Sunday, March 19, 2017

Mdahalo wa Kitaifa kuhusu Lugha ya Kufundishia


Karibuni katika Mdahalo (Debate) wa Kitaifa utakaofanyika Nkrumah siku ya Jumapili tangu saa 8 mchana hadi saa 12 jioni.

Kwa muda mrefu sasa, tumekuwa tukiandika, tukijadiliana na kulumbana kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili. Iwe katika kuitumia kama lugha ya kufundishia, au kutolea hotuba katika mikutano au hata mawasiliano rasmi katika maofisi ya Serikali na Mashirika yake n.k.

Katika mijadala hiyo kuna wanaosema kuwa, tutumie Kiswahili na kuna wanaosema tuachane na Kiswahili tutumie Kiingereza.

Siku ya Jumapili tarehe 19, ni mara ya kwanza ambapo pande mbili zinazokinzana zitakutana ili kubishana kwa HOJA.
Ukumbi wa Nkrumah umekuwa na sifa ya kuwa na mijadala yenye kuleta tija na mabadiliko mioyoni au vichwani mwa watu, wawe viongozi au waongozwaji. Karibu ili ushiriki katika utamaduni huu wa Nkrumah na utoe mchango wako, kwa hoja za kitaaluma.

Kwa wale ambao mtashindwa, Mdahalo huo utarushwa mubashara na Vyombo vyetu vya habari vya TBC, ITV, Azam TV, Star TV, na Clouds, ikiwa ni pamoja na radio zake.

Karibuni

Aldin

Mratibu

Prof. Aldin K. Mutembei (PhD) 
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili 
Kampasi ya Mwalimu J.K. Nyerere 
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP