Wednesday, April 12, 2017

Twaandika Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi


Taasisi ya Usomaji na Maendeleo – Soma, inaandaa warsha ya uandishi juu ya harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi itakayofanyika Mkahawa wa Vitabu Soma, Mikocheni, Dar es Salaam tarehe 4/5/2017—6/5/2017. Tunakaribisha maombi ya kushiriki kutoka kwa: wanaharakati wachanga na wakongwe wa ukombozi wa wanawake ambao wameanza kuandika au wanajiandaa kuandika juu ya harakati hizo hapa Tanzania. Waombaji wawe ni viongozi, wafanyakazi au wanachama wa taasisi/shirika linalojishughulisha na harakati za ukombozi na utetezi wa haki za wanawake; au wanaharakati binafsi wanaoshirikiana na mashirika/taasisi, mitandao au vikundi visivyo rasmi katika michakato ya harakati hizi. 

Warsha hii ambayo imepewa jina la ‘Twaandika Harakati za Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi’ ni mwendelezo wa mchakato wa uandishi wa historia ya wanawake unao- fanywa kwa pamoja na mashirika kadhaa yanayofanya harakati za usawa wa jinsia na utetezi wa haki za wanawake. Makusudi ya warsha hii ni kutoa fursa kwa rika mbili za wanaharakati za ukombozi na utetezi wa haki za wanawake kubadilishana mawazo na uzoefu juu ya hatua zilizofikiwa katika jitihada za kuleta usawa wa jinsia, ushiriki wao katika jitihada hizo; warsha inalenga pia kukuza stadi za uandishi unaotokana na tafiti au uzoefu, zilizoandikwa kifasihi au kitaaluma. Washiriki wataandika juu ya harakati za kuleta usawa wa jinsia na ujenzi wa vuguvugu la ukombozi wa wanawake kimapinduzi; iwe ni: simulizi binafsi na za pamoja za jinsi mlivyojitoa kwa ajili ya harakati hizi, mafanikio yenu, ngano za kukata tamaa/kuvunjika moyo kutokana na misukosuko na mwitikio hasi, za ustahimilivu na za mitafaruku inayoambatana na mikiki ya maisha ya uanaharakati katika muktadha ambao daima ni kigeugeu. 

Washiriki wanahimizwa kujikita kwenye maeneo yenye utata na yalio wekewa miiko kama vile ujinsia (mf. mfumodume unavyoathiri mtazamo wa jamii kuhusu mahusiano ya ngono na utambulisho wa ke na me); pamoja na aina anuai za uhafidhina. 
Warsha hii ya siku tatu itatumia njia za kujifunza kwa vitendo na kwa maelekezo ya kitaalam ya misingi na mbinu za uandishi wa kazi za kubuni na zisizo za kubuni kulingana na mahitaji halisi ya washiriki kama yatakavyojidhihirisha kwenye taarifa zitakazotolewa kwenye fomu ya maombi. Baada ya mafunzo kila mshiriki ataendelea kupata mwongozo na mrejesho wa kazi yake kutoka kwa mwandishi mahiri atakayepangiwa kumsaidia kukamilisha hatua ya kazi yake kama alivyojipangia.
Maelekezo ya jinsi ya kutuma maombi yametolewa kwenye fomu ya maombi. http://www.somabookcafe.com/applica....Siku ya mwisho ya kupokea maombi ni Tarehe 20/04/2017. Washiriki watakaochaguliwa watajulishwa kwa barua pepe. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa barua pepe info@somabookcafe.com au simu namba 0673 014 071

Watakaochaguliwa kushiriki watajulishwa kwa barua pepe 
Writing Feminist Struggles Workshop—call for participants 
E&D Readership and Development Agency—Soma, has secured funding to organize a feminist writing workshop planned to take place at Soma Book Cafe in Mikocheni, Dar es Salaam on 4 – 6 May 2017

We would therefore like to invite application for participation from: young and seasoned feminists who are in the process of/or are planning a writing project depicting feminist struggles in Tanzania. They may be leaders, staff or members of a women’s rights organization; or individual feminists affiliated to a formal or informal feminist process and/or activist network. 

The workshop, titled ‘Writing Feminist Struggles’ is meant to contribute to the ongoing ‘her- story’ documentation process currently undertaken by a coalition of various feminist and women’s rights organizations. It is specially designed to provide space for participants from two generations of feminist activist movement and women’s rights defenders to share insights on strides made in the struggles for gender equality and experiences of being a part of those struggles; as well as enhance their skills and resolve to write research and experience based literature on women’s struggle for gender transformation and feminist movement building in fiction and non-fiction. Stories will include but not limited to: ‘tales of individual and collective sacrifice, burn out, success, backlash, resilience and related complexities of activist life’ within a complex and ever changing terrain within which those struggles have taken place over time. Participants are encouraged to broach taboo subjects such as sexuality (including heteronormativity and patriarchal femininity/masculinity) and fundamentalism of various shades. 

The three-day workshop will combine learning by doing and reading into creative techniques for fiction and non fiction customized to target special writing experience that will be appraised from the participants’ applications. The workshops will be followed by a one on one coaching to assist authors to complete their writing projects/or reach a planned milestone. 

Application details are contained in an online application form found on this link http://www.somabookcafe.com/applica...

Deadline for receiving applications is mid- night of 20th April 2017. You may contact us on info@somabookcafe.com or 0673014071 for further information. 

Accepted applicants will be notified by email.

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP