to be American Companies? And then all these scandals that  her campaign has in terms of undermining someone [Bernie Sanders] who seems to be more progressive, I think all of them are casting some kind of  a shadow. Some people remember her husband’s [Bill Clinton] reign [for the Democrats] as a lively force compared to the Republicans, so, there are some people who hope maybe Hillary will be more like that. But based on these scandals that are coming out and what she is doing when she was Secretary of the State, I think that she is going to be just an Iron Lady who will probably make us see more of the ruthless side of America" - Chambi Chachage (@udadisi): Interviewed by Ruth Aine (@Ruthaine)

Tuesday, November 1, 2016

Mkuu wa Kaya Heri Ya Mwaka Mmoja Wa Hapa Kazi Tu

Kumbukizi ya Kwanza ya Falsafa ya ‘Hapa Kazi Tu’

Richard Mbunda


Siku hizi tumetumbukia kwenye mtego wa mipango ya muda mfupi ndio maana tunajikita kutathmini hata siku 100 tu za Rais mpya madarakani! Wanazuoni wanasema utaratibu huu ulianza tangu enzi za Napoleoni, lakini ulitamalaki zaidi kuanzia wakati wa Rais Franklin Roosevelt wa Marekani mwaka 1933 hata sasa. Japo siku 100 zinaweza kutupa mwelekeo wa viongozi na falsafa zao, walakini kipimo sahihi cha kiongozi mpya si budi kiwe mwaka mmoja na sio miezi kadhaa tu kwa kuzingatia uzito wa kazi yenyewe. NIONYE juu ya mipango ya muda mfupi kwani inatufanya tusahau ya muda mrefu. Kwa mfano, kuna barabara zinadumu mwaka mmoja tu kisha tunarudia tena ujenzi kitu ambacho kinatunyima uwekezaji wenye tija maeneo mengine. Vivyo hivyo, tunakosa kufanya uwekezaji wa muda mrefu katika rasilimali watu n.k.

Mwaka mmoja wa Ofisi Kuu kwa Mkuu wa Kaya uliadhimishwa sambamba na siku yake ya kuzaliwa. Hata hivyo kuna gazeti moja limeandika kuwa majukumu yalimfanya Mkuu wa Kaya asahau siku yake ya kuzaliwa. Hii inatuonyesha ni jinsi gani Tanzania ilivyo akilini mwa Mkuu wa Kaya kuliko kumbukumbu ya kuzaliwa kwake. Nadhani pia ameanza kuwapa uhalisia wa mambo wale waliokuwa wanakesha kuifikiria Ikulu wakidhani ni pahala pa kugonga cheers tu! Naam, ilitushangaza kidogo pale ambapo kila mtu tu alidhani anaweza kuvaa viatu vya ukuu wa kaya. Naamini mpaka aje atoke madarakani watu watajiuliza mara mbilimbili kama haswaaa wanaweza kuvaa viatu vyake.

Mkuu wa Kaya, umetimiza mwaka mmoja ofisini katika ngazi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi. Leo sitazungumzia hatua yako ya kuzuia shughuli za kisiasa bila sababu ya msingi, au ile hotuba yako iliyoleta mtafaruku kule Zanzibar, bali nikiri tu kuwa katika kipindi chako cha mwaka mmoja kila Mtanzania hata wapinzani wako kwa namna moja au nyingine wameridhika na utendaji wako. Wino umemwagwa vya kutosha kuelezea mafanikio yako ndani na nje ya mipaka yetu. Umeleta heshima ya kazi katika utumishi wa umma na umekuwa mfano wa kuigwa katika utendaji kazi. Pia umewafanya wafanyakazi wa kawaida kujawa na hisia za uzalendo na moyo wa kuitumikia nchi yao.

Umeleta pia mabadiliko katika matumizi ya mali ya umma. Mimi huwa napingana na wale wanaosema unabana matumizi, si kweli bali umeondoa matumizi mabaya. Matumizi ya bilioni mbili kusherehekea siku ya uhuru ni matumizi mabaya ya pesa za umma. Kutenga bilioni mbili kwa ajili ya semina elekezi kwa mawaziri ni matumizi mabaya ya pesa za umma. Kusafirisha viongozi wote wa kitaifa wakahudhuria kuzimwa kwa Mwenge wa Uhuru ni matumizi mabaya ya rasilimali watu na pesa za umma. Hatua nzuri ulizichukua na Tanzania ikapongeza. Lakini naomba usiishie hapo. Maana ukiondoka kesho matumizi haya yasiyo na tija yanaweza kurudishwa na watu wasio na nia njema na Tanzania huko mbeleni. Ni muda muafaka sasa mambo haya tuyawekee KANUNI za kuyazuia. Ukiamua linawezekana.

Mheshimiwa Mkuu wa Kaya, wafanyakazi hewa, wanafunzi hewa na miradi hewa umeishughulikia kwa umahiri mkubwa. Vita hii uliyoianzisha imekuwa muhimu sana kwani taifa limepoteza pesa mingi katika ghiliba hizi za ‘mabosi’ wa vitengo vya umma. Hili nalo tuliundie mfumo. Wakishasafisha hao wachafuzi na majizi ya pesa za umma itatupasa sasa tuwe na kanzidata (database) moja itakayomulika wafanyakazi wote na taarifa zao za kuachishwa kazi au vifo.

Mkuu wa Kaya, jitihada zako kuhusu kupambana na rushwa na uporwaji wa mali ya umma ni wa kupongezwa sana. Umeacha gumzo kila kona kwa jinsi ulivyobana mianya na zile njia za panya… kwa wale walioiona nchi hii kama shamba la bibi. Kusema kweli huku mtaani hali si hali. Lakini ni ukweli usiofichika tulizoea kuishi kiujanja ujanja! Hatuna budi kuisoma namba. Hatua yako ya kuanzishwa mahakama ya majizi na mafisadi itakuwa ya mfano kwa Afrika, na naamini Afrika na sio Tanzania pekee itakukumbuka kwa hatua hii.

Mkuu wa Kaya, watu sasa wanalipa kodi, na watu wanadai risiti. Lakini, niruhusu nikunong’oneze kidogo katika hili. Kuna mapungufu kadhaa kwenye kale kamashine ka kutolea risiti (EFD) kwani hakana maelezo (description) ya bidhaa ulizochukua, bali kanatoa jumla tu. Na hawa ndugu wafanyabishara wamegundua mtindo wa kupunguza tarakimu moja tu, lakini madhara yake unayajua. Kwa mfano, badala ya kutoa risiti ya shilingi 500,000 watatoa risiti ya shilingi 50,000.

Mkuu wa Kaya, mimi binafsi nimefurahishwa na teuzi zako, hasa wa Msaidizi wako Mkuu yule Waingereza wanamuita Premier. Natambua ya kuwa, kipimo cha kwanza cha kiongozi ni namna anavyopanga safu yake ya wasaidizi. Kinachonifurahisha zaidi ni jinsi ulivyowapoteza maboya watu katika uteuzi wako. Wengi hawakumdhania, lakini Premier amekuwa nguzo imara katika utawala wako. Kwa kuzingatia hulka, mawasiliano yake kwa umma, na utekelezaji wa majukumu yake huyu Premier ni mfano wa kuigwa. Amekuwa chachu ya utekelezaji wa kaulimbiu ya "Hapa Kazi Tu", lakini pia anaheshimika kwa umma wa Watanzania. Ukitaka ushahidi nitakupatia…... nikunong’oneze tu, Premier ni kiongozi pekee ambaye hatajwi kwa mizaha au kejeli katika mitandao ya kijamii hasa kuleee unakokujua.

NI MWAKA MMOJA SASA: Mheshimiwa Mkuu wa Kaya, katika utekelezaji wa ilani yako ya uchaguzi mimi nakunwa sana na mipango ya ujenzi wa reli ‘standard gauge’. Mimi naamini reli itachangamsha sana uchumi wetu hasa kama Dodoma unakohamishia makao yako utaifanya kuwa HUB ikaunganishwa na reli kwenda Pwani, Kanda ya Ziwa, Kusini, Rukwa mpaka Kigoma. Kama nchi tumekuwa na utegemezi wa hali ya juu wa barabara kusafirisha abiria na mizigo. Ndio maana ajali zinaongezeka kila leo na kwa kiasi kikubwa uchumi wetu unaathiriwa. Wakulima kule kijijini wamekosa faida katika mazao yao kwa kuwa miundombinu ya usafirishaji ni mibovu, na japo mazao yao yanahitajika kwa wingi sehemu zinginezo lakini wanakatishwa tamaa na suala la usafirishaji. Mkuu wa Kaya, naamini utaitumikia nchi hii miaka 10. Hivyo basi, ujenzi wa reli, ambao naamini ni gharama kubwa, na uwe nembo ya utawala wako uliotukuka.

Mipango yako ya mabadiliko nilipenda pia imulike jambo hili linalohusu SHERIA. Mkuu wa Kaya, Bunge letu linapanuka kila mwaka. Kwa Mamlaka ya NEC na ZEC kule Zanzibar kila baada ya miaka kadhaa wanafanya mapitio na kuona ni jinsi gani wabadili mipaka ya majimbo kitu ambacho kimekuwa kikiongeza idadi ya majimbo. Mkuu wa Kaya utakubaliana na mimi kuwa hatuhitaji wabunge 500 kulifanya bunge liwe wakilishi au lifanye kazi yake ya kutunga sheria na kuisimamia serikali kwa ufasaha! Na tukitaka uwakilishi kwa idadi ya watu basi China na India zingekuwa wa wabunge walao elfu kumi. Huku ni kuongeza gharama na ugumu wa maisha ya mtanzania wa kawaida bila sababu. Mkuu wa Kaya,  unaweza kutukomboa katika mwelekeo huu. Tunapaswa kuweka STOP uongezwaji wa majimbo ya Ubunge na viti maalumu. Mimi nilipenda sana pendekezo la Tume ya Jaji Warioba, iliyopendekeza kila Mkoa wa Tanzania Bara na Wilaya za Zanzibar kutoa wabunge wawili, wa kike na wa kiume, na Rais wa Jamhuri achague wabunge watano tu. Kwa mfano, hakuna sababu ya eneo la watu milioni moja na laki mbili tu kama Zanzibar wawe na majimbo 54 ya uwakilishi na 50 ya Ubunge kama ilivyokuwa 2015. Hatuwezi kupiga hatua za kimaendeleo kama tuna kada kubwa ya viongozi wanaoongeza matumizi kuliko uwekezaji.

MICHEZO: Mkuu wa Kaya, Watanzania wanapenda michezo. Utaliona hili siku Timu ya Taifa ikicheza mechi na timu kubwa au hata Yanga na Simba wanapokutana. Naamini pia unapenda michezo si ndio maana ukaomba kwa Mfalme wa Morocco uwanja mkubwa ujengwe Dodoma? Sisi ni nchi ya watu wanaokaribia miloni 50 lakini hatujajiendeleza kimichezo. Mzee Mwinyi alishawahi kutuita kichwa cha mwendawazimu… tumeendelea kuwa hivyo. Wakati wa michuano ya Olympic tulikuwa na wawakilishi wachache na aliyefahamika zaidi ni mwanariadha. Japo hakuleta medali lakini watanzania tulilipuka kwa furaha ya uwakilishi wake. Tuwekeze katika elimu ya michezo kama mkakati wa Serikali. Tujenge Vituo vya Michezo kwa kuanzia angalau katika kila kanda. Vituo hivi vihusishe michezo yote kuanzia mpira wa miguu, netball, bwawa la kuogelea, tennis, basketball, netball na cricket. Tunaweza kutumia vituo hivi kulea vipaji katika umri wa miaka 14 na kuendelea na tukapata professionals katika michezo mbalimbali. Vituo hivi vya michezo vikijengwa karibu na shule zilizopo vijana hawa watahudhuria madarasa ya kawaida na baadae kushiriki katika programu zao za michezo wakiwa hosteli maalum za vituo hivyo. Huu ni uwekezaji kwa kuwa vijana hawa wakiiva wataiingizia nchi mapato makubwa sana. Siamini pia kama gharama itakuwa kubwa zaidi. Tunayo mifano mizuri ya akina Mbwana Samatta, tunahitaji kutengeneza kama 1000 wengine achilia mbali watakaocheza hapa nchini. Ivory Coast ina wachezaji karibia kila nchi duniani ikiwemo Israel na hapa Tanzania, kwa nini sisi hatuna huko professionals huko nje?

Happy Birthday Mkuu wa Kaya!

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP